Zuia ukeketaji kwa mtoto wa kike: Wazazi na jamii tushirikiane

Jemmie

JF-Expert Member
Mar 6, 2018
216
285
Ukeketaji limekuwa janga kubwa katika jamii. Na kila ifikapo February 6, nchi ya Tanzania huungana na mataifa karibu yote ulmwenguni kuadhimisha siku ya kupinga ukeketaji. Historia ya ukeketaji imeendelea kuwa tishio kwa takribani karne 21 sasa. Historia inaonyesha kuwa katika kuthamini kwa kina madhara ya ukeketaji kwa wasichana na wanawake katika jamii. Mwaka 2003, baraza la umoja wa mataifa liliidhinisha tarehe 6 February kuwa ndiyo siku ya maadhimisho yake.

Ukeketaji ni kitendo kinachohusisha kukata au kuharibu sehemu ya uke wa mwanamke au msichana kwa sababu zisizo za kisayansi, kitendo hiki pia hujulikana kama TOHARA kwa mwanamke ambacho hutekelezwa kwa sababu za kimila au kijadi kuna aina mbali mbali za ukeketaji katika jamii zetu.
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO) imeelezea aina kuu nne za ukeketaji zinazofahamika:-

1. Ukeketaji unaohusisha kutoa sehemu fulani za uke.
2. Kutoa sehemu nzima ya eneo hilo
3. kutoa sehemu za ndani.
4. ukataji wa sehemu yoyote ya uke.

Aina zote hizi ni mbaya kwasababu humsababishia maumivu makali mwanamke anaekeketwa. Kwa Tanzania aina ya 1&2 hutumika zaidi.
jamii zinazoendeleza ukeketaji ni jamii zilizotawaliwa na mfumo dume.

ATHARI Zinazotokana na UKEKETAJI:-
1. kupata athari za kisaikolojia kama msongo wa mawazo.
2. kuongezeka kwa vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
3. Kifo wakati wa kujifungua au magonjwa kama ukimwi
4. Kovu la kudumu sehemu za siri hivyo kusababisha uke kushindwa kutanuka na kupasuka wakati wa kujifungua
5. Kutokufurahia tendo la ndoa na ugumba.

Kwa mujibu wa ripoti ya Tanzania Demographic Health Survey and Malaria Indicator Survey TDHS, ya mwaka 2015 na 2016 mikoa inayoongoza kwa ukeketaji Tanzania ni;-


1074264

Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuboresha sheria na sera kwa lengo la kukabiliana na ukeketaji na kuwawajibisha wote wanaoendeleza mila hiyo kandamizi kwa watoto wa kike na wananwake.

Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 emeendelea kusimamia masalhi mapana ya mtoto bila kubagua jinsia, sera ya elimu ya mwaka 2015 imekataza kila aina ya unyanyasaji wa mtoto wa kike na kutambua misingi ya haki na usawa kwa wote wa kike na wakiume.
 
Mbona Ukeketaji Ni Mila Nzuri? Inatunza Heshima Ya Mwanamke Anakuwa Mtulivu Na Ndoa Yake Daima. Kuipinga Mila Ya Kukeketa Wanawake Ni Mmomonyoko Wa Maadili Ya Jamii. Mila Imekuwepo Kwa Karne Nyingi, Iweje Ionekane Mbaya? Inamuweka Mwanamke Kuwa Msafi.
 
Back
Top Bottom