Zuhura Yunus BBC Swahili dira ya dunia

Zuhura Yunus BBC Swahili dira ya dunia

View attachment 182362
View attachment 182363
Mtangazaji wa kwanza Mwanamke BBC Swahili TV Nimependa Sauti yake na utangazaji wake kwenye TV na Redio safi sana. Kwa hakika BBC swahili Hawajakosea kumpa kutangaza kwenye Television mpaka raha.


Kweli unampenda Zuhura, yaani mpaka umeji-inamia ukilia kwa ajili yake? I hope anakusikia huko aliko aje kukufariji.
 
Hivi huyu Zuhura Yunus ni Mtanzania au ni kutoka Mombasa? Na kuna mwingine anaitwa Mariam Omary, nae ni Mtanzania au kutoka Mombasa?
Ni Tanzania na Mombasa pekee unaweza kupata Kiswahili fasaha vile
Mimi namfahamu mariam omary, yeye ni mkenya anatoka mombasa na jina lake hasa ni miriam lyambila, sasa akasilimu kuwa mwislamu alipoolewaa na mwislamu, zuhura yunus nasikia ni mtanzania ila alisomea mbale university uganda
 
Hao wote Mkuu ni kutoka Mombasa, Kenya.
Siyo kweli, haya ni maelezo ya Zuhura mwenyewe
" Zuhura: Mimi ni Mtanzania, ni wa pili kati ya watoto watatu na ni wa kike pekee. Kaka yangu anaitwa Suwedi na mdogo wangu Bashari. Baba yangu alikuwa mwanajeshi na alifariki dunia mwaka 1995 akiwa na cheo cha Kanali, akiitwa Kanali Yunus Abdallah. Mama yangu ni mstaafu na ni mtaalamu wa kilimo mwenye Shahada ya Uzamili ya Agronomy aliyohitimu Urusi. Alistaafu akiwa anafanya kazi Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
Nimesoma shule za sekondari Jangwani na Weruweru. Shahada yangu ya kwanza ni kutoka Chuo Kikuu cha Mbale, nchini Uganda na ya pili ni kutoka Chuo Kikuu cha Leicester, Uingereza."
 
Back
Top Bottom