Eng Inc
JF-Expert Member
- Feb 3, 2017
- 631
- 944
Wakuu habari za muda huu? Natumaini mmeshinda salama.
Niende moja kwa moja kwa nilichotaka kuzungumze japo kwa ufupi.
Mimi ni kijana niliyekuwa nikihangaika kutafuta fursa mbalimbali za kujiajiri au kuajiriwa sasa kwa bahati nzuri au mbaya nikakutana na rafiki yangu mmoja wa karibu ambaye huwa tunashauriana mambo mengi ndipo akanishauri niwe napitia pitia kwenye website ya Zoom Tanzania.
Nilifanya hivyo mara kadhaa pindi nilipoona kuna nafasi inatangazwa inayohusiana na taaluma yangu yani Civil Engineering au taaluma zinazohusiana na hiyo. Sasa zaidi ya mara tano nimetuma maombi sambamba na kutuma CV yangu kwenye kampuni tafauti kilichokua kinatokea kila nikituma maombi haitapita wiki moja kuna mtu atatokea na kujitambulisha Nanukuu:
Mimi ni Mr fulani (majina na namba zao ninazo nayahifadhi) wataanza kwa kusema tupo tunapitia CV yako na ni nzuri sana, nataka nikusaidie upate kazi hii kwa masharti yafuatayo: mshahara 1.3m take home utanipa laki 3 kwenye mshahara wako wa kwanza ila tuma elfu 20 tigopesa kwenye hii namba kabla ya saa 10 leo jioni nitakupigia nikitoka kikaoni.
Ikabidi nimuulize jamaa yangu kuhusiana na hiyo ishu akasema ni kweli kuna matapeli mule ila aliwasiliana na mmoja wa ma IT wa Zoom Tanzania akasema hakuna matapeli wewe uwe unatuma tu maombi.
Kama kuna yeyote ameshakutana na kitu kama hiki ebu na yeye atoe neno maana mimi wananikera sana hawa jamaa.
Maombi yangu:
Sina lengo baya la kuchafua brand yenu ila huu ujinga umenichosha sasa na kunichefua sana.
Kama kweli mpo makini na huduma zenu nyinyi zoom tanzania ebu tokomezeni huu upuuzi ambao sio tu mimi bali wapo rafiki zangu wa karibu wamesema zoom tanzania ni matapeli na hawawezi kuingia tena hivyo vyombo husika ichunguze huu mtandao maana wenyewe wananufaika kwa watu kuingia uku wengine wanatapeliwa kwa ujinga huu.