Zondeni Veronica Sobukwe mama wa taifa aliyesahaulika nchini Africa ya kusini

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
574
1,000
Afrika ilipoteza wana mapambano wawili kwa mpigo, Afrika imeshudia kumpoteza Kofi Annan Katibu Mkuu wa kwanza mweusi kutoka Afrika hii ni pigo kwa wana mapambano wa haki duniani. Lakini mapema jumatano huko Afrika kusini ilimpoteza mwanamama wa ukombozi na mpigania uhuru wa taifa hilo. Sio mwingine bali ni Mama Veronica Sobukwe.

Zondeni Veronica Sobukwe alizaliwa tarehe 27 Julai 1927 na kufariki tarehe 14 Agosti 2018 alikuwa ni mojawapo ya viongozi na alama ya kupambana dhidi ya ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini, Zondeni Veronica Sobukwe alikuwa ni mjane wa rais wa moja ya vyama vya ukombozi kilicho itwa Pan-African Congress (PAC) aliyeitwa Robert Mangaliso Sobukwe.

Veronica alizaliwa Julai 27,1927, huko Hlobane, Jimbo la KwaZulu-Natal. Yeye na Sobukwe walikutana katika mapambano ya kupinga ubaguzi wa rangi uliukuwa umetahamaraki taifa hilo hata hivyo historia yao wawili hawa ilikuwa ni "upendo kwanza", kama ambavyo Veronica alisema miaka kadhaa iliyopita.

Wakati huo, 1949, Sobukwe alikuwa rais wa Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Fort Hare aliko kuwa akisoma masomo ya sheria wakati Veronica alikuwa muuguzi wa mafunzo katika Hospitali ya Victoria huko Lovedale. Wakati huo wauguzi katika hospitali walikuwa wameitisha mgomo wa kazi na juu ya usimamizi wa mahospitali wakati huo, na Veronica alikuwa mmoja wa viongozi katika mgomo huo ambao ulipata tahadhari ya Sobukwe na viongozi wengine wa wanafunzi.

Katika wito wake kwa wanafunzi Veronica Sobukwe alisema: "watumishi wa hospitali ni sehemu ya mapambano mapana. Tunapaswa kupigana kwa kuleta uhuru, kwa haki ya kuzitoa roho zetu wenyewe na tunapaswa kulipa deni hili kwa vizazi vyetu."

Kwa sababu ya kuhusika kwake katika mgomo huo, Veronica alifukuzwa kutoka Chuo cha Lovedale yeye na rafiki yake Thandiwe Moletsane (huyu baadaye aliolewa na Mheshimiwa Makiwane) walikwenda Johannesburg baada ya kuamua na kujiunga na umoja wa Vijana wa ANC ya tawi la Fort Hare pamoja na kuandika walaka kwa Walter Sisulu juu kuomba kuungwa mkono ya tahadhari yake ya mgomo wa wauguzi huko Alice.

Kipindi hicho Ilikuwa ni wakati mgumu Sana na wa majaribio ambayo kati yao kila mmoja alikamatwa na kua mfungwa mara kadhaa ikiwa ni pamoja na mwaka wa 1950.

Hata hivyo Veronica alimsaidia mumewe katika harakati zote nchini kote, ikiwa ni pamoja na Ile Ibada ya kuomba pamoja Machi 21, 1960,(iliyoitwa Ibada ya taifa kwa mapambano) kipindi ambacho Sobukwe alipojitoa kupambana wazi na kukamatwa kwa kupinga sheria za ubaguzi wa rangi ambazo kipindi hicho serekali ya makaburu walikuwa wamezipitisha hasa sheria ya kutembea na kitambulisho kwa waafrika weusi (pass law).

Hata hivyo Sobukwe Alihukumiwa miaka mitatu gerezani kwa ajili ya uchochezi, lakini serikali ya ubaguzi wa rangi ilikataa kumfungua baada ya muda wake wa jela kumalizika. Serikali badala yake ilifanya "Kifungo cha Sobukwe" kuwa kifungo haramu Kwani Sobukwe aliwekwa jela kwa muda mrefu bila utaratibu halali kama makaburu walivyotaka. Sobukwe alipelekwa Robben Island mwaka wa 1963 na akawekwa mbali na wafungwa wengine maana serikali ya ubaguzi wa rangi ilimuona kuwa mtu hatari sana.

Miaka ishirini na moja iliyopita Veronica alielezea maumivu aliyopata ya kutengana na mumewe na hali aliyokuwa nayo kwa watoto wao. Pia kipindi hicho alipata unyanyasaji na kuteseka kutokana na Sobukwe kuwa jela. Hata hivyo maelezo haya yote yalitolewa kwa umma wakati Veronica alipoonekana hadharani mbele ya Tume ya Kweli na Upatanisho (TRC) Mei 12, 1997, katika jitihada zake za kupata ukweli kuhusu sababu za kifo cha mumewe.

Viongozi wengi na wajumbe walisikiliza kwa hofu pale Veronica alivyowaambia jinsi mamlaka ya ubaguzi wa rangi walikataa mumewe kupatiwa huduma ya upimaji na matibabu na kumuacha na ugonjwa akiwa gerezani. Mwaka wa 1964, afya ya Sobukwe ilizoofu sana ni wakati huo mapendekezo ya maafisa magereza waliliomba Bunge kuzunguza kutolewa kwake, lakini Bunge hilo la kibaguzi lilikataa.

"Mnamo Februari 1966, Sobukwe walimpeleka Karl Bremer kwenye Hospitali ya Bellville, Anasema Veronica kuwa wao awakuambia chochote juu ya kupatiwa matibabu kwa Sobukwe. Veronica anaendelea kusema "Nikasikia habari hii wakati aliporudi kutoka Karl Bremer kuwa Alikubaliwa kwenda kutibiwa na maafisa wa magereza chini ya jina la uongo".

Veronica anaendelea kusema kuwa hata alipozuru kwenye gerezani hilo hawa kuwa na ushauri na yeye. Inasemekana kuwa Sobukwe alipelekwa Robben Island na wakati Veronica alipomtembelea Sobukwe alilalamika kuwa chakula chake kilikua anakikuta na glasi zilizovunjwa maelezo yote hayo Veronica aliiambia TRC.

"Unamaanisha glasi zilizovunjika katika chakula chake?" Mmoja wa wakuu aliuliza "Ndiyo, katika chakula chake. Alikuwa peke yake wakati huo ... Kuna vitu vilivyofanyika kwa watu jela wakati huo na nina uhakika kwamba walifanya mambo haya kwa mume wangu, kwa sababu alikuwa peke yake katika chumba cha gereza hilo." Veronica alisema.

Baada ya kutolewa kwake gerezani ghafla Mei 1969, polisi waliendelea kumshtaki na kumuandama yeye Sobukwe na familia yake. Walikataa kuruhusu Sobukwe kwenda ng'ambo kupata matibabu ya kansa iliyokuwa imempata. Pia walimkatalia kumpatia pasipoti kuondoka nchini baada ya kupatikana kwa nafasi ya kufundisha (lectureship) katika Chuo Kikuu cha Wisconsin nchini Marekani.

Harakati za Veronica kama mwanamke huwezi kuzipata ndani ya ANC Maana ndani ya ANC hakuna mwanamke aliwahi kuteswa kama yeye kwani hata hivyo wapo walioamini kwamba taifa la Afrika kusini limekataa kumtambua Veronica kama icons za mapambano nchini humo. Kufatia mchango huo wa Veronica hata hivyo, mwezi wa Aprili 2018, Veronica, anayejulikana kama "Mama wa Azania", alipewa tuzo ya Luthuli.

Thando Sipuye, mwanachama mtendaji wa Kikundi cha Utafiti cha Afrocetrik katika Chuo Kikuu cha Fort Hare aliandika: "... lakini serikali ya ANC haitamheshimu Mama Sobukwe kutokana na ubinafsi wa chama au kwa sababu inamtazama mama Sobukwe Kama mpinzani wa ANC maana ANC imekuwa na mitazamo tofauti ya wapigania uhuru walio nje ya chama hicho na katika mtazamo wake huo kuelekea katika mchango wa Mjane wa Sobukwe au urithi wa Sobukwe mwenywe serekali ya ANC imeshindwa kutoa hata tuzo kwa Mama Sobukwe ni jambo la aibu na mashtaka dhidi ya uzalendo kwa taifa letu yenye aibu juu ya dhamiri ya serikali ambayo inajitokeza leo kwa michango na kuonesha maadili ambayo inaadhimisha leo Kwenye kifo chake".

Mwandishi huyo anaishutumu serekari ya Pretoria kuwa... "Katika miongo miwili iliyopita serikali hii imesababisha Mama Sobukwe kuwa sio kitu wala kutokuwa na maana yoyote Ile ndani ya nchi yake, kwani imekuwa ikishindwa kumuweka katika uangalifu kama mpigania uhuru wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuto kumtambua kwenye 0kumbukumbu mbali mbali za kitaifa na kutoka kwenye majadiliano yoyote ya umma juu ya mashujaa wa Afrika kusini waliopambana katika utafutwaji wa Uhuru na wanajeshi wa mapigano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Wanaharakati wengi wa nchi ya Afrika kusini wametaka taifa hilo kutoa heshima kwa Mama Sobukwe kwani yeye anawakilisha kikundi cha wapigania uhuru wa uhuru wa taifa hilo. Mama Veronica Sobukwe ni miongoni mwa wapigania uhuru ambao wamekwisha kufutwa na kusaulika katika kumbukumbu ya wapigania uhuru nchini humo na viongozi wa mwanzo waliopinga ubaguzi wa rangi wa taifa hilo wakati wa utawala wa makaburu.

Veronica na Sobukwe walibahatika kupata watoto wanne ambao ni Miliswa, Dinilesizwe, Dalinyebo na Dedanizwe.

Veronica Sobukwe Alikufa mnamo Agosti 14, 2018. Kifo chake kilitokea katika hospitali ya Midland huko Graaff-Reinet, Rasi ya Mashariki ambako alikuwa amekwenda kupatiwa matibabu kwa wiki tatu.

Iliripotiwa kuwa kutolewa kwake kutoka hospitali kulichelewa kwa sababu hakuweza kupata dawa yake kwa muda maalumu baada ya kuchanganya dawa katika maduka ya kuuza dawa mitaani. Hata hivyo Veronica Sobukwe alitolewa hospital na kwenda nyumbani kwa mapumziko madogo na baada ya masaa kadhaa ililipotiwa kuwa alikufa nyumbani kwake akizungukwa na wapendwa wake huko Graaff-Reinet huko Rasi ya Mashariki siku ya Jumatano asubuhi.

Umauti ulimkuta akiwa na na umri wa miaka 91 Mungu ailaze roho yake mahali pema huko aendako atufikishie Salam kwa Robert Sobukwe, Nelson Mandela, Julius Nyerere, Samora Machel, Nkwame Nkhuruma, Abdul Naser Gamal na wengine wengi ambao walipigana dhidi ya dhurma ya mabeberu Afrika zama zake.

Na mjumbe wa mkutano mkuu kijana wa mwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom