Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
(Habari hii nimeiweka kidogo kidogo ili isichoshe kufuatilia)
Aitaka serikali kuacha kubambikia watu kesi!
Source: Na Happiness Katabazi. http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=9216
ALIYEKUWA Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe (55). ambaye hivi karibuni alishinda kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja, ameibuka na kusema hatishwi na rufaa inayokusudiwa kukatwa dhidi ya hukumu yake.
Zombe alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, katika mahojiano maalum na Tanzania Daima, yakiwa ya kwanza kwake tangu aachiwe huru na Mahakama Kuu ya Tanzania, Agosti 17 mwaka huu.
Katika mahojiano hayo, Zombe alisema hatua hiyo ya serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), ni ya kutaka kujikosha kwa umma kuwa inafanya kazi vizuri wakati inajua kuwa wapelelezi wake walikiuka taratibu na sheria, na kwamba rufaa hiyo ni mwendelezo wa kufuja fedha za walipa kodi.
Zombe alisema uamuzi wa ofisi ya DPP kukata rufaa dhidi yake, anaufananisha na mcheza mpira anayemfanyia faulo mchezaji mwenzake na kisha adhabu ya penati inapigwa kwenye lango la mchezaji aliyefanyiwa faulo na kufafanua kuwa, Jeshi la Polisi na DPP walimchezea mchezo mchafu wa kisheria, hivyo hawawezi kupiga penati kwake. Nasubiri kwa hamu kuona huo mtindo wa msuko (wa rufaa) unaousukwa na ofisi ya DPP, kama ni Twende kilioni, Kilimanjaro au Jicho la kuku dhidi yangu Ofisi ya DPP ina wataalamu wengi wa sheria, kwanini inashindwa kukubali ukweli kwamba kesi dhidi yangu ina upungufu mkubwa wa kisheria ambao hata mtoto wa shule ya chekechea anauona?