Hii case iwe isiwe, Zombe hana hatia ya kuua, hakufyatua risasi kuua mtu. Labla wamtie hatiani kwa makosa ambayo hakushitakiwa nayo ya kuficha na kupindisha ukweli na kufundisha wahalifu jinsi ya kuongea kwenye Tume ya Kipenka.
Waendesha mashitaka wetu ni mbumbumbu, walitakiwa kuleta counts kama 50 kwa zombe na wenzake, saa hizi tungekuwa tumeshasahau kama kulikuwa na kesi ya Zombe na wenzake. Maana wasingetiwa hatiani kwa mauaji ila wangetiwa hatiani kwa counts nyingine.
Mwacheni Zombe aombe kustaafu, ajichukulie stahili zake, mapema. Na kesi zote za ufisadi zitashindwa kama hii ya Zombe na wenzake. Tumesha mwagiwa pilipili za macho na waendesha mashitaka wa kisiasa. Sasa baada ya kuona wananchi wanakuja juu na uchaguzi unakaribia wanajifanya kumshikia bango Zombe. Mwacheni ajipumzikie baada ya kusota mahabusu kwa muda mrefu