Zoezi la ukaguzi wa leseni: Tatizo ni mtoa leseni au mmiliki wa leseni?

Ichobela

JF-Expert Member
Jan 7, 2012
326
156
Najaribu sana kufikiria hili zoezi linalotangazwa kutokea hivi karibuni. kinachonisukuma hata kuandika ni jinsi livyosikia kamanda akielezea, kwamba ni zoezi rafiki kwa madereva. Najaribu tu kufikiria kwa akili yangu isiyo ya kidereva.

Hivi kiini cha tatizo mpaka kupelekea kubuniwa kwa hili zoezi ni nini? Kuna mtu aliniambia ni mwarobaini wa ajari zinzolikumba taifa!!! Najaribu kujitafutia majibu ya kuwa, hivi ni kweli ajari zinasababishwa na leseni? Kuwa imepatikana baada ya muombaji kupitia chuo cha udereva?

Kuna rafiki yangu alibahatika kuzaliwa familia yenye magari, alianza kujifunza kuendesha toka akiwa na umri wa miaka kumi na tisa, ukiachilia mbali ile kuchukua funguo za gari anaambiwa kuosha gari anaamua kulisogeza nyuma kidogo au mbele kidogo, hiyo kaanza akiwa mdogo sana. Kwa sasa anakimbilia miaka hamsini na mitano na dereva mzoefu. Anaendesha malori na hajawahi kupata ajari toka aendeshe magari.

Kuna madereva wa mabasi ambao wengi wao kama sio wote,wamepitia chuo cha taifa cha usafirishaji, lakini hakuna madereva wanaongoza kwa kupata ajali au kusababisha ajali kama madereva wa mabasi!

Maajabu sasa ya hili zoezi, ni kufanya uhakiki kama leseni ilitolewa kufuata utaratibu........!!!!!

Hivi anaetakiwa kuulizwa hapa ni nani? Mwenye leseni au aloitoa hiyo leseni?

Mwenye leseni anachotaka ni leseni. Utaratibu wa kuipata anaeujua ni mtoa leseni.

Unanipa leseni mwenyewe,halafu unakuja kunikagua kama nimeipata kihalali!!!!! Kwa nini usihangaike na mtoa leseni?

Serikali yangu,hapa nafikiri pangeangaliwa vizuri, inawezekana kabisa nia ni njema lakini kwa nianavyo mimi ni kwamba mnatengeneza mianya ya rushwa! Kama leseni zilitolewa kwa kupindisha taratubu bado na ukaguzi utafanyika kwa kupindisha utaratibu.

Kaeni na watoa leseni,waelekezeni,waonyeni wasipindishe taratibu.

mnaotaka kuleta ni usumbufu wa bila sababu. Kagueni leseni FEKi ( Ambazo hazijatokwa Vehcle na kulipiwa TRA. Lakini mlizotoa nyie tena halali achaneni nazo. Wengi hawatakuwa na vyeti hata kama walisoma chuo.
 
Ahsante sana, hii issue nlikuwa nawaambia jamaa juzi wawatafute hao waliotoa Leseni bila Vyeti sijui certificate. Leseni uzuri zina tarehe ya kutolewa na mahali/eneo, wakikuta mwenye leseni hana certificate au aliipata kimagumashi basi wamtafute huyo Vehicle Inspector aliyehusika kuitoa hiyo leseni na awajibishwe mbn vitu viko wazi mnataka kutukaba mchana hivi.
 
Back
Top Bottom