Hakika ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni!
Wakati Dar es Salaam Mkuu wao wa Mkoa akijinasibu kwa kuongoza mikoa mingine zoezi la uandikishaji, Halima Mdee anaibuka na tuhuma kwamba majina mengi hayana saini za wahusika
Sasa kituko ni huko Morogoro, baada ya juzi kupenyezewa kwamba wajumbe wa mtaa wanapita nyumba kwa nyumba kuorodhesha watu wote wenye miaka 18 na kuendelea, sasa zoezi limehamia kwa wanafunzi
Ili kuendana na kasi, waandikishaji wamepewa target ya watu 40 kwa siku. Wanachokifanya wanadaka yeyeto anayepita mbele yao, na wanaorodhesha wanafunzi kuanzia kidato cha pili na kuendelea wanaosoma ndani ya shule iliyomo ndani ya kata husika au jirani ilimradi tu wafikishe target.
Pia Wakuu wa shule wameambiwa wawahimize watoto wakajiandikishe na kila siku wanatoa taarifa ya idadi kwa mkurugenzi.
Shule zenye idadi ndogo ya wanafunzi waliojiandikisha Wakuu wa shule hupewa maneno yenye mwelekeo wa vitisho. Nani atakubali kutishiwa kisa watoto hawajiandikishi na uwezo wa kuwalazimisha anao!? Kinachotokea ni watoto kupigwa biti wakajiandikishe hata kama hawana miaka 18 ilimradi idadi iwe kubwa
Hizi taarifa wanazo walimu na watendaji wa mitaa.