Paul Kijoka
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 1,399
- 256
Hii ni kuchezea fedha ya wafadhili na kuharibu mambo ya msingi ya kitaifa! Zoezi hili ni lazima lifanywe kwa uangalifu na si kitu cha kufanyia mzaha! Angalia, ungekuwa mwenge ungeona kuwepo umakini lakini zoezi muhimu ambalo hadi shule zinafungwa na la muda mfupi linafanyiwa mzaha! Tunaomba kupewa taarifa ya kuwaondoa wale wote walioingia kwa kutokuwa na vigezo na wale waliolipishwa hela wajulikane na waseme wamempa nani na amekusanya kiasi gani kwakuwa tunajua na kwakujiamini kuwa RUSHWA imetembea na bado inaendele kutembea.serikali yetu bhana sijui watu wa usalama wanatusaidiaje kama nchi?
Katika hali ya kushangaza watendaji wanapiga simu kwa watu na kuwauzia nafasi. Kinachotia shaka ni jinsi UZEMBE huu unavyoachwa kwenye zoezi hili muhimu. Mambo ya sensa katika eneo muhimu sana ni hili la ukusanyaji taarifa (Data Collection). Iwapo eneo hili litaaribika basi maeneo yote yanayofuata yatakuwa yamehariba pia! Yaani maeneo ya Data Organization, Data Analysis, Data Interpretation and Report Writing. Tusubiri kupata data zisizo sahihi kwa uzembe huu.
Nimewasiliana na marafiki zangu sehemu mbali mbali mbali kwa hapa Dar wanakiri kuwa zoezi limefunikwa na utata. Rafiki yangu aliyepo kata ya Buyuni Dar amesema kule si rushwa tu ya 20 elf bali posho ni makubaliano. Amesema kuwa hali hii ni ya kwaida kwani ata kwenye uchaguzi huwa ndo muda wa watendaji kata kuvuna na anakupa nafasi alafu mnagawana pasu. Hii ni hatari na itatuletea balaa kwenye zoezi hili muhimu.