Ni hoja nzuri lakini sijui kama wabunge wa chama tawala walio ktk hizo kamati watakubali ku-step down. Maana leo nimesikia kwa wale walioweka sahihi zao juzi bungeni wamepigwa mikwala na katibu mkuu ccm.Mi naona pia hili suala kwenye katiba inayokuja tusisahau kuliweka sawa ili pasije kutokea rais hovyo kama huyu akatuyumbisha tena.ASANTE.
Snyamairo;
Ni kweli kwamba wale Wabunge takriban 7 waliweka sahihi zao watakumbana na mengi mno ndani ya UCCM na ndani ya vikao vyao, watasemwa, watadhalilishwa, watawakejeli, watawafumbia, watawatishia, watawabeza, watawasengenya, hata vidole watanyooshewa ila ifikie mahali CCM wakumbuke "bila CCM imara nchi hii itayumba" na ndiyo hiyo kama ni meli basi wananikumbusha MV-Bukoba ikianza kuyumba.
Hilo ni moja lakini la pili hawa Wabunge walionesha nia njema kuchagua fungu lililo jema na kimsingi CCM wangetumia busara hapa watu hawakuwa na nia ya kupambana na Cama hata kidogo. Watu lengo lao ni kuhakikisha kuwa wale wanaolitia Taifa hasara wanawajibishwa na hili vile vile lillikuwa na lengo la kukisaidia CCM. Mi nadhani japo walilifukia warudi tena wakasome Azimio la Arusha lakini vile vile Ahadi za MwanaTANU zimekuwa inco-porated ndani ya Katiba ya CCM nazo wazisome kwamba cheo ni dhamana.................
Mimi labda niwaambie hawa Wabunge wa CCM walioanza kutishiwa katika Siasa Pilato wa kweli si Katibu wala Mwenyekiti wa Chama, Pilato wa kweli si Hakimu wala Jaji, Pilato wa kweli si Spika wala Katibu wa Bunge, Pilato wa kweli si Chama cha Siasa, Pilato wa kweli si yule anayekufadhali kwa fedha na mambo yafananayo na hayo bali wapo kina Pilato wa kweli ambao huamka asubuhi na kwenda kupanga foleni kwa ajili ya kuwachagua wale wawafaao na hao kina Pilato ndio wa kuwaangalia na kuwajali sasa hivi manake hawatawachagua tena kutokana na Vyama bali uwajibikaji, uzalendo,pamoja na uwakilishi uliotukuka.