Zitto Zuberi Kabwe sasa MJIUZULU Nyadhifa zenu BUNGENI!

Hapa Mkuu umesoma mawazo yangu, ni suala lilikuwa niliingize kwenye maelezo yangu.
Nilianza hapo juu na kusema kuwa hii nchi ni ya Kusadikika, ni nchi ya kuhemea fursa, ni nchi ya mmoja kuendelea kwa mgongo wa mwenzake....

Bahati mbaya kwa sasa kwa Tanzania, hatuna upinzani ulioungana na/au uliotayari kufanya hivo. Hoja ya kutokuwa na imani na serikali (PM), ingawa ilikuwa ya CDM, ilipaswa iwe ya wapinzani wote, kama sio ya wabunge wote. Mkuu, umeangalia ni wabunge wangapi wa upinzani hawakusaini ile fomu? Kwa nini? Hao ndio kikwazo, hao ndio wanasubiri vinywa wazi "tonge idondoshwe waidake wao".

Hapa hapa jamvini, njoo na hoja ya kuwataka wapinzani waungane uone utakavyopata jawabu za kutisha:
- CUF ni CCM B
- Mrema anatumiwa na CCM
- TLP hivi, UDP vile.

Mkuu, bado naamini Roma haikujengwa siku moja, nikiwa na maana tuendelee na mapmbano na Njia yoyote inakufikisha Roma, nikiwa na maana tunaweza kutafautiana njia lakini bado lengo likawa ni moja - KUIKOMBOA TANZANIA. Mimi na wewe, na wengine wengi, tuendelee kuwahamasisha, kuwafahamisha na kuwaongoza Watanzania KUIKOMBOA TANZANIA

Well said Comrade nimeyachukua kama yalivyo.........
 
Sidhani kama kujiuzulu kwa wabunge ni suluhisho sahihi bali kinachotakiwa ni kwa wabunge kukataa kujadili hoja zote za serikali ikiwa ni pamoja na kutopitisha bajeti!

Nakuunga mkono kabisaaa! Kukwamisha bajeti ya serikali kutamfanya Rais na serikali yake kukubali kuyaondoa haya MAGUBEGUBE yanayojiona serikali na nyadhifa yaliyopewa NI ZA KUDUMU NA WAKO JUU YA SHERIA NA KILA MTU NCHI HII
 
mimi nafikiri umefika wakati wa wananchi kuwajibisha wabunge wao. nafikiri sisi tulio na access na jf basi tuanzie hapo tuonyeshe jinsi ambavyo haturidhishwi na dharau na jeuri ya serikali,hasa wa ccm jinsi ambavyo hawaoni kama wanakosea, nafikiri tunaweza kutoka na kudai haki yetu kwa nini watuibie tukiona?

libya na misri yalianza hivi hivi sasa wasitake na sisi tufike huko. zitto waambie wenzio kuwa tumechoka kudanganywa na sasa tunahitaji mapinduzi ya dhati. hata kama itatugharimu wengine lakin wapo wachache watapona na watatushukuru sisi tulo jitoa muhanga, tuache woga tuseme kwa sauti moja. hivi kuna mtu amewah kujiuliza mpaka 2015 tz itakuwa inamiliki rasilimali gani iwapo zote zimeshauzwa?
 
Hapa tatizo ni huyu mama mwenye sura m.ba..ya kama Ken..ng...e anashindwa kabisa kusimamamia sheria zinavyosema naa yeye anaadeal na watu waliomuweka madarakani kuwakingia kifuu na pia kuzui Bunge kuwajadili pie yeye hana nia njema kabisa na nchi hii kwani sasa anajijengea maisha ya kuustaafu so anaona ooh i dont care soon i'll be ritired so let it burn pasibo kufahamu kuwa ndio kabisa anachachua.
Kama kweli huyu bibi ana nia njema ya kutetea maslahi ya nchi bunge lingekuwa safi sana na hata Serikali ya hawa Magamba wasingesubutu kupeleka miswada uchwara Bungeni.Hapa ni kuamua moja tu Nguvu ya Umaa aaaaaa basi sie ndio wenye majibu i mean we have full packeg so we need action kutoa hizi takataka.
 
Mi naona akina zitto wakijiuzulu italeta intarraption coz amepeleka concern G75 kutokuwa na imani na PM akiwa kama chaiman wa kamati ya bunge,so pengine akistep aside iyo hoja ita_invalid.hebu mwenye kujua kipengele hiki a2juze.
 
Hapa tatizo ni huyu mama mwenye sura m.ba..ya kama Ken..ng...e anashindwa kabisa kusimamamia sheria zinavyosema naa yeye anaadeal na watu waliomuweka madarakani kuwakingia kifuu na pia kuzui Bunge kuwajadili pie yeye hana nia njema kabisa na nchi hii kwani sasa anajijengea maisha ya kuustaafu so anaona ooh i dont care soon i'll be ritired so let it burn pasibo kufahamu kuwa ndio kabisa anachachua.
Kama kweli huyu bibi ana nia njema ya kutetea maslahi ya nchi bunge lingekuwa safi sana na hata Serikali ya hawa Magamba wasingesubutu kupeleka miswada uchwara Bungeni.Hapa ni kuamua moja tu Nguvu ya Umaa aaaaaa basi sie ndio wenye majibu i mean we have full packeg so we need action kutoa hizi takataka.

KahaluaJr;

Ni dhahiri kuwa Madame Speaker kwa hapa tulipofikia hana nia njema ama na Bunge au Taifa kwa ujumla manake msimamo wake haujawahi kueleweka na hakuna dhambi mbaya kama kushindwa kutafsiri Sheria unaweza ukawa unajua kusoma vizuri lakini tafsiri ikawa mbovu ambayo hupelekea miscarriage of justice. Hili naona ndilo tatizo kubwa la Madame Speaker katika kufafanua ama Katiba au Kanuni za Bunge.

Mfano mzuri ni juzi alipokuwa akifafanua ile Ibara ya 53A ya Katiba juu ya namna ya kumwondoa PM aliishia kusema hoja ikiletwa na Zitto itakuwa ni batili sasa kwa mtu wa wadhifa wa Speaker angeamua kuweka kando Itikadi angetoa ufafanuzi uliojitosheleza kwamba ili isiwe batili ni kipi kifanyike, haitoshi tu kusema kuwa siku 14 zitakuwa hazijafika hivyo kukiuka matakwa ya Ibara ya 53A(3).

Kwa kuwa lilikuwa jambo zito kama yeye mwenyewe Speaker alivyokiri basi naye angekuja na maelezo mazito kweli kweli ambayo baadae Bunge lingine mathalan Bunge la 11 yangeyatumia kama "Precedent" endapo swala la namna hiyo litajitokeza. Ni kutokana na kutoweza kujua msimamo wa Speaker juu ya Taifa ndiyo maana tunataka kujua kipi kifanyike...
 
Watanzania walio wengi ikiwa ni pamoja na Wabunge, Viongozi wa ngazi mbali mbali Serikalini, Viongozi wa dini na watu wengine wa kada mbalimbali walitegemea na walikuwa na matumaini chanya katika hotuba ya Waziri Mkuu wakati akilihitimisha Bunge la 10 katika Mkutano wake wa 7 na Kikao chake cha 10 tarehe 23.04.2012, matumaini ambayo yamekuwa tofauti kabisa na mategemeo yao hivyo kupelekea walio wengi kubaki kujiuliza ni nini hatma yaTaifa letu.

Nitaomba nianzie mbali kidogo, ukiacha ile Ibara ya 64(1) ya Katiba (1977) inayoipa Bunge mamlaka na madaraka ya kutunga Sheria, Ibara ya 63(2) ya Katiba inatamka wazi nanukuu
“Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.”

Katiba hiyo hiyo Chini ya Ibara ya 96(1) inaipa Bunge nguvu ama uwezo, wa kuunda Kamati mbali mbali kwa ajili ya ufanisi wa kazi za Bunge kazi ambazo zimeshatajwa hapo juu. Na bila ya kuathiri masharti ya Ibara 96(1), Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Kanuni ya 115 pia inatambua uwepo wa Kamati za Kudumu za Bunge. Vile vile Kanuni hiyo ya 115 ndiyo inayotambua na kuipa nguvu Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

Nyongeza ya Nane ya Kanuni, katika Sehemu yake ya Kwanza inatambua Kamati za Kudumu zisizo za Sekta, Sehemu ya Pili inatambua Kamati za Kudumu za Bunge za Sekta na sehemu ya Mwisho ni ile inayotambua Kamati ya Kudumu za Bunge zinazosimamia Fedha za umma. Ni sehemu ile ya Pili pamoja na ya Tatu ambayo Kamati ya Zitto Zuberi ambaye ni Mwenyekiti pamoja na Wenyev
 
Naunga mkono hoja

Ni hoja nzuri lakini sijui kama wabunge wa chama tawala walio ktk hizo kamati watakubali ku-step down. Maana leo nimesikia kwa wale walioweka sahihi zao juzi bungeni wamepigwa mikwala na katibu mkuu ccm.Mi naona pia hili suala kwenye katiba inayokuja tusisahau kuliweka sawa ili pasije kutokea rais hovyo kama huyu akatuyumbisha tena.ASANTE.
 
Back
Top Bottom