Zitto Zuberi Kabwe sasa MJIUZULU Nyadhifa zenu BUNGENI! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Zuberi Kabwe sasa MJIUZULU Nyadhifa zenu BUNGENI!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Meitinyiku L. Robinson, Apr 25, 2012.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania walio wengi ikiwa ni pamoja na Wabunge, Viongozi wa ngazi mbali mbali Serikalini, Viongozi wa dini na watu wengine wa kada mbalimbali walitegemea na walikuwa na matumaini chanya katika hotuba ya Waziri Mkuu wakati akilihitimisha Bunge la 10 katika Mkutano wake wa 7 na Kikao chake cha 10 tarehe 23.04.2012, matumaini ambayo yamekuwa tofauti kabisa na mategemeo yao hivyo kupelekea walio wengi kubaki kujiuliza ni nini hatma yaTaifa letu.

  Nitaomba nianzie mbali kidogo, ukiacha ile Ibara ya 64(1) ya Katiba (1977) inayoipa Bunge mamlaka na madaraka ya kutunga Sheria, Ibara ya 63(2) ya Katiba inatamka wazi nanukuu
  "Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii."

  Katiba hiyo hiyo Chini ya Ibara ya 96(1) inaipa Bunge nguvu ama uwezo, wa kuunda Kamati mbali mbali kwa ajili ya ufanisi wa kazi za Bunge kazi ambazo zimeshatajwa hapo juu. Na bila ya kuathiri masharti ya Ibara 96(1), Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Kanuni ya 115 pia inatambua uwepo wa Kamati za Kudumu za Bunge. Vile vile Kanuni hiyo ya 115 ndiyo inayotambua na kuipa nguvu Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

  Nyongeza ya Nane ya Kanuni, katika Sehemu yake ya Kwanza inatambua Kamati za Kudumu zisizo za Sekta, Sehemu ya Pili inatambua Kamati za Kudumu za Bunge za Sekta na sehemu ya Mwisho ni ile inayotambua Kamati ya Kudumu za Bunge zinazosimamia Fedha za umma. Ni sehemu ile ya Pili pamoja na ya Tatu ambayo Kamati ya Zitto Zuberi ambaye ni Mwenyekiti pamoja na Wenyeviti wengine wa Kamati mbali mbali za Kudumu za Bunge wamo. Kamati hizi zote chini ya Nyongeza hii ya Nane zimepewa majukumu mahususi juu ya ama Wizara au Sekta mbali mbali ambazo zinapaswa kuzisimamia ipasavyo.

  Ni vyema ikatambulika kwamba kazi zinazopewa kamati ni katika kuhakikisha kuwa ile Ibara ya 63(2) ya Katiba inasimamiwa ipasavyo katika kuhakikisha kuwa Bunge inaishauri na kuisimamia Serikali.
  Wananchi tumeona namna ambavyo Kamati husika zimekuwa zikifanya kazi kwa niaba ya Wananchi waliowatuma humo Bungeni kwa ufanisi na uzalendo mkubwa ila cha kustaajabisha Serikali ambayo inapaswa kusimamiwa na kushauriwa na Bunge kwa kupitia Kamati husika ama imekuwa ikipuuza ushauri utolewao au kulidharau Bunge kwa ujumla wake na hivyo kudhihirisha kutotambua kazi ya Mhimili huu mwingine hivyo kupelekea kuvunja Katiba ambayo Serikali imeapa kuilinda na kuitetea.

  Binafsi ningependa kutoa wito, kwa kuwa hata Spika anaonekana kutoona kuwa Bunge linadharauliwa basi Wenyeviti na Wanakamati wao wafanye maamuzi ya kujivua nyadhifa zao Bungeni mara moja ili kulinda heshima zao na za wale waliowatuma. Haiwezekani watu wakafanya kazi nzito namna ile na kutoa ushauri wenye nia njema kwa Taifa lakini hakuna hatua zozote za kutia matumaini zilizo ama zinazoonesha kuchukuliwa. Niwaulize wanakamati;

  1. Kuna haja gani ya kuwa na hizo Kamati ambazo ni rubberstamp ??
  2. Kuna haja gani wanakamati kukutana Dar es Salaam kwa shughuli ambazo Serikali inaziona ni batili ??
  3. Kuna haja gani ya kutoa ushauri na maelekezo ambayo yataendelea kuwekwa kapuni ??
  4. Kuna haja gani ya kuendelea kuvumilia Kanuni na Katiba zikivunjwa wazi wazi ??
  5. Kuna haja gani ya kuendelea kulidhalilisha na kulidharau Bunge ??
  6. Kuna haja gani ya kuendelea kuitwa mwanakamati ilihali kazi uifanyayo inapuuzwa ??
  7. Kuna haja gani ya kuendelea kutumia kodi za Watanzania ilihali mafanikio hayaonekani ??
  8. Kuna haja gani ya kuendelea kutukanwa na kunyooshewa vidole kwa sababu tu wewe ni mwanakamati uliyeamua kuwasaidia watanzania lakini Serikali isiyowajali Watanzania inakung'ata na kukupuliza ??
  9. Kuna haja gani ya kuendelea kuishauri Serikali inayoongozwa kwa Upepo wa Kisiasa ??
  10. Kuna haja gani ya kusema Bunge lina Haki na Madaraka ??

  SASA BASI;KAMA Anne Semamba Makinda haoni Bunge likidhalilishwa na kudharauliwa, KAMA Anne Semamba Makinda haoni wanakamati wake wakipuuzwa kwa kiwango cha juu, KAMA Anne Semamba Makinda haoni Katiba na Kanuni za Bunge zikivunjwa kwa uhodari na kishujaa BASI NINYI Wanakamati na Wenyeviti wenu oneni hilo na mwonyesheni pia Anne Semamba Makinda hilo mwachieni hizo nafasi ili tuone kama ataweza kuliongoza Bunge pasipo hizo Kamati.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki JF

  MEITINYIKU L. Robinson
   
 2. M

  Malova JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Huenda Makinda mwenyewe haoni kama Bunge lake linadhalilishwa.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Hii ngoma iko kwa wananchi, wataamua wenyewe nani wataamua kumwajibisha
   
 4. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Andiko zuri sana....
  Na kwa kweli ni muda sasa wabunge nao kama walivyotarajia Waziri Mkuu angejiuzuru kwa kuwa amedharauliwa na Rais,
  Kwa mtiririko huo huo ni sahihi kwa wabunge kujiudhuru kwa kudharauliwa na kudhalilishwa na serikali.
  Warudi kwa wananchi na wawaambie kuwa Bunge halina tija kwa Taifa kwa muundo huu!
  Kama wabunge wakichukua hatua hiyo inaweza kuwa move nzuri zaidi na lazima system ikwame sababu itakuwa ni scenario mpya kabisa.

  Hebu tuangalie hii ya kutaka kumuondoa Pinda ya wabunge 75 itafikia wapi, ila nayo ikihujumiwa kama wengi tunavyotarajia ni bora kwa wabunge makini kujiondoa bungeni.
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ni hoja nzuri sana lakini iko katika nchi ya Kusadikika.
  Kuvunja Kamati hakuwezi kuwa suluhisho na hakutakuwa na taathira zozote kwa nchi na katika upepeo huu unaoendelea kuvuma ambapo Mkuu wa Kaya anasema Utapita. Watakaokuwa wamejijengea heshima ni hawa wenyeviti wa kamati tu lakini sio mwengine yeyote.

  Kuvunja kamati ndiko kutakoufanya huo upepo uwe umepita, kwani Bunge litachagua kamati nyengine na kuwafanya CCM wajihisi wameshinda kiulaini.

  Pamoja na kuwa iko haja ya kufanya ulilosema, kutoka hapa hadi 2015 ni muda mkubwa sana. Kuna viako vya bunge visivypungua 9 mpaka wakati huo. Ikiwa kamati zitaendelea kubakia, na ikiwa katika kila kikao yatatokea kama yaliyotokea wiki iliyopita:
  - CAG kuendelea kumwaga uoza wa serikali,
  - Wabunge wa CCM kukijia juu chama chao,
  - Wabunge wa CCM na upinzani kushiakana mkono pale maslahi ya taifa yanapohusika,
  - Wanachama kwa maelfu wa CCM kukihama chama chao,
  - Watanzania kuwatambua zaidi maadui zao,
  -
  -
  -...kila tukio kama hilo ni turufu mkononi kwa Wananchi na Upinzani kuelekea uchaguzi wa 2015.
  Tusiuache Upepo Upite kama anavyotaka/anavyojidanganya Mkuu wa Kaya
   
 6. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama kujiuzulu kwa wabunge ni suluhisho sahihi bali kinachotakiwa ni kwa wabunge kukataa kujadili hoja zote za serikali ikiwa ni pamoja na kutopitisha bajeti!
   
 7. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MAMMAMIA Heshima kwako Mkuu,

  Kimsingi hatujapishana sana kimtazamo na kifkra, katika hili ila swala la kuvunjwa kwa hizi kamati ama kujiuzulu kwa Viongozi wa kamati hizi sidhani kama wana CCM watakuwa na pa kujisifia Mathalan ile kamati ya Fedha za umma kiutaratibu ni lazma iongozwe na wabunge kutoka Upinzani sasa kama wabunge wa upinzani watakataa kuongoza kamati hizo kutokana na ushauri wao kupuuzwa ni nini itakuwa hatma ya Bunge na Spika??
   
 8. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Indinyikwa meitinyiku,iroro esidai lengajang'
   
 9. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ileje ndugu;

  Swala langu si kujiuzulu kwa Wabunge ila ni wabunge kujiuzulu nyadhifa walizonazo Bungeni mathalan wenyeviti wa Kamati mbali mbali pamoja na wanakamati hao na kujiuzulu huko automatically kutapelekea kutojadiliwa kwa hoja za Serikali kama ulivyoshauri.
   
 10. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Emeka;

  Ajo aashe naleng' lengajang'
   
 11. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  Pweinti mkuu.. Zitto akusome alafu ajipime kama bado anaona umuhimu wa yeye kuongoza hiyo kamati
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  @Meitinyiku L. Robinson & Emeka Anyaoku
  Ashee Oleng' lalashe!
  Engai engoitoi' bhabhalai
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hapa Mkuu umesoma mawazo yangu, ni suala lilikuwa niliingize kwenye maelezo yangu.
  Nilianza hapo juu na kusema kuwa hii nchi ni ya Kusadikika, ni nchi ya kuhemea fursa, ni nchi ya mmoja kuendelea kwa mgongo wa mwenzake....

  Bahati mbaya kwa sasa kwa Tanzania, hatuna upinzani ulioungana na/au uliotayari kufanya hivo. Hoja ya kutokuwa na imani na serikali (PM), ingawa ilikuwa ya CDM, ilipaswa iwe ya wapinzani wote, kama sio ya wabunge wote. Mkuu, umeangalia ni wabunge wangapi wa upinzani hawakusaini ile fomu? Kwa nini? Hao ndio kikwazo, hao ndio wanasubiri vinywa wazi "tonge idondoshwe waidake wao".

  Hapa hapa jamvini, njoo na hoja ya kuwataka wapinzani waungane uone utakavyopata jawabu za kutisha:
  - CUF ni CCM B
  - Mrema anatumiwa na CCM
  - TLP hivi, UDP vile.

  Mkuu, bado naamini Roma haikujengwa siku moja, nikiwa na maana tuendelee na mapmbano na Njia yoyote inakufikisha Roma, nikiwa na maana tunaweza kutafautiana njia lakini bado lengo likawa ni moja - KUIKOMBOA TANZANIA. Mimi na wewe, na wengine wengi, tuendelee kuwahamasisha, kuwafahamisha na kuwaongoza Watanzania KUIKOMBOA TANZANIA
   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sisi wananchi tutawaadabisha wabunge!
   
 15. KML

  KML JF-Expert Member

  #15
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 863
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mnazingua...andikeni lugha ya kueleweka bwana au anzisheni forum ya kilugha chenu muongee kilugha
   
 16. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Umeweza kuainisha kikanuni na 2mekuelewa..sasa basi mimi naona Akina zitto wakistep aside kutoka ktk kamati hizi kutaibuka utata wa kikanuni.Zitto kapeleka hoja concern G75 may b kama chaiman wa kamati ya mashirika ya uma kama cjakosea,akijiuzulu atapoteza nguvu dhidi ya hoja ya kutokuwa na imani na PM.Pengine kama suala la hoja halimbani.
   
 17. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Wasiotawala ni chakula cha watawala.
   
 18. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,749
  Trophy Points: 280
  hii imekaa vizuri ila heading iko off kidogo!
   
 19. mase88

  mase88 JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 248
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  hapa bongo (TZ) bunge na mahakama si tena mihimiri mikuu ya dola kama ilivyo serikali kuu kwani unaona kabisa hawa wote yaani bunge na mahakama kuwa chini ya sirikali ya ccm sasa sijui katiba mpya tuu ndo suluhisho au tatizo ni CCM na vibaraka wao kama wakuu wa mkoa cha ajabu hadi :target:SPIKA UPO KULINDA :target:SIRIKALI NA CCM:target: hapo chacha
   
 20. M

  Mr. Teacher JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 330
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Naunga mkono hoja
   
Loading...