Zitto Zuberi Kabwe sasa MJIUZULU Nyadhifa zenu BUNGENI!

Mi naona akina zitto wakijiuzulu italeta intarraption coz amepeleka concern G75 kutokuwa na imani na PM akiwa kama chaiman wa kamati ya bunge,so pengine akistep aside iyo hoja ita_invalid.hebu mwenye kujua kipengele hiki a2juze.

Emeka Anyaoku;

Japo bado sijapata supporting provision ya swali lako lakini binafsi sioni ni kwa namna gani kujiuzulu kwa Zitto kama Mwenyekiti ama Mwanakamati kuta nullify ama vitiate kile alichokipeleka kwa Speaker.

Submission yake itabaki pale pale, japo Katiba katika ile Ibara ya 53 (A) haijaainisha kuwa ni nani anaweza kupeleka hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ila imefafanua kuwa Bunge linaweza kupitisha azimio la kutokuwa na imani na PM hivyo basi kwa kuwa Bunge hukaliwa na Wabunge tafsiri ni kwamba Mbunge yeyote (I stand to be corrected) anaweza kutoa ama kupeleka hoja hiyo pale inapobidi.

Hivyo ni wazi kwamba hata Zitto yaweza ikawa kapeleka hoja yake si chini ya mwamvuli wa Uenyekiti bali kwa nafasi yake kama Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Ni hoja nzuri lakini sijui kama wabunge wa chama tawala walio ktk hizo kamati watakubali ku-step down. Maana leo nimesikia kwa wale walioweka sahihi zao juzi bungeni wamepigwa mikwala na katibu mkuu ccm.Mi naona pia hili suala kwenye katiba inayokuja tusisahau kuliweka sawa ili pasije kutokea rais hovyo kama huyu akatuyumbisha tena.ASANTE.

Snyamairo;

Ni kweli kwamba wale Wabunge takriban 7 waliweka sahihi zao watakumbana na mengi mno ndani ya UCCM na ndani ya vikao vyao, watasemwa, watadhalilishwa, watawakejeli, watawafumbia, watawatishia, watawabeza, watawasengenya, hata vidole watanyooshewa ila ifikie mahali CCM wakumbuke "bila CCM imara nchi hii itayumba" na ndiyo hiyo kama ni meli basi wananikumbusha MV-Bukoba ikianza kuyumba.

Hilo ni moja lakini la pili hawa Wabunge walionesha nia njema kuchagua fungu lililo jema na kimsingi CCM wangetumia busara hapa watu hawakuwa na nia ya kupambana na Cama hata kidogo. Watu lengo lao ni kuhakikisha kuwa wale wanaolitia Taifa hasara wanawajibishwa na hili vile vile lillikuwa na lengo la kukisaidia CCM. Mi nadhani japo walilifukia warudi tena wakasome Azimio la Arusha lakini vile vile Ahadi za MwanaTANU zimekuwa inco-porated ndani ya Katiba ya CCM nazo wazisome kwamba cheo ni dhamana.................

Mimi labda niwaambie hawa Wabunge wa CCM walioanza kutishiwa katika Siasa Pilato wa kweli si Katibu wala Mwenyekiti wa Chama, Pilato wa kweli si Hakimu wala Jaji, Pilato wa kweli si Spika wala Katibu wa Bunge, Pilato wa kweli si Chama cha Siasa, Pilato wa kweli si yule anayekufadhali kwa fedha na mambo yafananayo na hayo bali wapo kina Pilato wa kweli ambao huamka asubuhi na kwenda kupanga foleni kwa ajili ya kuwachagua wale wawafaao na hao kina Pilato ndio wa kuwaangalia na kuwajali sasa hivi manake hawatawachagua tena kutokana na Vyama bali uwajibikaji, uzalendo,pamoja na uwakilishi uliotukuka.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom