Zitto:Wizara ya Nishati imezoea kuzusha tuhuma

Zitto:Wizara ya Nishati imezoea kuzusha tuhuma

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Wizara ya Nishati imezoea kuzusha tuhuma kwa wabunge ili kukwepesha hoja za msingi. Mwaka huu wamenoa. Nawashukuru sana wabunge Chris Ole Sendeka na David Kafulila kwa kusimama imara bila woga kuhusu hoja ya Tegeta Escrow. Mbinu za Katibu Mkuu Maswi za kugawa wabunge kwa kuzusha tuhuma za kuokoteza zimeshindwa. Uchunguzi wa tuhuma za tshs 200 bilioni lazima ufanyike. Tusivalishwe miwani za mbao kwa mambo ya uzushi. Uchunguzi ndio utatoa ukweli. Kwanini mnakimbia uchunguzi?
Chanzo:Zitto Kabwe FB wall
 
Hili swala naona hata Dr Hamisi kingwngara amelizungumzia Kambi rasmi Bungeni kwa Maoni yangu wasinge toka Nje ili waibane serikari vizuri.
 
Wakati akiwa naibu katibu Mkuu CHADEMA ilisemekana ofisi zake zipo facebook na Twitter,sasa siku hizi haonekani bungeni ila matamko na majibu yake anachangia kupitia facebook,ofisi zake za bunge na vikao anavifanyia facebook siku hizi??!! Ugonjwa wa Shida Salum isiwe sababu,vinginevyo auguze kwanza aachane na kuchangia mijadala kwa kuvizia kupitia Facebook!!
 
Hili swala naona hata Dr Hamisi kingwngara amelizungumzia Kambi rasmi Bungeni kwa Maoni yangu wasinge toka Nje ili waibane serikari vizuri.
Kwa uzoefu wako wangebaki wangebadili kitu gani? wangezuia bajeti isipitishwe?
 
Hili swala naona hata Dr Hamisi kingwngara amelizungumzia Kambi rasmi Bungeni kwa Maoni yangu wasinge toka Nje ili waibane serikari vizuri.

Kwa utaratibu wa kugawa wazungumzaji kwa idadi maalumu huku maCCM akiwa yamepanga wamwaga mitusi isingesaidia kwani pia wangekuja kushindwa kwa kula ya ndio na sio na hoja ingefia hapo!!
 
Nataka pesa zirudi,lakini sio Zito kuwa ndo msemaji,huyu anauza mechi,tazama watu wametoka nje coz ni hoja ya UKAWA,lakini yeye hubinafsisha na ananuna wengine wakizungumza
 
Naona watu wameanza kujadili mtu na sio hoja. Huu ugonjwa mpaka uje kutoka vichwani mwa watanzania itkuwa kizazi cha sita kutoka sasa.
 
Wizara ya Nishati imezoea kuzusha tuhuma kwa wabunge ili kukwepesha hoja za msingi. Mwaka huu wamenoa. Nawashukuru sana wabunge Chris Ole Sendeka na David Kafulila kwa kusimama imara bila woga kuhusu hoja ya Tegeta Escrow. Mbinu za Katibu Mkuu Maswi za kugawa wabunge kwa kuzusha tuhuma za kuokoteza zimeshindwa. Uchunguzi wa tuhuma za tshs 200 bilioni lazima ufanyike. Tusivalishwe miwani za mbao kwa mambo ya uzushi. Uchunguzi ndio utatoa ukweli. Kwanini mnakimbia uchunguzi?
Chanzo:Zitto Kabwe FB wall

Mama anaendeleaje? Leo huhitaji kufarijiwa?
 
Wangeaibika tu wala hawana jipya walafi wa madaraka na kuandaa fujo.

toka lini msukule usiojitambua kama wewe ukawa na mawazo ya kizalendo? Sijawahi ona msukuma mpumbafu kama wewe unayeendekeza njaa!
 
Kwa uzoefu wako wangebaki wangebadili kitu gani? wangezuia bajeti isipitishwe?

Wayasema hayo Madudu ya Escrow tunajua kupita itapita tu lakini kusema kwa ingesaidia kuliko kutoka na kwenda kwenye vyombo vya habari kama wanavyofanya sasa hapa kwenye Ukumbi wa kiongozi wa kambi ya Upinzani ambapo kwenye taarifa za habari kwenye Tv zetu ni dakika 3 mpaka 5 wakati Wwngekuwepo ndani ya Bunge walikuwa na Dakika 7 za kuchangia na nyingine wakati Bunge likikaa kama kamati wanashikilia shilingi wanapata kuchangia kwa wingi kwa upana wake.
 
Ni mtazamo sahihi na CCM waachane na Petty Politics. Profesa mzima anafanya siasa za kitoto namna hii akishirikiana na katibu wake?

Kaka Benn! Kwani mnafanya siasa kushindana na ccm au mnataka kutusaidia watanzania kujikomboa? Nyie toeni hoja waamuzi tuko huku nje wala sio mjengoni.
 
Back
Top Bottom