Zitto waweza rudi sasa mambo ni shwari

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
18,716
28,623
Kwanza pole sana kiongoz wangu mkuu wa chama haya ndo maisha kaka lakin kwanini ukimbie nchi yako kaka

Hebu rudi bhana mambo yamesha isha rudi tupambane kamanda wangu bunge limekaribia kuanza

Nishaweka mambo sawa wewe njoo tu usiogope.

Mhariri na muandishi nguli wa gazeti la jamhuri Ndugu Deodatus Balile (i stand to be corrected)ametoa nasaha zake kuhusiana na habari zinazoendelea zinamhusu Zitto Kabwe.

Akiongea katika kipindi cha "Morning Trumpet Weekend" kilichokuwa kikiangazia habari zilizopata umaarufu kwa wiki hii, Balile alishauri Zitto ajitokeze na ajisalimishe polisi ili ajue wanachomtafutia.

"Zitto kama raia mwema hapaswi kujificha bali ajitokeze ili sheria ichukue mkondo wake" alisema Balile.

Balile aliendelea kwa kusema habari hizi za watu kupotea si sifa nzuri kwa taifa....na ana uhakika kuwa mashtaka yote ya uchochezi serikali imekuwa ikishindwa mahakamani hivyo Zitto hatakiwi kuogopa.

Pia Balile amesema ni wakati muafaka kwa serikali kuondokana na sheria hii ya uchochezi kwani haina mashiko.
 
Kwanza pole sana kiongoz wangu mkuu wa chama haya ndo maisha kaka lakin kwanini ukimbie nchi yako kaka

Hebu rudi bhana mambo yamesha isha rudi tupambane kamanda wangu bunge limekaribia kuanza

Nishaweka mambo sawa wewe njoo tu usiogope
Ina maana Mh alitoka nduki?
 
Kesi ya Jinai ya kughushi nyaraka za Umiliki wa gari haina kikomo cha Mashtaka!
 
Sasa Kama wao wakitishiwa wanajificha pasipojulikana, laki wakiitisha maandamano wanataka sisi walalahoi tuwe msitari was mbele, hivi huuu si utapeli kweli??
 
Wewe ni kamanda yupi? Mbona mnatumia akili za kitoto kumkamata mtu? Kwanini msimuite kiustaarabu mkamhoji kuliko kujigeuza kituko mbele za watu?
 
Kwanza pole sana kiongoz wangu mkuu wa chama haya ndo maisha kaka lakin kwanini ukimbie nchi yako kaka

Hebu rudi bhana mambo yamesha isha rudi tupambane kamanda wangu bunge limekaribia kuanza

Nishaweka mambo sawa wewe njoo tu usiogope
Umetumwa?
 
Shida ni pale utakapowekwa kwenye sandarusi mto Ruvu afadhali uwe na kesi isiyo na dhamana maana mahakamani utayashinda makanjanja
 
Mhariri na muandishi nguli wa gazeti la jamhuri Ndugu Deodatus Balile (i stand to be corrected)ametoa nasaha zake kuhusiana na habari zinazoendelea zinamhusu Zitto Kabwe.

Akiongea katika kipindi cha "Morning Trumpet Weekend" kilichokuwa kikiangazia habari zilizopata umaarufu kwa wiki hii, Balile alishauri Zitto ajitokeze na ajisalimishe polisi ili ajue wanachomtafutia.

"Zitto kama raia mwema hapaswi kujificha bali ajitokeze ili sheria ichukue mkondo wake" alisema Balile.

Balile aliendelea kwa kusema habari hizi za watu kupotea si sifa nzuri kwa taifa....na ana uhakika kuwa mashtaka yote ya uchochezi serikali imekuwa ikishindwa mahakamani hivyo Zitto hatakiwi kuogopa.

Pia Balile amesema ni wakati muafaka kwa serikali kuondokana na sheria hii ya uchochezi kwani haina mashiko.
 
Atajitokeza wakati wa Bunge.....ili akasemee ndani ya Bunge!! Then hata wakimkamata dunia nzima iwe naye pamoja daima!! Ila utawala huu hauoni aibu?? Nchi haina rabber stamp kwa mtu mmoja!!! Yetu sote kwa nini tunanyanyaswa?
 
Back
Top Bottom