Zitto vs Muhongo; nani ni Political Stunt Engineer | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto vs Muhongo; nani ni Political Stunt Engineer

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babykailama, Sep 21, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Zitto vs Muhongo; nani ni Political Stunt Engineer

  1.Muhongo anajulikana ni mwanachama wa CCM, Zitto ni CHADEMA (kwa utambulisho wa kadi na gwanda) na ni CCM (kwa maisha yake)

  2. Muda mfupi, Muhongo alipoingia tu akaona uozo wa Muhando na Mafisadi huko TANESCO na akasema Mkurugenzi akae pembeni kupisha uchunguzi kamili; Zitto kakaa Bungeni muda wote na akiwa mwenyekiti wa POAC hajawahi kusema kuwa kuna migao ya umeme isiyo ya lazima wala kupiga kelele juu ya mateso na uhujumu unaofanywa na wenye majenereta dhidi ya TANESCO na Taifa letu. Na kusimamishwa kwa Muhando kunamkosesha usingizi Zitto hadi kesho!

  3. Muhongo anasema Bodi mpya ya TPDC ifanye kazi yake barabara ikiwa ni pamoja na kupitia mikataba yote na kutoa mapendekezo yao tayari kwa hatua zinazopaswa kufuatwa kwa mujibu wa sheria. Zitto hataki anabaki kusema tu mikataba iwekwe wazi, wapi na bila kusema baada ya kuwekwa wazi nini kitafanyika.
  4. Zitto anasema Bodi (tena mpya ) ya TPDC ni wale wale hivyo hawana moral authority kupitia mikataba hiyo; lakini hasemi Bunge (hilo hilo akiwemo yeye) la zamani hawana moral authority kupitia nyongeza za marekebisho ya Sheria ya Mafao waliyoyapitisha wao au mambo mengi tu ambayo wameyapitisha au kuyajadili na kuyasema karibu kila mwaka.

  5. Zitto aliwahi sema aliingia Siasa kwa bahati mbaya, na akaueleza umma yuko njiani kuacha siasa aende kusoma. Hakuacha siasa tena badala yake tumemwona akifanya hata siasa chafu kiasi cha kuwachukuwa wenzake wa CHADEMA na kuwapeleka kwenye Leka Dutigite kwa kisingizio cha kuwanyanyua Wasanii kisha kuwacha njia panda waonekane kuwa wao wamemwandaa yeye kugombea Urais ili alete mtafaruku CHADEMA na alifikia hatua ya kusema hapa kuwa analiamini gazeti kuliko maneno ya wenzake akina Mh. Halima Mdee.

  6. Tumemsikia Dkt. Muhongo kila mara akiueleza umma hapa Chuo Kikuu Mlimani na katika makongamano ya wasomi akizungumzia na kupigania kwa vitendo umuhimu wa elimu hasa tafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa nchi yetu na Bara la Afrika hadi ulimwengu ukamtambua akawa wa kwanza kupata tuzo ya Mwingereza, Prof. Robert Shackleton (the Robert Shackleton award), akifanya tafiti hadi Wasomi wa Kitanzania wakamkubali na kumpa tuzo ya Kitaifa ya Utafiti Bora (The Tanzanian National Award for Outstanding Research in Science & Technology toka COSTECH), akileta michango ya nguvu kusimamia elimu bora na mchango katika tasnia ya uchimbaji madini hadi dunia ya Wasomi wa Kifaransa wakasimama na kumvika nishani ya Emperor Napoleon na kupewa ngazi ya Ordre des Palmes Académiques. Wengi tunamfahamu si tu kama Msomi bali mbunifu na mpigania haki za Mwafrika kufikia kuasisi na kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kwanza wa Shirika la Kimataifa la Sayansi – Afrika (ICSU) (Latest news: Regional Office for Africa — ICSU) – Afrika ya kusini.

  7. Tumemwona Zitto anaamka asubuhi na kukimbilia media na kutembeza karatasi ya kutafuta saini za kutosha eti kupiga kura ya kutokuwa na matumaini kwa Waziri Mkuu endapo Mawaziri (wahusika) hawatabadilishwa; akisha pata hizo saini hajawahi kurudi kwa Wabunge wala Wananchi kuwaeleza alichokuwa anakitafuta na kimepatikanaje sasa maana Mawaziri wapya tena wenye mashiko ndio hawa akina Muhongo hawataki na anawapiga vita bila sababu.
  Ninyi mtaamua ni nani flip- floper na Mhadisi wa kutaka misifa (Political Stunt Engineer) kati ya Dr. Muhongo, Officier, Ordre des Palmes Academiques na Bwana Zitto, Leka Dutigite .
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  I wish ingekuwa rahisi kama ulivyoainisha hapo juu.

  Wote wawili wana nafasi wanayofanya. Hata ushauri wa mwendawazimu unaweza okoa kitu fulani, so kuna wakati kila mmoja wao hoja zake zinakuwa na mashiko.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  zito level zengine kwa kuweka watu 'attention pliz'
   
 4. H

  Hansen Nasli JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 881
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Yaan thread yako imeonesha chuki zilizo wazi kwa Zitto na kubeza mazuri anayofanza ila bado sana viwanda vyenu vya kutengeneza uongo na majungu bado havijafanikiwa
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,109
  Trophy Points: 280
  ..nadhani flip-floper ni Prof.Muhongo.

  ..jumapili kadai mikataba ipitiwe kwa nia ya kuirekebisha.

  ..jumanne akasema mikataba itaheshimiwa.
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kisiasa 'Flip Flopping' ya Prof. Muhongo imendoa nguvu zake zote..
   
 7. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Amin amin nawaambieni, Mgao wa umeme utakaolikumba taifa hili ni bab KK...

  Muhongo atleast he's shown MD Mhando for wht he is..incompetent(sp) and power hungry...but still removing him doesn't mean we shall have power reliability and availability, not that he had erred in removing this stupid excuse of leadership flop naaah, Mhando is corrupt through and through !!


  Zitto has political advantage...

  There needs to be formed a 'technical team' to study power system master plan and its shortcomings, this needs to be made available as its crucial for all backbone,turnkey and power generation,transmission and distribution in our country.

  Will be back when its dark!

  We should demand technical team even formed by TANESCO, Ministry and JICA and EWURA to study this moose on the table

  'POWER SYSTEM MASTERPLAN' tuwekewe wazi...ndio tutajua siasa ianzie wapi iishie wapi, na lini Mgao ulioanza kulikumba taifa hili tangu 1995 unaisha lini
   
 8. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Peleka mauchafu yako huko,msiwe mnajaza seva kwa kuweka uhalo hapa,ujui hata kulinganisha vitu polojo nyingi no points
   
 9. saidyakub

  saidyakub Senior Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Muhongo alikuja na ahadi ya kutokua na mgawo wa umeme, hii hoja inamuumiza sana sasa hivi maana viwanda vikubwa wanalazimishwa sasa kupunguza matumizi ya umeme na Tanesco, huku na sisi tukikatiwa umeme kwa kisingizio cha kurekebisha miundombinu kujiandaa na mvua kubwa zinazotarajiwa kushesha karibuni pia mgogoro wa watumia natural gas na Songas dhidi ya Tanesco bado ngoma ngumu lengo ni kupeleka gas yote izalishe umeme kusiwe na mgao. Nachooona hapa ni presha toka mamlaka za juu ya Muhongo ndizo zinazoanza kuendesha wizara ila Muhongo kama Muhongo hana matatizo kama ilivyo kwa Zitto na hoja zake za msingi
   
 10. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Zitto haaminiki tena na yeye ndiye anaonekana kigeugeu. Kama Mashaka alivyo mwambia amwache Prof. Muhongo afanye kazi yake. Lugha aliyoitumia dhidi ya Prof. Muhongo haikuwa ya staha na ukweli ni kwamba hata yeye Zitto hajatoa suluisho la hiyo mikataba maana kuiweka wazi tu si tija sema kisha ifanyweje kama ni mibaya.
   
 11. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Huyo waziri ni mzembe ..TPDC haiingii mikataba, mikataba yote husainiwa na waziri sasa waziri anawezaje kupeleka mikataba ikaangaliwe ma watu ambao hawana maamuzi nayo? ...hapo ndipo ninapomuona zitto kuwa anafaa kuwa rais wa nchi hii
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Bado napata shida sana ni kitu gani kilicho sababisha Prof Muhongo kubadili kauli ndani ya masaa 24! Kwa haraka haraka tunaweza kusema alipata order toka juu. Lakini kama ndivyo, order ya juu ilikuja hivi hivi? Nani alitibua mambo, au kama ni simu zilitoka wapi? Nani alimpigia simu nani hadi 'juu' (pengine) wakatoa order?
   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Wakati Prof. Muhongo anateuliwa kuwa waziri na kwa kuangalia cv yake nami nilidhani kwamba sasa wizara ya nishati na madini imepata mtu sahihi.
  Lakini kadri siku zinavyosonga mbele nagundua kwamba Prof.Muhongo si mtaalamu kama tulivyoaminishwa tangu awali, bali huyu Prof.ni mwanaccm kama walivyo wanaccm wengine. Na wanaccm wote wanafanana, awe amesoma sana ama hajasoma kabisa. Mawaziri waliomtangulia Muhongo (ambao hawakuwa maprof) nao walipata kuahidi kama yeye anavyofanya na baada ya muda mfupi sana wakaja kula matapishi yao. Kwahiyo ni wazi kwamba Prof. Muhongo anaendeleza kilekile walichokuwa wakifanya watangulizi wake.
  Ushauri wangu kwa Zitto, kwakuwa unafanya kazi nzuri sana kwa ajili ya nchi hii, jambo la muhimu sasa ni kuhakikisha kwamba unafanya mambo haya chini ya mwavuli wa chama chako ili ccm wasitumie mwanya kama huu wanaoutumia hapa kudilute hoja zako ambazo mara zote zimekuwa ni nzuri kwa manufaa ya taifa hili.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  The problem is that ZZK determined to win this battle he is attacking on many fronts. And to counterattack Prof Muhongo finds himself having to make some concessions

  For example ZZK attacks the review plan. Prof Muhongo goes ahead with the plan. ZZK cooks a story that investors are skeptical and have lost interest. What do you think prof Muhongo will do in that case? He'll definitely give reassurance. ZZK brandishes him flip flopper!

  ZZK is so conniving. Make no mistake I'm in favor of the Norwegians nonetheless
   
 15. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Zitto ni jembe anafaa kuwa hata rais wetu.Prof Muhongo hana lolote yeye ni msomi kwa ajili ya tumbo lake kama alikuwa mshauri kwenye sera na sheria za madini mwaka 1998 mbona hakushauri sheria zenye manufaa kwa watanzania au alipokuwa mshauri wa Satton resources walipowauzia mgodi wa Bulyanhulu kwa Kahama Mining(KMCL)watu wengi walifukiwa kwenye maduara refer kesi ya kina Tundu Lissu na Mrema na tena hawakulipwa fidia yeye alishauri nini.Mzungu huyo alilipwa dola mil 230 lakini serikali ya Tanzania haiikupata chochote mzungu huyo anaitwa Dr Sinclair yuko Tanzania hii mpaka leo na Barrick wameuza mgodi kwa Wachina China Gold najua Tanzania bado hatutapata kitu kwani nasikia tayari washatua Tanzania na wakanada wanaondoka mmoja kwa kisingizio wanaresign
   
Loading...