Zitto Vs Mkulo, Nani Mwongo? IMF yaikalia kooni serikali

Zitto Vs Mkulo, Nani Mwongo? IMF yaikalia kooni serikali

The Finest hizo semina elekezi ni njia ya kula fedha za umma vilevile, yote hayo ni kufilisi nchi yetu. Wewe uchague mawaziri incompetent na wafanya kazi wa ngazi za juu mafisadi type ya Mkulo unategemea nini, the whole managerial system ya hii serikali ni lotten. Bado tutaona mengi tuu!!!!
Mtumishi Wetu ukianza kufikiri sana unaishia kujiuliza hivi tumeachiwa laana au ni kitu gani jana Rais amekutana na IMF officals who presented various papers na moja ya mambo ya msingi waliishauri serikali kuongeza kodi kwenye madini kama strategy ya ku-boost revenue collection to meet budgetary obligations si ajabu Serikali haitoweza hata kuuchukua kidogo ushauri huu kwa kigezo cha kuwaogopa wawekezaji.
 
Zitto usibadili mada, ulisema Wabunge hawajalipwa.

Waziri kasema wamelipwa na tarehe katoa.

Sasa unakuja na michongo ya makusanyo ya kodi 15% imepungua blah blah blah

Zitto ulibwatuka uzushi, kwa watu makini credibility yako ina suffer!

Kazi kweli kweli, inahitaji ujasiri mkubwa kutoa utetezi kama huu!
 
Nimesema kwa mfano dhahiri, mpaka tarehe 7 Mei sikuwa nimelipwa. Hata Mbunge wa CCM Serukamba hakuwa amelipwa na wajumbe wote wa kamati ya Bunge ninayoongoza hawakuwa wamelipwa. Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma hawakuwa wamelipwa. Ruzuku za vyama ambazo huwa zinalipwa tarehe 25 kila mwezi hazikuwa zimelipwa mpaka tarehe 5 Mei.

Hii ni mifano tu. Hoja ni kwamba Serikali imefilisika. Haina uwezo wa kukusanya mapato ya kutosha japo kulipia matumizi ya kawaida. Imekwenda kukopa benki. Tutamwajibisha Mkulo Bungeni.

mkulo anaongea kiserikali au analeta propaganada za chama kwa uma wa watanzania?

hawa watu wanaonyesha hawataki kukosolewa hata kwa vitu vya msingi...

i wish wabunge wa ccm wangekua na hata chembe ya uchungu kwa taifa hili.. pengine tungeweza kumwajibisha bungeni
 
Jamani hii serikali ya ccm awamu ya nne ni hafifuuuu kulikooo awamuuu zoteee...kwa sasa mapato yameshuka,haukna uwekezajii wa maana zaidii ya richmond/dowans, blah blah kila kukicha na kupanda kwa kasii gharamaa za maisha kulikooo wakatii wowotee uleeeeeee......
 
Hali ya Tanzania inatisha sana. Na ninavyoelewa mimi kwa jinsi ilivyo hakuna vyazo mbadala ambavyo vitaanishwa na hatimaye kuunusuru uchumi kuanguka kabisa.

Na hata hivyo ningekuwa mie kwa hali iliyopo ninge anza hivi.
1. Kufuta ruzuku zote ktk vyama vya siasa.
2.Mshahara wa aina yoyote ile wafanyakazi/wabunge/mawaziri kutovuka milioni 2.
3.Hakuna posho, ondoa posho zote panapostahili kama usafiri nk wanatumia fedha zao harafu wanatuma invoinces zao zinafanyiwa ukaguzi yakinifu ndo inalipwa.
 
IMF yaikalia kooni serikali

*Yaitaka iangalie upya misamaha ya kodi
*yasisitiza ongezeko la kodi katika madini

Na Mnaku Mbani

Source Majira - 11/05/2011

MAOFISA wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) wameitaka serikali kuangalia upya suala la misamaha ya kodi, kuongeza wigo wa malipo ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT), pamoja na kuongeza wigo wa kodi katika madini ili kuongeza mapato ambayo nyanazidi kudorora.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema wiki hii na IMF, baada ya kumalizika mazungumzo baina ya maofisa wake na wale wa serikali, ushauri huo unalenga katika kuiwezesha serikali ya Tanzania kuongeza wigo wa ukusanyaji wa kodi.

“Wakurugenzi wamependekeza umuhimu wa kuongeza wigo wa kodi, kupunguza misamaha na kuongeza udhibiti wa fedha za umma. Wamependekeza kuongeza wigo wa ulipaji wa VAT na kuongeza wigo wa kodi katika madini,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo pia imekemea suala la Tanzania kuendelea kutegemea wafadhiri wa nje katika kuendesha bajeti yake kwani utegemezi unatarajia kukua hadi kufikia asilimia 10 ya pato la ndani la taifa (GDP) kwa mwaka huu.

Hali hii inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuwepo na taarifa kwamba serikali ya Tanzania inakumbwa na ukata mkubwa ambao umesababisha baadhi wa watumishi kuchelewezewa mishahara yao, huku ikiwa imebakia mwezi mmoja tu kumalizika kwa mwaka wa fedha 2010/2011.

Hata hivyo, waziri wa fedha, uchumi na mipango Mustafa Mkulo alikanusha vikali habari hizo juzi na kusema kuwa serikali ina hali nzuri ya kifedha na yote yanayosemwa ni siasa za kujitafutia umaarufu.

“Hali ya upatikanaji wa mapato na matumizi bado ina changamoto zaidi kipindi hiki: makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2010/2011 hayataweza kutimiza malengo ya bajeti kutokana na hali mbaya ha hewa, ukata wa fedha za matumizi ya serikali pamoja na riba za madeni ya nyuma. Kumekuwepo na upunguzaji wa matumizi lakini tunatarajia uthibiti zaidi wa matumizi,” imesema taarifa ya IMF.

“Wakurugenzi wamekubali kwamba mwaka 2011/2012 utakuwa ni hatua moja au nyingine ya serikali ya Tanzania kuboresha uthibiti wa fedha za umma. Tunatambua kwamba bei kubwa ya mafuta, hali ya hewa na upungufu wa misaada utasababisha matatizo katika kugharamia mipango ya bajeti, wameitaka serikali kuendelea kubana matumizi ili yalingane na hali halisi ya mapato.”

Maafisa hao wameiomba serikali kuongeza matumizi katika huduma za kijamii na miundombinu ambayo ina mrejesho mkubwa.

“Wakurugenzi wamesisitiza maofisa wa serikali kukamilisha mkakati wa kuratibu madeni ili kuhakikisha kwamba mikopo yote itakayokopwa inazingatia kupunguza riba,” inasema taarifa hiyo.

Hata hivyo, wakurugenzi hao wa IMF wamesisitiza umuhimu wa serikali kuangalia maendeleo ya mfumuko wa bei kwa kubana masharti ya masoko ya fedha ikiwa ni pamoja na kuangalia tatizo ya kushindwa kurudisha mikopo katika benki kwa baadhi ya wakopaji hasa watu binafsi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo yenye kumbukumbu namba No. 11/53 iliyotolewa Mei 9, 2011, maafisa hao walisema kwamba ukuaji wa uchumi wa nchi kwa mwaka 2011 utashuka hadi kufikia asilimia 6 ikiwa hali ya bei za mafuta, umeme zinaendelea kwa muda mrefu.

“Kwa makadirio yetu ya kipindi cha kati, tunaona kwamba hali ya kiuchumi sio mbaya sana lakini kutakuwepo na changamoto za kisera. Kuongezeka kwa idadi ya watu kutaongeza changamoto katika utoaji wa huduma za kijamii achilia mbali kushuka kwa kodi na misaada,” ilisema taarifa hiyo.

Source; Majira 11/05/2011

My Take:
  1. Yaliyosema na Zitto kuhusu ukata Serikalini ni kweli tupu.
  2. Kelele za CHADEMA kuhusu serikali kuongeza mapato, hasa kwenye madini na kuangalia vyanzo vingine ni kweli tupu.
  3. Kelele za wafanyakazi kuhusu wigo finyu wa mapato serikalini ni hakika na kweli tupu
  4. Mkulo ni mwongo na ni hatari kwa nchi hiii
Kwenye red kwa sababu siyo raia wa nchii hana uchungu na watanzania wala nchi hii yeye hapo yupo kujaza tumbo lake tu kisha akale nchini kwake
 
Kwenye red kwa sababu siyo raia wa nchii hana uchungu na watanzania wala nchi hii yeye hapo yupo kujaza tumbo lake tu kisha akale nchini kwake

Sasa inakuaje tunampa uwaziri mtu ambaye sio raia?Kweli Tanzania tumelogwa.
 
tatizo Zitto alitoa kauli yake wakati mawaziri wa mr. kikwete wametoka kwenye semina elekezi walikoagizwa kujibu chochote ambacho kinasemwa kuhusu serekali badala ya kukaa kimya.

kwa hiyo bwana mkulo alikuwa anatekeleza agizo la mkuu wake. suala kama alichosema (mkulo) ni uwongo au ukweli, siyo ishu...ishu ni kujibu mapigo kama alivyoagizwa na mkuu wake.

Hii ni sahihi kabisa, alikuwa nafuata maagizo ya bosi wake kujibu kila kombora linaloelekezwa lakini kimsingi kakurupuka kama ambavyo alichemsha baada ya kuwapelekea wadfadhili bajeti ya kimagumashi tofautui na aliyoiwasilisha bungeni. MTU HUYU NI HATARI KWA TAIFA NA KWA BOSI WAKE NA HATA KWA CHAMA CHAKE
 
Wana JF jana jioni nimemsikia huyu kibonde akisema kama serikali imeamua kukopa katika benki za ndani ili kulipa mishahara ya watumishi wake haina neno so long as itakaporejesha deni hilo fedha izo zitatumika kuinua uchumi wa humu humu nchini,kivipi wachumi naomba mnisaidie??serikali ikope stanbic au exim irejeshe iyo pesa inasaidia vp uchumi wetu??? labda kama iyo pesa iliyokopwa ingekuwa kwa shuguli ya maendeleo kujenga barabara,hospitali nk lakini kwa kulipa mishahara,bado hai click. Tusaidiana wanajf uyo ndio kibonde na radio yao ya clouds CCM B...!!!
 
Mkuu uliyeanzisha hii habari, mbona kwenye kichwa cha habari kuna maneno "IMF yaikalia kooni serikali" lakini kwenye habari yenyewe hakuna mahali ulipoeleza chochote kuhusu IMF?
 
Wana JF jana jioni nimemsikia huyu kibonde akisema kama serikali imeamua kukopa katika benki za ndani ili kulipa mishahara ya watumishi wake haina neno so long as itakaporejesha deni hilo fedha izo zitatumika kuinua uchumi wa humu humu nchini,kivipi wachumi naomba mnisaidie??serikali ikope stanbic au exim irejeshe iyo pesa inasaidia vp uchumi wetu??? labda kama iyo pesa iliyokopwa ingekuwa kwa shuguli ya maendeleo kujenga barabara,hospitali nk lakini kwa kulipa mishahara,bado hai click. Tusaidiana wanajf uyo ndio kibonde na radio yao ya clouds CCM B...!!!

Huyu jamaa msamehe, maana elimu yake kwa kweli sijui ni nini, hana reasoning hata kidogo
 
Wana JF jana jioni nimemsikia huyu kibonde akisema kama serikali imeamua kukopa katika benki za ndani ili kulipa mishahara ya watumishi wake haina neno so long as itakaporejesha deni hilo fedha izo zitatumika kuinua uchumi wa humu humu nchini,kivipi wachumi naomba mnisaidie??serikali ikope stanbic au exim irejeshe iyo pesa inasaidia vp uchumi wetu??? labda kama iyo pesa iliyokopwa ingekuwa kwa shuguli ya maendeleo kujenga barabara,hospitali nk lakini kwa kulipa mishahara,bado hai click. Tusaidiana wanajf uyo ndio kibonde na radio yao ya clouds CCM B...!!!

kazi ngumu sana kuwa mnafiki.

hata mimi nilimsikia.

lakini nachelea kumnanga nisijepigwa ban
 
Kibonde is a stupid fellow!! Lets ignore him!! Hata anaowatetea inaonekana wanamshanggaa kwani walimplipa wakati wa uchaguzi na si kipindi hiki!! Kwani ana akili finyu!!
 
Zitto amjibu Waziri Mkulo
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema atamthibitishia bungeni, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo kuwa Serikali imefilisika.Zitto alisema jana mjini Sumbawanga kuwa wataweka hadharani jinsi Serikali ilivyokopa fedha benki ili Waziri Mkulo aweze kuwajibika kutokana na kauli yake aliyoiita ya kukataa kusema ukweli.

Alisisitiza kwamba serikali haina fedha na kudokeza kuwa taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya mapitio ya uchumi ya mwezi Machi mwaka huu, inaonyesha kuwa imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15.

"Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali katika makusanyo ya kodi zote imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15 isipokuwa ushuru wa forodha. Hivyo haikufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi," alisema Zitto.

Kwa mujibu wa Zitto, Machi, mwaka huu Serikali ilikopa fedha katika Benki ya Exim na benki zote za biashara nchini na ilikuwa ikihangaika ili iweze kuwalipa wafanyakazi."Mkulo atueleze ni serikali gani duniani inakopa kwenye benki za biashara kwa kuwa kitendo hicho ni hatari sana kwa nchi," alisema na kuongeza:"Bajeti ya mwaka uliopita ilikuwa ni Sh11 trilioni ambayo Serikali ilishindwa kufikia malengo ya Sh 1.6 trilioni kutokana na kushindwa kukusanya kodi kwa asilimia hiyo 15 isipokuwa ushuru wa forodha."
Alimtaka Mkulo kuacha kuwaona wanaosema kwamba serikali haina fedha si wazalendo kwa kuwa wawekezaji hawatakuja nchini, bali atambue kuwa kukosekana kwa fedha si suala la uzalendo.

"Serikali ni kweli haina fedha na hakuna suala la uzalendo katika hili. Tatizo la uwekezaji ambalo analizungumzia, linatokana na sera mbovu za CCM kwa kuwa tangu mwaka 2007, hakuna uwekezaji wowote wa maana uliofanyika hapa nchini," alisema Zitto.

Akiwahutubia wanachama wa Chadema na wananchi wa mji wa Vwawa, Mbozi, mkoani Mbeya hivi karibuni, Zitto alisema Serikali ina hali mbaya kifedha kwa sasa kiasi cha kukopa ili kulipa mishahara ya wafanyakazi.
Alidai kuwa hali hiyo mbaya kifedha kwa serikali imesababisha watumishi wake pamoja na wabunge kutolipwa mishahara hadi Mei 7, 2011.

Alisema Serikali sasa inatafuta fedha za kuwalipa watumishi wake mishahara ya mwezi Aprili.
"Hata sehemu ya posho za wabunge mkutano uliopita, zikiwemo za kugharimia mafuta ya safari za wabunge majimboni bado hazijalipwa kutokana na Serikali kukosa fedha," alidai Zitto.

Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali imekwenda kukopa Sh540 bilioni kutoka benki za ndani ili watu wasijue kuwa inakabiliwa na ukata."Serikali haikopi fedha ili ijenge bandari, viwanda au kugharimia miradi ya maendeleo, bali inakopa ili ilipe mishahara ya wafanyakazi," alisema Zitto.

Kama hii taarifa ya mh. Zitto ni ya ukweli, je kuna sababu gani inayomfanya rais wa hii serkali asijiuzulu??
 
sema nao kaka....huyo mkulo ni kilaza kabisa...na tunaomba aeleze sababu ya wafanyakazi kukosa mishahara tangu mwezi wa pili hadi sasa.
 
Kwa CCM-Magamba, ukisema ukweli unapewa kila jina la kukuonyesha kuwa ni Adui, Mropokaji, mzushi na kila aina ya kejeli na vitisho!
Sasa kwa mambo verifiable kama haya ya serikali kukopa kwenye mabenki ya biashara, ni mambo ya kuficha kweli?...Pembe la ngombe halifichiki, nakusihi Zitto linda heshima yako kwa kuweka sawa kumbukumbu bungeni, ili ijulikane wasanii ni nani!
Huu uzalendo unaolindwa kwa kusema UWONGO si mzuri hata kidogo, bora tuseme ukweli huenda tukasaidika!
 
Back
Top Bottom