Zitto Vs Mkulo, Nani Mwongo? IMF yaikalia kooni serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Vs Mkulo, Nani Mwongo? IMF yaikalia kooni serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by josiah2008, May 11, 2011.

 1. j

  josiah2008 Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema atamthibitishia bungeni, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo kuwa Serikali imefilisika.Zitto alisema jana mjini Sumbawanga kuwa wataweka hadharani jinsi Serikali ilivyokopa fedha benki ili Waziri Mkulo aweze kuwajibika kutokana na kauli yake aliyoiita ya kukataa kusema ukweli.

  Alisisitiza kwamba serikali haina fedha na kudokeza kuwa taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya mapitio ya uchumi ya mwezi Machi mwaka huu, inaonyesha kuwa imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15.

  "Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali katika makusanyo ya kodi zote imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15 isipokuwa ushuru wa forodha. Hivyo haikufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi," alisema Zitto.

  Kwa mujibu wa Zitto, Machi, mwaka huu Serikali ilikopa fedha katika Benki ya Exim na benki zote za biashara nchini na ilikuwa ikihangaika ili iweze kuwalipa wafanyakazi.

  "Mkulo atueleze ni serikali gani duniani inakopa kwenye benki za biashara kwa kuwa kitendo hicho ni hatari sana kwa nchi," alisema na kuongeza:"Bajeti ya mwaka uliopita ilikuwa ni Sh11 trilioni ambayo Serikali ilishindwa kufikia malengo ya Sh 1.6 trilioni kutokana na kushindwa kukusanya kodi kwa asilimia hiyo 15 isipokuwa ushuru wa forodha."
  Alimtaka Mkulo kuacha kuwaona wanaosema kwamba serikali haina fedha si wazalendo kwa kuwa wawekezaji hawatakuja nchini, bali atambue kuwa kukosekana kwa fedha si suala la uzalendo.

  "Serikali ni kweli haina fedha na hakuna suala la uzalendo katika hili. Tatizo la uwekezaji ambalo analizungumzia, linatokana na sera mbovu za CCM kwa kuwa tangu mwaka 2007, hakuna uwekezaji wowote wa maana uliofanyika hapa nchini," alisema Zitto.

  Akiwahutubia wanachama wa Chadema na wananchi wa mji wa Vwawa, Mbozi, mkoani Mbeya hivi karibuni, Zitto alisema Serikali ina hali mbaya kifedha kwa sasa kiasi cha kukopa ili kulipa mishahara ya wafanyakazi.
  Alidai kuwa hali hiyo mbaya kifedha kwa serikali imesababisha watumishi wake pamoja na wabunge kutolipwa mishahara hadi Mei 7, 2011.

  Alisema Serikali sasa inatafuta fedha za kuwalipa watumishi wake mishahara ya mwezi Aprili.
  "Hata sehemu ya posho za wabunge mkutano uliopita, zikiwemo za kugharimia mafuta ya safari za wabunge majimboni bado hazijalipwa kutokana na Serikali kukosa fedha," alidai Zitto.

  Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali imekwenda kukopa Sh540 bilioni kutoka benki za ndani ili watu wasijue kuwa inakabiliwa na ukata."Serikali haikopi fedha ili ijenge bandari, viwanda au kugharimia miradi ya maendeleo, bali inakopa ili ilipe mishahara ya wafanyakazi," alisema Zitto.
  source; mwananchi
   
 2. j

  josiah2008 Member

  #2

 3. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Picha linaendelea
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hapa sasa Mkulo atajibu nini? Au ataleta masihara tena?
   
 6. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  imefika wakati viongozi wetu wawe wasema kweli.Mkulo unashindwaje kuukubali ukweli huu anaoeleza Mhe. Zitto??
   
 7. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  duh! Tanzania,tanzania nakupenda tanzania.....!!!!!!
   
 8. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mkulo hatasema kitu wala hatajiuzuru atakaa kimyaa yatapita, kwani ameshazoea huwa yanapita anaendelea kupeta. Nani wakumwajibisha Mkulo?
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  ccm wamezoea ubishi wa kijinga...wanalazimisha mambo sana
   
 10. Abigree

  Abigree Member

  #10
  May 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  haya sasa mkulo,akili kumkchwa
   
 11. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,302
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  Ndio maana Exim bank imeshindwa kutoa mikopo ya magari kwa wafanyakazi wake waliotuma maombi tangu February! Kumbe benki imeikopesha Serikari! Asante Mh Zitto kwa kutujuza!
   
 12. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkulo... Time will tell!!!
   
 13. k

  kagamba kadogo Senior Member

  #13
  May 11, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  au ndo maana mama mwambenja kaondoka exim bank
   
 14. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  Tanzania tanzaniaaaaa, ukweli ni kwamba sisi wananchi ndio tumeshindwa kuipeleka nchi yetu kule inakotakiwa kwenda...lets say enough is enough tujue moja!

  hawa watu wanapata wapi nguvu za kuudanganya uma na kufanya mambo ya kipuuzi namna hii?

  huyu mkulo si ndio alidanganya kwenye budget hadi wafadhili wa EU wakashtukia?
   
 15. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,161
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  IMF yaikalia kooni serikali  *Yaitaka iangalie upya misamaha ya kodi
  *yasisitiza ongezeko la kodi katika madini

  Na Mnaku Mbani

  Source Majira - 11/05/2011

  MAOFISA wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) wameitaka serikali kuangalia upya suala la misamaha ya kodi, kuongeza wigo wa malipo ya Kodi ya
  Ongezeko la Thamani (VAT), pamoja na kuongeza wigo wa kodi katika madini ili kuongeza mapato ambayo nyanazidi kudorora.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema wiki hii na IMF, baada ya kumalizika mazungumzo baina ya maofisa wake na wale wa serikali, ushauri huo unalenga katika kuiwezesha serikali ya Tanzania kuongeza wigo wa ukusanyaji wa kodi.

  “Wakurugenzi wamependekeza umuhimu wa kuongeza wigo wa kodi, kupunguza misamaha na kuongeza udhibiti wa fedha za umma. Wamependekeza kuongeza wigo wa ulipaji wa VAT na kuongeza wigo wa kodi katika madini,” ilisema taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo pia imekemea suala la Tanzania kuendelea kutegemea wafadhiri wa nje katika kuendesha bajeti yake kwani utegemezi unatarajia kukua hadi kufikia asilimia 10 ya pato la ndani la taifa (GDP) kwa mwaka huu.

  Hali hii inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuwepo na taarifa kwamba serikali ya Tanzania inakumbwa na ukata mkubwa ambao umesababisha baadhi wa watumishi kuchelewezewa mishahara yao, huku ikiwa imebakia mwezi mmoja tu kumalizika kwa mwaka wa fedha 2010/2011.

  Hata hivyo, waziri wa fedha, uchumi na mipango Mustafa Mkulo alikanusha vikali habari hizo juzi na kusema kuwa serikali ina hali nzuri ya kifedha na yote yanayosemwa ni siasa za kujitafutia umaarufu.

  “Hali ya upatikanaji wa mapato na matumizi bado ina changamoto zaidi kipindi hiki: makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2010/2011 hayataweza kutimiza malengo ya bajeti kutokana na hali mbaya ha hewa, ukata wa fedha za matumizi ya serikali pamoja na riba za madeni ya nyuma. Kumekuwepo na upunguzaji wa matumizi lakini tunatarajia uthibiti zaidi wa matumizi,” imesema taarifa ya IMF.

  “Wakurugenzi wamekubali kwamba mwaka 2011/2012 utakuwa ni hatua moja au nyingine ya serikali ya Tanzania kuboresha uthibiti wa fedha za umma. Tunatambua kwamba bei kubwa ya mafuta, hali ya hewa na upungufu wa misaada utasababisha matatizo katika kugharamia mipango ya bajeti, wameitaka serikali kuendelea kubana matumizi ili yalingane na hali halisi ya mapato.”

  Maafisa hao wameiomba serikali kuongeza matumizi katika huduma za kijamii na miundombinu ambayo ina mrejesho mkubwa.

  “Wakurugenzi wamesisitiza maofisa wa serikali kukamilisha mkakati wa kuratibu madeni ili kuhakikisha kwamba mikopo yote itakayokopwa inazingatia kupunguza riba,” inasema taarifa hiyo.

  Hata hivyo, wakurugenzi hao wa IMF wamesisitiza umuhimu wa serikali kuangalia maendeleo ya mfumuko wa bei kwa kubana masharti ya masoko ya fedha ikiwa ni pamoja na kuangalia tatizo ya kushindwa kurudisha mikopo katika benki kwa baadhi ya wakopaji hasa watu binafsi.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo yenye kumbukumbu namba No. 11/53 iliyotolewa Mei 9, 2011, maafisa hao walisema kwamba ukuaji wa uchumi wa nchi kwa mwaka 2011 utashuka hadi kufikia asilimia 6 ikiwa hali ya bei za mafuta, umeme zinaendelea kwa muda mrefu.

  “Kwa makadirio yetu ya kipindi cha kati, tunaona kwamba hali ya kiuchumi sio mbaya sana lakini kutakuwepo na changamoto za kisera. Kuongezeka kwa idadi ya watu kutaongeza changamoto katika utoaji wa huduma za kijamii achilia mbali kushuka kwa kodi na misaada,” ilisema taarifa hiyo.

  Source; Majira 11/05/2011

  My Take:
  1. Yaliyosema na Zitto kuhusu ukata Serikalini ni kweli tupu.
  2. Kelele za CHADEMA kuhusu serikali kuongeza mapato, hasa kwenye madini na kuangalia vyanzo vingine ni kweli tupu.
  3. Kelele za wafanyakazi kuhusu wigo finyu wa mapato serikalini ni hakika na kweli tupu
  4. Mkulo ni mwongo na ni hatari kwa nchi hiii
   
 16. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  tatizo Zitto alitoa kauli yake wakati mawaziri wa mr. kikwete wametoka kwenye semina elekezi walikoagizwa kujibu chochote ambacho kinasemwa kuhusu serekali badala ya kukaa kimya.

  kwa hiyo bwana mkulo alikuwa anatekeleza agizo la mkuu wake. suala kama alichosema (mkulo) ni uwongo au ukweli, siyo ishu...ishu ni kujibu mapigo kama alivyoagizwa na mkuu wake.
   
 17. T

  Taso JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Zitto usibadili mada, ulisema Wabunge hawajalipwa.

  Waziri kasema wamelipwa na tarehe katoa.

  Sasa unakuja na michongo ya makusanyo ya kodi 15% imepungua blah blah blah

  Zitto ulibwatuka uzushi, kwa watu makini credibility yako ina suffer!
   
 18. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Unajuaje......pengine wamelipwa wachache(wa CCM hasa) na wengine bado....yaani Zitto alipwe halafu aseme hajalipwa yeye hajui gharama ya kaulki yake?
   
 19. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Heri uchi wa mwili.... kuliko uchi wa akili.....
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Matumizi ya kianasa bila uzalishaji, serikali kuu hadi za mitaa... gavana, manaibu, mawaziri, wabunge wote wanalipwa mishahara utafikiri wako ndani ya Taifa linaloingiza mabilioni ya dollar kwa mwezi katika hazina! Tunapenda mno starehe na kuishi maisha ya "u-Pididdy" hata katika uongozi. Uhayawani wa kupenda maisha ya anasa huku tukitegemea misaada. Tabia imeshamiri, kuanzia Rais wa nchi na sasa hata inaambukizwa kwa watoto.

  Tulijua tangu mwaka jana kuwa bajeti ya matumizi katika mwaka huu itabidi serikali ikope, tena ikope kwenye benki binafsi. Chaajabu ni kwamba, ili kukabiliana na tatizo hili, hamna pahala serikali ilipoonekana inadhamiria kubana matumizi. Mikutano, makongamano, mishahara, posho, samani maofsini, n.k. vyote vimeendelea kuwa hivyo hivyo... It's unsustainable, haswa ukizingatia huu uzalishaji wetu wa kutegemea mvua za vuli na uwekezaji wenye kutoa misamaha ya kodi utafikiri wameturoga.

  Viongozi wetu pamoja na madigrii na maphd yao wameziba masikio na macho kujionea ya serikali ya Ugiriki na austerity measures zilizokuwa imposed huko na IMF ili kuepusha nchi kufirisika.
   
Loading...