RUSTEM PASHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2016
- 4,330
- 10,538
ZITTO UTAMKOMA RAIS MAGUFULI
Mwaka 2013, CAG katika ripoti yake, alitoa hati chafu kwa Wizara ya Ujenzi, kutokana na fedha kiasi cha Sh253 bilioni ambazo wizara hiyo iliziomba kwa ajili ya utekelezaji wa miradi maalum, lakini matumizi yake yalijaa giza.
Waziri wa Ujenzi alikuwa Dk John Magufuli. Hivyo kashfa hiyo ikawa inamwelekea yeye.
Zitto Kabwe akiwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), aliibebea bango kashfa hiyo. Bungeni pakachimbika. Zitto akashikilia mshahara wa Magufuli.
Kashfa hiyo ilimtesa sana Magufuli ambaye alihangaika kutoa maelezo na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii kujisafisha. Zitto alimkalia kooni.
Zitto akiwa Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, aliwakataza wabunge wa Chadema wakati huo kumsifia Magufuli. Wabunge wengi wa Chadema walikuwa wakisimama wanamsifu Magufuli kwa utendaji wake, Zitto akawaonya kuwa Magufuli alizitumia vibaya sifa hizo kwa kuushusha hadhi upinzani.
Kimsingi Magufuli na Zitto hawajawahi kuiva chungu kimoja. Ni Zitto aliyeahidi kuwa Magufuli atakuwa Rais wa muhula mmoja. Kwamba mwaka 2020 atakataliwa na wananchi.
Leo hii Magufuli ndiye Rais wa Tanzania. Zitto ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo, chama kichanga ambacho kinahitaji uwekezaji imara ili kiimarike na kukua.
Ni wakati huu sasa Magufuli anavuna vichwa ACT. Alimtwaa mshauri wa chama, Prof Kitila Mkumbo, akampa Ukatibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, sasa amemtwaa Mwenyekiti wa ACT, Anna Mghwira, kampa Ukuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kitila na Mghwira walikuwa nguzo hasa za ACT. Magufuli kawatwaa na kukiachia pengo chama, kisha kukijaza kashfa kuwa viongozi wake wana nasaba na CCM.
Kipindi hiki Zitto lazima ajue Magufuli ni nani. Magufuli ni Rais. Anatumia mamlaka yake kisayansi kukidhoofisha na kukipa wasifu mbaya chama cha ACT. Watu wakione chama ni ndugu na CCM, jambo ambalo ni sumu mbaya kwa siasa za upinzani Afrika.
Zitto wewe endelea kukomaa na usahihi wa sheria za madini, endelea kupambana kudai utawala wa sheria, endelea kunadi maono yako kuwa Magufuli ni Rais wa muhula mmoja, halafu yeye anakupiga kwa vitendo tu.
Ni sawa Magufuli kuwapa kazi wapinzani maana nchi ni ya wote, lakini uteuzi wa Kitila na Mghwira siyo afya kwa ACT.
Pole Zitto. Sisemi kuwa Rais Magufuli anakukomoa au anakulipizia kisasi, ila kiukweli utamkoma. Nakuhurumia sana.
Ndimi Luqman MALOTO.