Uchaguzi 2020 Zitto usijidanganye, Membe kaja ACT-Wazalendo kutafuta Urais siyo kumuunga mkono Tundu Lissu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
86,856
148,263
Dhambi nyingine ni za kujitakia tu, KC Zitto unaamini kabisa BKM amekuja ACT wazalendo ili amuunge mkono mgombea wa CHADEMA?

Hiyo unaweza kuwadanganya watoto wadogo lakini sisi tulioshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 1985 kamwe huwezi kutulaghai, tunakumbuka mzee ruksa alivyokomaa na kutinga magogoni.

Bernard Kamilius Membe alishika namba 5 kwenye kura za maoni za chama tawala aka CCM mwaka 2015. Membe ni kachero mbobezi aliyewahi kuwa naibu waziri mambo ya ndani na waziri wa mambo ya nje alichobakiza ni kuwa Rais na siyo meneja kampeni wa mgombea wa urais.

Niishie hapo.

Siasa ni uwongo lakini mambo mengine yako wazi sana.

2020 Hakunaga kama Dkt. Magufuli!
 
Membe amekuja ACT kwa sababu ya kuipenda nchi yake, na anaamini nchi yake haiko salama mikononi mwa John Joseph Pombe Magufuli.
Kwa hiyo yuko tayari yeye mwenyewe kuingia front kumng'oa Magufuli au kumuunga mkono yeyote anayeamini kuwa anafaa kuliko Magufuli
 
ACT wazalendo mwaka huu wanaichukua Zanzibar hiyo tu inatosha Membe kuweka heshima. ccm tutajutia sana kumuacha huyu kada aende upinzani
 
Membe alisema kabla ya mwezi wa October mwaka huu lolote laweza kutokea. Kajiunga ACT na kuteuliwa na kuchukua form ya Kugombea uraisi kwa tiketi ya ACT Wazalendo.

Kafariki Raisi Benjamin Mkapa. Tindu Lissu Karejea Nyumbani na kuteuliwa na kuchukuwa form kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema.

Kuna mengi mbeleni mchezo ndio kwanza unaanza kunoga.
 
Membe amekuja ACT kwa sababu ya kuipenda nchi yake, na anaamini nchi yake haiko salama mikononi mwa John Joseph Pombe Magufuli.
Kwa hiyo yuko tayari yeye mwenyewe kuingia front kumng'oa Magufuli au kumuunga mkono yeyote anayeamini kuwa anafaa kuliko Magufuli

Mpaka huku tunakubeba mabox. Tunajua nchi ipo salama kuliko wakati mwingine wowote. Labda kama kichwa chako Hakina kumbukumbu ya mabomu na ugaidi na wageni wa ajabu. Ujambazi wa kusukwa nk. Pole sana mkuu. JPM 2025. then akampuzike
 
Huku bongo ni full udikteta

Leo vyombo vya habari vimepigwa pini tena!
 
Back
Top Bottom