Zitto, unatuachaje?

Zitto, unatuachaje?

Zitto hachaguliki Kigoma Kaskazini.
 
si alisema anatak igeuza kigoma na tz kuwa malaysia na singapore?Au alikuwa anamaanisha ktk ndoto ?
 
Wabunge wote wa Chadema, uwa nacheka sana uteteza wa Chadema ukihoji kuhusu wabunge wao kutimiza ahadi zao wanarukia CCM na kujenga hoja kama za kwako.


Kwa hiyo nyie na CCM hamna tofauti?

Hawana dola,hawakusanyi kodi,unatarajia watoe pesa zao mfukoni? Nilichogundua kushabikia CCM zama hizi lazima uwe nuts
 
Ningependa maswali haya yajibiwe

Hivi Nyarubanda Secondary haina High school, au wewe sio wa Kigoma Kaskazini? Ulitaka barabara nyingine ya kutoka wapi kwenda wapi? Mbona Mahembe panafikika mpaka Kinazi hadi Janda, na kidahwe panafikika pia, sasa hatukuelewi, labda ufafanue
 
Wazungu wanasema... "Charity begins at home".

Mheshimiwa Zitto Kabwe najua wewe ni maarufu sana nje ya Kigoma Kaskazini. Lakini huku hamna ulichofanya.

-Tunakufa na kipindupindu katika soko la kibirizi.

-Hakuna hospitali hata ya kumzalisha mama wa Kigoma Kaskazini.

-Ukiacha barabara ya Mwandiga-Manyovu barabara zingine hazipitiki jimbo zima.

-Hatuna soko la kuuzia mazao yetu.

-Si kwamba watu wa Kigoma hatuna akili, tunafeli kuwa mkiani kimkoa kila mara. Hali ya Elimu jimboni ni mahututi.

Hakuna High School hata moja.
Sisi bado ni mkoa uliokuwa nyuma kimaendeleo... Mwisho kwa maana ya mkiani.

Mara nyingi umekuwa ukijisifia kwa maendeleo ya majimbo mengine ya mkoa wa Kigoma, mathalan Barabara ya mwandiga-Manyovu ambayo hata hivyo ililenga kuifikia jimbo la manyovu ambalo liko CCM basi tu kwa vile Kigoma Kask ikaangukia njiani...........

Tuoneshe kitu ambacho ni tangible cha kujivunia kwa Kigoma Kaskazini.......

Utupu

UNATUACHAJE??

Sasa huko Kigoma mjini utapaweza?

Kibirizi ni Jimbo la kigoma Kaskazini?
 
Siasa za kutumwa kuchafu watu kama hii hata mtoto hawezi kuzikubali
 
Back
Top Bottom