beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameingia madarakani kutokana na msiba, hivyo asipelekeshwe sana na badala yake apewe muda
Ameeleza Samia ambaye awali alikuwa Makamu wa Rais hakujiandaa kuwa Rais, bali msiba umetokea na amechukua mamlaka kwa mujibu wa Katiba
Aidha, amesema kuna masuala ambayo ni mapendekezo ya watu wengi Rais ameanza kuyachukulia hatua. Ameeleza, ni muhimu Rais kutafuta wataalamu ili kutazama namna ya utekelezaji wa bwawa la Mwalimu Nyerere, SGR, uboreshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na mengineyo