Zitto, Slaa na Kigwangalla mifano ya kuigwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto, Slaa na Kigwangalla mifano ya kuigwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Matteo, Apr 21, 2011.

 1. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mimi ni kati ya vijana wanaofurahishwa sana na jukwaa huru la chambuzi mbalimbali zinazofanyika humu ndani ya Jamii Forum, na kinachonifurahisha zaidi ni pale watu wanapoibuka na hoja nzito na zikachambuliwa kwa kina. Hivi karibuni nimeona thread mbili ambazo zilitolewa humu jukwaani na zikajibiwa na wahusika. Ya kwanza ni ile iliyokua na Heading "Siri nzito uteuzi wa Dr. Hamis Andrea Kigwangala kuwa mgombea wa Ubunge jimbo la Nzega. Na ya pili ni "Watanzania wameanza kumwelewa Dr. Slaa na siasa za kukurupuka.

  Walioongeliwa kwenye thread hizo hapo juu walijitokeza wazi wazi na kujibu tuhuma zilizo kuwa zikiwakabili. Mimi binafsi nawaunga mkono kwa ujasiri walioonyesha japo ufafanuzi wao, unaangukia kwa mtizamo binafsi wa msomaji. Mimi ninacho kipongeza ni kutoogopa kukosolewa na kujitokeza hadharani kwenye chombo husika ili kuweka record sawa pale ambapo unadhani alie kutuhumu hakuziweka sawa. Dr. Hamisi na Dr. Slaa waliweka record zao sawa, ila ni kwa kiasi gani walitushawishi hilo ni jambo la mtu binafsi.

  Ninacho kiomba hapa kwa watu mbalimbali, mashirika na asasi mbalimbali zinazotuhumiwa, kwa tuhuma mbalimbali humu ndani ya Jukwaa kujitokeza na kuweka record sawa. Mnacho ogopa nikipi haswa na msitake kusingizia kuwa hamuufahamu mtandao huu hata kama hujawahi kuutembelea najua ushawahi kuambia kuwa kunatuhuma zako JF. kwahiyo ingia, jiunge weka record sawa, tuone mambo yamekaa vipi.

  Kwa muda niliokuwa mwanachama hapa ndani sidhani kama lengo la JF ni kuchafuana ila lengo lililo wazi ni kutafuta way foward ya matatizo yanalo likabili Taifa letu ili kuweza kupata maendeleo endelevu.

  Vilevile nina Rai kwa wanachama wote wa JF tafadhali hakuna haja yakuficha jina lako, kwa sababu hapa ndipo tunapo weza kuongea wazi. Mfano unapo kuja na tuhuma kuhusu mtu fulani na ili hali umeficha jina, unajenga taswira ya uoga. Tuongee wazi kwa lengo moja la kujenga na si kubomoa na kama tunajenga nchi yetu kwa maslai yetu sote hatuna haja ya kuogopana kwanini lakini tuogopane.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu subiri kidogo sasa hivi utajibiwa
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aksante mwita matteo! Nasikitika sijakuelewa kwenye hii sred yako! Yan hapa nilichoambulia ni tuandike majina ya ukweli JF!!!
   
 4. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  chatu dume, sihitaji kujibiwa mimi nataka wanaotuhumiwa wazijibu tuhuma zao na sio kukaa kimya ama kuponda
   
 5. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  sweetlady,mi hapa najaribu kuwahimiza watu wote waliotuhumiwa humu Jamvini wajibu kama alivyofanya Dr. Slaa na Hamisi
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nashukuru sana mkuu, nmekupata sasa. Ntarudi bdae kuchangia zaidi.
   
 7. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Atleast umekuwa muungwana wa kupongez.
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ...Watasoma wahusika mimi sihusiki.........
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Asiyeelewa concept ya anonimity katika freedom of information anaonyesha upeo mdogo. Anayehusisha anonimity moja kwa moja na inauthenticity pia anaonyesha upeo mdogo na pia hata alama za ujasusi.

  Let's talk issues, not personalities.
   
 10. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa kutumia jina wanapongeza mh Zitto,na Dr Slaa(phd)lakini huyo mwingine siyo jina lake,jina lake halisi ni Said Nassor Bogoile,naomba umfute kwenye list ya wanaotumia majina halisi
   
 11. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa kutumia jina nawapongeza mh Zitto,na Dr Slaa(phd)lakini huyo mwingine siyo jina lake,jina lake halisi ni Said Nassor Bogoile,naomba umfute kwenye list ya wanaotumia majina halisi
   
 12. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  teh teh dr kingwalala bado wanawewe haya na huku karibu ufafanue km hili jina ni lako au la mpiga kura wako?
   
 13. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu kijallo,
  Kabla ya early 90s shule za sekondari zilikuwa adimu, mikoa michache ilikuwa na zaidi ya shule tatu. Kufaulu drs la saba ilikwa mbinde.
  Watu walirudia primary kwa majina ya walioacha ili kupata nafasi ya kwenda sec. Walioacha shule ama waliolewa, walioa, au waliamua tu kuacha. Wenye kiu na elimu walitumia nafasi hizi. Na watu wa aina hii wako wengi tu.
   
 14. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mi sikuelewi uliyeanzisha mjadala una lenga nini na utafaidika na nini zaidi ya kupoteza muda watu watumie majina yao ili iweje unataka kwenda kuwakopa au maana ishu humu ni hoja nA si majina ya watu ambao hawakupi mlo mazafaka
   
 15. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  We mode na wenzio mna wazimu hamjapost yangu kwanini mmefuta
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na mtoa mada.

  Bila kujali wanajibuje na wana matatizo gani huko waliko, nafikiri inabidi kuwapa HONGERA. Hongera nyingi zaidi naweza kuzitowa kwa Homeboy "Mbunge wa Nzega" kwa ujasiri wake mkubwa zaidi wa kuja hapa na kujianika wazi na GAMBA lake la KIJANI (CCM).

  Ukiangalia jinsi CCM wanavyopigwa madongo humu ndani kwa makosa ya wale wa juu (Magamba yenyewe) hadi unamshangaa huyu Mbunge kwa kuja hapa huku amejiweka lile bango la SHABAHA. Na watu TUMEMLENGA kwelikweli juzi na tena bila huruma.

  Kama ataendelea kuja hapa basi kweli ni NGOSHA wa nguvu. Nitamsisitiza aendelee kuja hapa na kujibu zile habari muhimu zinahusu hasa jimbo lake au maslahi ya TAIFA. Haya mengine wala asiwe ana hangaika nayo kama ambavyo hutamuona Dr. wa ukweli Slaa akijibu habari zinazomhusu yeye mwenyewe na maisha yake binafsi na hutamsikia akishambulia maisha ya mtu binafsi.

  Maadamu hapa tunaongelea UJASIRI wa hawa watu kuja na majina yao, basi hakuna haja ya kwenda zaidi ya hapo. Labda katika listi ongeza na Regia Mtema na mbunge wa Ubungo John Mnyika na wengine kadhaa ambao inawezekana siwafahamu.

  Kutumia au kutokutumia jina lako ni uamuzi wa mtu. Kila kitu kina gharama zake. Ila kwa Mwanasiasa kutumia jina lako hasa kuna ubaya wa aina mbili:

  1. Huwezi kuandika Pumba maana watu wanakufahamu.

  2. Utapashwa na kutukanwa sana na sisi tusiojulikana. Utakosolewa na kurushiwa madongo na kila aina ya mashambuli hadi uipate.

  Uzuri wake ni ule upande wa pili wa shilingi:

  1. Watu wanaokufahamu wataongea na wewe kwa heshima.

  2. Wengine watakupa mawaidha mazuri kwa faida ya nchi na wewe kama kiongozi. Kutoka kwao utasomeshwa shule nzuri sana katika mambo ya uongozi. Itakuwa kama umejianika wazi na kusema "nikosoeni na nijifunze kutoka kwenu."

  Hilo la pili, ndilo naona limewafanya hawa waje na majina yao. Ila wengine wakifikiria madongo, wanaona heri wajikalie kimya na majina yao ya bandia au kutokusajili kabisa.

  Nimalize kwa kuwapa hongera tena wote na zaidi Mbunge PEKEE wa Chama Cha Magamba kutoka Nzega. Kweli una ngozi ngumu ila wee endelea kudunda tu humu maana utajifunza mengi sana. Siyo yote humu ni Pumba. Kuna Pumba nyingi na MAZURI mengi tu......
   
 17. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #17
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Ndg. Mnataka na hapa ni-clarify kuhusu jina? Mimi naitwa Hamisi Andrea Kigwangalla wa mpanda Motto. Babu yangu aliishi maeneo ya Mlimani, Goweko na alikuwa maarufu kama Kigwangalla wa Mpanda Motto. Kwa sasa hivi yupo mdogo wake akiitwa Kigwangalla maeneo ya palepale Goweko - Mlimani. Asili ya baba yao na hawa babu zangu ni Kata ya Igalula, kijiji cha Chabutwa, na mpaka leo kuna 'mahame' ya ukoo wetu kwenye hizi sehemu mbili - maarufu kabisa! Majina yangu na asili yangu hayana utata kabisa, sema kuna watu wanapotosha kwa sababu za kutafuta umaarufu wa kisiasa na kunichafua mimi. Back home, nikiwa mtoto niliwahi kujulikana kama Hamisi/Saidi 'Bagaile' nikiitwa na watu wa nyumbani na wa mtaani kwa jina maarufu la mama yangu mzazi (ambaye pia alinilea na kunisomesha single-handedly). Bagaile si jina la baba wala la babu wala la ukoo, ni jina la 'kike' la kinyamwezi na ni 1st name ya mama yangu mzazi, ambaye anajulikana kama Bagaile Bakari Lumola (after her grandmother - Kwa wanaofahamu historia ya wanyamwezi vizuri:'Bagaile' alikuwa 1st born princess wa chifu wa wanyamwezi wa usaguzi aliyeitwa Lumola, pia alikuwa mke mdogo wa Mtemi Mirambo ambaye hakudumu kwenye ndoa hiyo). Kwa aliyenifahamu enzi zile aidha angeniita Hamisi/Saidi Kigwa au Hamisi/Saidi Bagaile. Wanaoileta hiyo story ya majina yangu wala hawanijui vizuri, wanayakosea kosea, wanayapindua pindua, na kwa mara ya kwanza ilianzia mwaka 2005 nilipogombea ubunge ambapo Ndg. Mgombea mmoja mwenzangu wa Ubunge wa Nzega ali-comission ikaandikwa kwenye gazeti fulani la kiswahili. Nilidhani iliisha lakini wapi. Akaiibua tena mwaka jana. Na juzi kaiibua kupitia watu wake. Sasa nimeazimia kuchukua hatua za kisheria ili kulimaliza kabisa hili. Uchunguzi unaendelea na muda si mrefu mtalisikia mahakamani.

  Otherwise, nawashukuru nyote kwa kujadili hoja na tuhuma mbalimbali zinazonihusu kwa ukali. Naomba nikiri kujifunza mengi kutoka humu. Mimi nadhani ni vema wawakilishi tukawepo hapa ili kupata elimu zaidi ya diplomasia na kusikia maoni na mawazo kutoka kwa watanzania ili tuwawakilishe vizuri bungeni!
   
 18. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Asante mheshimiwa,
  kwa kweli kwa sisi wengine hii ni chance ya pekee ku-interact na wawakilishi wetu.Mie binafsi nakupongeza.

  Hapo kwenye RED, am humbled by your acknowledgement..
  Kwenye BLUE, yes, ni platform nzuri, nadhani unaweza kuwa kama catalyst ya wana-CCM wengine kupenyeza baadhi ya hoja.. To be honest, JF inarepresent wasomi wa kila aina..
   
 19. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nimeyapenda majibu yako!

  Hongera sana mkuu

   
 20. R

  Rare JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimshukuru aliyeanzisha thread na pia nimtoe wasiwasi kuwa anonymity ni kitu kizuri tu mradi uko sahihi katika kile unachotaka kuwashirikisha wana JF, na kwa jamii ya watanzania.
  Mimi kwa mara nyingi wakati mwingi sipati muda wa kuchakingia mara kwa mara kwani napenda kusoma na kujifunza na kupokea taarifa mbalimbali.

  Kwa watu wanaojitokeza na kushiriki katika hoja inafurahisha kwani ni ukomavu wa kipekee na kujua si wakamilifu, na hata kama watafanya kitu sahihi watu wanaweza kuwapokea vinginevyo ama kwa kutoelewa ama kwa kutaka kupotosha, na ama vyote, tumshauri babu Msekwa kama anajua kubofya aje atoe mawazo yake humu badala ya kuattribute kiwanja hiki na viwanja vya watu ambao hawakulelewa ki vota fasta, japo wapo nadhani waliwahi kuchongwa na watu walioitwa UPE na kisha kukutana na mitambo kama akina shivji na akina kabudi, Chachage, baregu na wengine wengi. Namwomba Hamisi amweleze babu, alete hoja zake manake akiongelea jukwaani tu hawezi kujua twamdhani vipi naye atueleze wapi hatuko sahihi.
   
Loading...