Zitto, Slaa na Kigwangalla mifano ya kuigwa!

Mimi nadhani ni vema wawakilishi tukawepo hapa ili kupata elimu zaidi ya diplomasia na kusikia maoni na mawazo kutoka kwa watanzania ili tuwawakilishe vizuri bungeni!
Na hili ndo linakutofautisha na Babu yako Msekwa na wengi wa aina yake. Si wote walioko CCM wanaridhishwa na utendaji wa serikali ya chama chao, na hata namna ya kufikiri inatofautiana.
Mh. HAK, MD, ukiwa bungeni, kwanza uwe Mtanzania badae uwe mwanaCCM,
Sitegemei daktari na wewe uwe kati ya wale wagonga madawati kwa kila kinacholetwa na serkali.
Sitegemei upondeponde hoja iliyoletwa na serikali ya chama chako mwanzomwisho halaf kabla ya kukaa unasema unaunga MIA KWA MIA kwa sababu tu ni CCM!
Sitegemei kuwa utaziba masikio na kupinga kila hoja itakayotolewa na mbunge asiye wa chama chako bila kujali ina maslahi ya kitaifa au la.
Dr. HA Kigwa, make a name in the HOUSE by serving Tanzania siyo kulinda chama.
Historia haitakukumbuka kwa kupiga meza, na kutamka MIA kwa MIA ila kwa kuweka Tanzania kwanza na kuitetea bila ghiliba.
Mwisho nakupongeza kwa ujasiri wa "kujianika" jamvini.
Alika wengine.
 
Mi sikuelewi uliyeanzisha mjadala una lenga nini na utafaidika na nini zaidi ya kupoteza muda watu watumie majina yao ili iweje unataka kwenda kuwakopa au maana ishu humu ni hoja nA si majina ya watu ambao hawakupi mlo mazafaka
NAtofautiana.
Mara kadhaa hapa Jamvini kunatokea hoja inayohitaji wahusika walitolee fafanuzi, na ni sisi ndo tunawaambia kuwa "tunajua we mwanajamvi na huu mjadala unakuhusu hebu tupe fafanuzi"
Si mara moja wamejitokeza, Slaa (PhD), Zitto, Regia, Mnyika, na tumemshuhudia Kigwangala (MD) kwenye hii thread.
Bado kuna haja ya wanasiasa kuwemo humu jamvini kwa majina yao na pia kwa kutumia anonymous ID tunajua wanazo nyingi tu humu.
 
Ndg. Mnataka na hapa ni-clarify kuhusu jina? Mimi naitwa Hamisi Andrea Kigwangalla wa mpanda Motto. Babu yangu aliishi maeneo ya Mlimani, Goweko na alikuwa maarufu kama Kigwangalla wa Mpanda Motto. Kwa sasa hivi yupo mdogo wake akiitwa Kigwangalla maeneo ya palepale Goweko - Mlimani. Asili ya baba yao na hawa babu zangu ni Kata ya Igalula, kijiji cha Chabutwa, na mpaka leo kuna 'mahame' ya ukoo wetu kwenye hizi sehemu mbili - maarufu kabisa! Majina yangu na asili yangu hayana utata kabisa, sema kuna watu wanapotosha kwa sababu za kutafuta umaarufu wa kisiasa na kunichafua mimi. Back home, nikiwa mtoto niliwahi kujulikana kama Hamisi/Saidi 'Bagaile' nikiitwa na watu wa nyumbani na wa mtaani kwa jina maarufu la mama yangu mzazi (ambaye pia alinilea na kunisomesha single-handedly). Bagaile si jina la baba wala la babu wala la ukoo, ni jina la 'kike' la kinyamwezi na ni 1st name ya mama yangu mzazi, ambaye anajulikana kama Bagaile Bakari Lumola (after her grandmother - Kwa wanaofahamu historia ya wanyamwezi vizuri:'Bagaile' alikuwa 1st born princess wa chifu wa wanyamwezi wa usaguzi aliyeitwa Lumola, pia alikuwa mke mdogo wa Mtemi Mirambo ambaye hakudumu kwenye ndoa hiyo). Kwa aliyenifahamu enzi zile aidha angeniita Hamisi/Saidi Kigwa au Hamisi/Saidi Bagaile. Wanaoileta hiyo story ya majina yangu wala hawanijui vizuri, wanayakosea kosea, wanayapindua pindua, na kwa mara ya kwanza ilianzia mwaka 2005 nilipogombea ubunge ambapo Ndg. Mgombea mmoja mwenzangu wa Ubunge wa Nzega ali-comission ikaandikwa kwenye gazeti fulani la kiswahili. Nilidhani iliisha lakini wapi. Akaiibua tena mwaka jana. Na juzi kaiibua kupitia watu wake. Sasa nimeazimia kuchukua hatua za kisheria ili kulimaliza kabisa hili. Uchunguzi unaendelea na muda si mrefu mtalisikia mahakamani.

Otherwise, nawashukuru nyote kwa kujadili hoja na tuhuma mbalimbali zinazonihusu kwa ukali. Naomba nikiri kujifunza mengi kutoka humu. Mimi nadhani ni vema wawakilishi tukawepo hapa ili kupata elimu zaidi ya diplomasia na kusikia maoni na mawazo kutoka kwa watanzania ili tuwawakilishe vizuri bungeni!

naona nikiri kuwa haya ndo maelezo murua yanayokidhi hali zozote kutoka ktk kinywa cha mbunge. Haijalishi ukweli wa maneno ila kama mtu anatafuta maelezo,haya yanajitosheleza,labda mi ntabaki na "professional skeptism" kutokana na taaluma yangu kukataza kukubali kila kitu bila kuchunguza. Mi ntalizika pale utakapokuwa umempandisha Nassor/kigwangalla original kizimbani kwa kukusingizia kama kweli si kweli. Nakupongeza sana kwa kufika jamvini bila woga!
 
Back
Top Bottom