Zitto: Sitagombea ubunge 2015, Nitagombea Urais kupitia CHADEMA...

Status
Not open for further replies.
Nionavyo hapa kuna kazi kweli kweli cdm. Sawa ni haki yake lakini sijui kwanini wanacdm wengi wanawasiwasi na Zito. Mawazo yangu Zito itakapotokea asichaguliwe kugombea urais kwa kupitia cdm, Nasema na mtayakumbuka haya maandishi atahama chama. Ni maandalizi ya siri sana, ila hapa ukiyasema utapigwa mawe kuwa Zito hapendwi wakati hali liko wazi. Yetu macho bana usicheze na ccmafisi wale ni mafia wako tayari na kwa gharama yoyote kufanya lolote kuendeleza ufisadi wao. Kwa kumtafuta mtu wa kuwalinda ni mipango ya kuwagawa wanacdm. Ccmafisi wanasiri nzito ya Zito ambayo hawawezi kuitoa sasa wakati lengo lao bado subiri 2015.

Unaweza ukawa sahihi sana mkuu,na mawazo yako ndio mawazo yaliyopo akilini mwa wana Cdm wengi,kwa hiyo kama Zitto ataamua kuhama chama,litakua jambo la kheri na afya sana kwa chama cha Cdm
 
Zitto sasa afurushwe rasmi nje ya cdm.TUMEMCHOKA.
e

Ni bora kasema mapema ili wasingojea masalia watakaoachwa CCM ndio wasimamishwe kugombea Uraisi. Vile vile ni vizuri katamka mapema ili CDM waandae mtu wa kuchuckua jimbo lake.

kwanza amewatukana wazee wote Tanzania huku ni kukosa busara na hana sifa ya Uongozi kwani ni mbaguzi. Wapo Wazee waliozaliwa kabla ya uhuru na wanailetea Tanzania maendeleo na wapo wapuuzi waliozaliwa baada ya uhuru ni wapuuzi wa kutisha . Zitto hana busara kwa hili
Kauli hii inanikumbushwa maneno anayopenda kutumia Mbunge wa Iringa mjini kuwa tatizo haliwezi kumalizwa na mtu yule yule aliyelisababisha. Haa waze ambao wamekuwa wakuzunguza wizara mbalimbali tangu utawala wa Kambarage Nyerere hadi huu wa Jakaya Kikwete si watu wakuaminiwa na kupewa tena nchi; hawataweza kufikiri tofauti na walivyozoea.

Kama haujamuandika "out of context" Zitto anapaswa atuombe radhi tuliozaliwa kabla ya Uhuru, awaombe radhi na wazazi wake ambao bila wao, nna uhakika wote walizaliwa kabla ya Uhuru, asingekuwepo hapo alipo.
Haombwi mtu radhi mambo mengi nyie wazee mliamua kwenye vikao vya chama, serikali ambayo nyie ndie viongozi ikaenda kusimamia utekelezaji ambao haukutoa matunda zaidi ya kuwaongezea umaskini Watanzania. Mfano kwa nini Mwalimu Nyerere alianzisha kozi kama za Full Technician Certificate? Leo mnataka kila mtu awe na shahda ya chuo kikuu nani atakayefanya kazi ya kubadilisha belts, bearings? Tunahitaji kweli mtu wa shahada ya kwanza kufanya kazi za Bank Teller?

"Aleee wazee wa zamani kwaheri eeee!!!......... Akudo impact. Kwa wale wazee walioshindwa kuitumikia nchi wakiwa vijana na nguvu zao basi hata uzeeni hatuwataki.

Wazee kuna kazi zao kama wenyeviti, mabalozi na watendaji wa vijiji hizo bado tutawaachia waendelee kula posho za kusaini mikataba ya mauzo ya viwanja katika maeneo yao.


Inasikitisha sana kuona ndivyo itakavyo someka na wanaChadema wanaendelea kumpiga vita hata anapo exercise his right.. hapo ndipo napokoma na jamaa zangu.

Si miongoni mwao lakini kauli kama hizi zipokelewe kwa mtazamo chanya na ikiwezekana kwa majimbo yote watu waanze kujitokeza badala ya kungojea masalia watakaoachwa kwenye vyama vingine.
 
zitto sasa afurushwe rasmi nje ya cdm.tumemchoka.

yaani kama kuna mbunge wa chadema ninayemchukia kwa sasa ni - zitto kabwe
yaani ni mgomvi na mtaka madaraka sana.

Hivi yeye ndiye anajichagua au anapendekezwa na wanachama wa chadema?

Ukiona mtu anasema anataka kugombea urais kama zitto mapema kiasi hiki ujue ana uchu wa madaraka
tena tuna mkanya aache upuuzi huo na kwanza aende ccm.

Tumemchoka analeta malumbano kwenye chama mara kwa mara
mimi zitto akichaguliwa kugombea urais chadema simpi kuara yangu ngoooooooo
nitampigia mgombea wa wa ccm
asanteni
 
Zitto sasa afurushwe rasmi nje ya cdm.TUMEMCHOKA.

Huu ni ufinyu wa mawazo na upumbavu.
Kisa kasema atagombea uraisi au?
kwanini mnadhani yeye kusema hivo ni dhambi?
Kwanini hata kama mnadhani hayupo tayari kwa sasa,msi mfikirie
kwenye nafasi ya makamu wa raisi ili 2020 awe tayari?

Acheni utumwa wa kifikra.
 
Ninachokiana mimi hapa ni kweli zitto anatumiwa na ccm, ila yawezekana hana nia ya kugombea urais na yeye analijua hilo kutokana na kushuka kwa credibility yake cdm, kwanza anazo sababu za kutokushiriki M4C kwa maana kwamba ana-feel guilty kwa kuisaliti cdm katika occasions mbalimbali.
Anachokifanya ni ku-divert attention ya watu toka CCM dodoma kujadili matokeo ya uteuzi na sasa kutwa nzima ya leo tutajadili kauli ya zitto.kwa hiyo zitto amekatiwa specifically kuhakikisha attention ya watu ihamie kujadili zitto na hilo kaliweza zitto maana leo ndiyo tunachofanya.
Kwa sasa watanzania wamemuelewa zitto undumila kuwili wake na hivyo hawawezi kufanya makosa yaliyotokea ezni ya nccr-mageuzi. Kwa ujinga wa ccm na kukosa ubunifu wameamua kutumia njia ile ile kwa akili ileile kwa kazi ilele.NO INNOVATION
 
Inawauma sana Zitto akiondoka na toto lenu na Mujini eeeh!.. Msijali Zitto bado hana umri wa kugombea lakini haina maana haruhusiwi kusema wazee wang'atuke. Ubaguzi gani wakati umefika kweli wang'atuke? Je wao sio wabaguzi kung'ang'ania nafasi za juu ktk uongozi kwa miaka zaidi ya 50 wakiwaachia vijana makapi!.. Wengine tutakula wapi aaah! Mpaka Mungu awalazimishe kwa vifo jamani..

mwenye masikio haambiwe sikia na mwenye macho haambiwi tazama. mkuu hebu jiulize kwanini zitto?
 
e

ni bora kasema mapema ili wasingojea masalia watakaoachwa ccm ndio wasimamishwe kugombea uraisi. Vile vile ni vizuri katamka mapema ili cdm waandae mtu wa kuchuckua jimbo lake.


kauli hii inanikumbushwa maneno anayopenda kutumia mbunge wa iringa mjini kuwa tatizo haliwezi kumalizwa na mtu yule yule aliyelisababisha. Haa waze ambao wamekuwa wakuzunguza wizara mbalimbali tangu utawala wa kambarage nyerere hadi huu wa jakaya kikwete si watu wakuaminiwa na kupewa tena nchi; hawataweza kufikiri tofauti na walivyozoea.

haombwi mtu radhi mambo mengi nyie wazee mliamua kwenye vikao vya chama, serikali ambayo nyie ndie viongozi ikaenda kusimamia utekelezaji ambao haukutoa matunda zaidi ya kuwaongezea umaskini watanzania. Mfano kwa nini mwalimu nyerere alianzisha kozi kama za full technician certificate? Leo mnataka kila mtu awe na shahda ya chuo kikuu nani atakayefanya kazi ya kubadilisha belts, bearings? Tunahitaji kweli mtu wa shahada ya kwanza kufanya kazi za bank teller?



wazee kuna kazi zao kama wenyeviti, mabalozi na watendaji wa vijiji hizo bado tutawaachia waendelee kula posho za kusaini mikataba ya mauzo ya viwanja katika maeneo yao.




si miongoni mwao lakini kauli kama hizi zipokelewe kwa mtazamo chanya na ikiwezekana kwa majimbo yote watu waanze kujitokeza badala ya kungojea masalia watakaoachwa kwenye vyama vingine.
hata mimi nautaka urais pia
 
Ana haki ya kikatiba kugombea nafasi yoyote, muda ukifika CDM kitaangalia kati yake na wengine watakaojitokeza ni nani ataweza kusimama ili CDM itwae dola, kuanza kumshambulia sioni kama ni vyema,
 
....what...!!! This guy is a kid, child, baby mentally.... 100%
eti aliyezawaliwa KABLA YA UHURU.... MEANING he is attacking DR. Slaa openly, insulting....very silly guy, .... Ana uchu wa madaraka sana huyu.... KWANZA ATUELEZE HONGO ZA HELA ZA MAFUTA ZA IPTL ALIKUWA ANAJIDAI HATAKI BUNGE ALLOWANCES ZIENDE JIMBONI KWAKE KUMBE MLA RUSHWA MKUBWA.... HE IS COMPARING MALAYSIA & Tz, meanwhile yy ndiye mla rushwa mkubwa, mzee wa Vogue, HUMMER, katoa wapi.... Uwizi tu.....
He is not even fit to be a presidential aspirant.... Hajatulia huyu mpepeeni, huyu vp..! eeh katumwa nn...!!! Akacheze mziki....
Halafu maneno yake yansmharibia, eti aliyezawa kabla ya uhuru.... what a local/silly/poor statement, MP mzima anaongea hovyo hovyo....like he is talking to his gf....
 
Kuna ubaya gani lakini mbona nilichoelewa ni kwamba Wazee wang'atuke waachie vijana. Ebu jiulize wewe mtu alikuwepo madarakani toka tupate Uhuru ina maana huyu alikuwa kijana wa miaka 18 kuendelea, leo hii miaka 50 baadaye bado anataka kuwa madarakani... Come on now ukishafika miaka 70 kuwa mlezi wa chama, pilka pilka hutaziweza, kubali kuitwa babu waachie wengine waiendeleze familia.

Ni kweli,kama huwezi pilika pilika za chama achia ngazi.
Lakini yeye anae msema hapo ni slaa.
Sasa kati ya yeye anae jiona kijana,na slaa nani anaweza pilika pilika za chama?
 
Me sioni shida mtu anapotangaza nia yake hadharani, zitto anaonyesha yeye si mnafiki ila ni mkweli, na mara nyingi watu kama yeye huwa wanachukiwa, me naamina kila mtu anapenda kushika wadhifa huo mkubwa katika nchi ya Tanzania, tatizo ni wachache wanaojiamini hadi kusema hadharani kama zitto. Kila la kheri brother I wish you all the best!, keep on saying brother eventually it will materialise, mwanzoni lazima iwe ngumu kwa watu kukubali lakini kadri unavyozidi kusema it become real!
 
At best as simplistic as saying "vijana bado hawajakomaa kisiasa".

Different ends but the spectrum is the same.

This immature diction, plagued with a panache of plaques immersed in relentless abandon to common decorum and a knavery full of wanton reductivism is unbefitting a gentleman simpleton, let alone an aspiring statesman of supposedly Herculean proportions.

he! Mkuu hapa ulikuwa unanena kwa lugha?
 
Kama maneno haya, "Jukumu la kuleta maendeleo haliwezi kuletwa na aliyezaliwa kabla ya uhuru." kweli yametamkwa na Zitto basi amepotoka, ajifunze kufikiri kabla ya kukurupuka na pia kuwaheshimu wakubwa zake. Wako wengi tu waliozaliwa kabla ya uhuru ambao wanaweza kusimamia jukumu hilo ipasavyo.
 
Katika kauli ya huyu mh. Nayaona yafuatayo;1)Ukaburu\ubaguzi wa waziwazi kwa kigezo cha umri.Napata tabu kuelewa kuwa baada ya umri kitafuata kipi,lakini akina Lau,Malima,Ngeleja you name them walikuwa vijana...see what they have done!2)Kuingilia mchakato wa katiba mpya;Sijui ni nani kampa uhakika kuwa umri wa kugombea UTAPUNGUZWA,is he trying to read a letter in the envelope!?3)Poor timing;kwa uchaguzi wa 2015 kuanza kutangaza nia sasa si sahihi,huu ni wakati wa kuendelea kujenga poilitical base,sasa wakati wengine wakiwa huko vijijini kuna MAALWATAN wako busy kutangaza nia ya urais(of which reminds me of the coca colla advert 'I love Africa')4)Arrogance at its peak;maneno kwamba sijui tulioanza nao sasa hawapo mara oh kuna wanajifanya CDM wanaijua xana is simply el crapiso!!!Kwasasa niishie hapa niende kibaruani....

baregu na shivji ndo wamemthibitishia umri utapunguzwa kwenye katiba mpya
 
Kwa hilo la umri nadhani amepotoka sana. Anataka urais wa Tanganyika au Tanzania? Anazungumzia "uhuru" wa nchi gani?- Tanganyika, Zanzibar au Tanzania? Kwa nini? Ni nini kitachomfanya mtu aliyezaliwa 10 December 1961, kwa mfano,kuwa rais bora zaidi kuliko yule aliyezaliwa 8 December 1961?

..."Wazee wetu walitusaidia kutupatia maendeleo ya kisiasa, sasa ni jukumu letu kuleta maendeleo ya kiuchumi. Ila naomba nisisitize, jukumu hili haliwezi kutekelezwa na mtu yeyote aliyezaliwa kabla ya uhuru.."
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom