WanaJF,
Zitto awapa za uso UKAWA baada ya kujibu hoja kuhusu tabia iliyozoeleka ya wapinzani kuingia ndani ya bunge, kusaini posho na kisha kuleta vurugu makusudi ili wakimbie bunge.
Zitto kwa upande wake ameeleza kuwa, kwanza hapokei posho na kana kwamba hiyo haitoshi, kamwe hawezi kulikimbia bunge.
Rai: Mbowe na Nyumbu wako jifunzeni hili kutoka kwa Zitto.
wewe huna akili kama wabunge wa SISIYEMU,
Hebu niambie 2004 Waziri wa Elimu MUNGAI kipindi hicho alifuta masomo ya ufundi,biashara, kilimo na kuyachanganya Physics with Chemistry
lakini alivyowasilisha bungeni wabunge wa SISIYEMU Walishangilia na kuipitisha Bajeti kwa mbwembwe huku wakijua kbs kilimo ni uti wa mgongo wa Watanzania zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania wanategemea kilimo.kwnn nasema wabunge wa sisiyemu hawana akili km wewe? jibu ni kwamba hivi wewe unaweza kukata uti wa mgongo wa mwili wako halafu ukafurahia kuwa utaendelea kuishi ? Wabunge wa upinzani walipinga lkn waliowengi wakaipitisha kwa mbwembwe.Halafu mwaka 2006 haohao wa sisiyemu wakarudisha hayohayo masomo,kwa maana nyingine wakaramba matapishi yao
Naye Waziri kawambwa alipokuwa Waziri wa Elimu akaazisha mtihani wa drs la saba wa kuchagua na G.P.A kwa matokeo ya sekondari na vyuo vya ualimu,wakati anawasilisha hoja bungeni wabunge wa sisiyemu alipinga makofi kwa mbwembwe kama kasuku,wakati wanajua kbs kwamba G.P.A sio kipimo cha kumpima mwanafunzi kwa kuwa hakionyeshi tathimini halisi ya ufaulu.Lkn kwa kuwa wanajivunia uwingi wao wakaipitisha.Mwaka huu tumeona tena wanaramba matapishi yao kwa kufuta G.P.A na kurudisha mfumo wa Division
Bunge hili tena wamekuja na mpya ya TBC isionyeshe Live ila ionyeshe tuu saa nne za usiku,bunge linatumia masaa sita kwa siku itakuwaje ionyeshwe kwa saa moja?huu ni umasikini wa fikra wa wabunge wailowengi,kwa maana wanataka TBC wapate muda wa ku edit ili waonyeshe vipengere vichache na vzr tuu vya serikali.Eti serikali inabana matumizi, kama ni kubana matumizi kwann wasipunguze posho zao ili wabaki na mshahara tuu kama wana nia ya dhati ya kupunguza matumizi?? au kama wanaona ni gharama basi waachie vyombo binafsi viendelee kuonyesha? TBC inaendeshwa kwa kodi za wananchi kwnn wanachi haohao wasiangalie bunge Live? je nani amewaambia wabunge wa sisiyemu kuwa kero kubwa ya wananchi ni kuonyeshwa kwa bunge live?? kweli huu ni umasikini wa fikra hata Rais nadhani anawashangaa kwa maana hawamsaidii bali wanampa wakati mgumu Magufuri atakapo kuwa anafanya kampeni 2020 maana ataona wananchi wanazidi kuichukia serikali kwasbsb ya upuuuzii huuu wa wabunge wa sisiyemu kuendelea kushabikia chama chao baadala ya maslahi ya Taifa.kama kweli mtastisha bunge si muda mrefu mtaramba matapishi yao maana wananchi tulikuwa na Imani na Magufuri lkn kwa dalili hizi sisiyemu ni ile ile hakuna maendeleo chini ya utawala wa sisiyemu hata iweje?.Nakuomba Rais Magufuri tumbua majipu ya mawaziri wanaokuangusha Mfano NAPE anakuangusha,na amefanya tuichukie serikali kwa kutunyima haki zetu.
JIBU tuhuma hii wewe unafikiri ni sababu gani za msingi zinazopelekea ukubali kuwa bunge lisionyeshwe Live ? majibu yako ndo yatatoa tathimini kama una akili au huna km wenzio??