Zitto Sio wa Muhimu Kiasi Hicho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Sio wa Muhimu Kiasi Hicho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Goodrich, Mar 26, 2012.

 1. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Nimeona watu wengi wanatumia muda wao mwingi kujadili upuu zi wa Zitto.
  Ninaita upu uzi kwa kuwa niliusoma kwenye blog yake na kuutafakari. Kwa upeo wangu naona hana lengo la kugombea Urais, ila ana nia nyingine labda kujiweka juu ya viongozi wote CDM au kuonyesha kuwa yeye ndie kawalea kina Mnyika, Mdee nk na kwamba Dr Slaa hana umuhimu kwake, au pengine lengo lake ni kuonyesha kuwa Januari ni mtu wa muhimu zaidi kwake kuliko wanachama wenzake wa CDM.
  Lakini inaleta maana kudhani kuwa lengo lake ni kuivuruga Chadema wakati huu mgumu wa Kampeni Arumeru.
  Kuwajulisha tu mnaopoteza muda kwenye hoja za ndugu zitto ni kuwa, huyu Bwana yupo idara ya usalama wa taifa, na alikubali kununuliwa baada ya sakata la buzwagi. Yupo upinzani kama kibaraka wa CCM, anatumika kila inapobidi.
  Wanaomjua zitto wanakili kuwa kwa sasa hana unuhimu kwa taifa, na hivyo hana umuhimu kwa Chadema.
  Zitto ni mtu anayenunulika kirahisi, anajijua kuwa kwa sasa hakubaliki, na hiyo kutangaza nia kwake ni kwa lengo la kukivuruga CDM.
  Ila kama hujanielewa unaweza kwenda Zitto na Demokrasia utasoma alichoandika na pengine kujua nia yake.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Yeye kautaka urais, je, nani atampa?
   
 3. M

  Martinez JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Kwa sasa Zitto hana tofauti na Shibuda ndani ya Chadema.
  Nimeusoma waraka wake kwenye hiyo blog yake, ukweli ni kuwa jamaa ni kibaraka kabisa na anatumika kwa malengo maalumu.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,596
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  sio wa muhimu wakati umemuanzishia thread???
   
 5. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama hana umuhimu why all this fuss?
   
 6. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mwacheni agombee Katiba inamruhusu na hata ikija mpya tutaweka umri agombee
   
 7. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Ana haki ya kugombea, hata wewe una haki ya kugombea.
  Nimepost thread kuwajulisha behind the scene baada ya kuona wana CDM tunaacha mambo ya msingi na kujadili mislead alioanzisha zito wakati usio muafaka.
  Kumbuka zitto anatumiwa kila CCM inapoona kuna haja ya kumtumia, ni kibaraka.
   
 8. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mwacheni agombee Katiba inamruhusu na hata ikija mpya tutaweka umri agombee
   
 9. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Zitto is a papet of magamba tulimuamini lakini kumbe ni mbwa mwitu aliye vaa ngozi ya kondoo!!!
   
 10. Codon

  Codon JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ukizozana na kichaaa?Hapo kwenye urais kuna kichaa kinaanza!Mbivu nambichi tutaziona muda ukifika!
   
 11. M

  Martinez JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Suala sio Urais. Na wala hakuna anayeweza kumpinga yeyote, hata wewe kugombea. Suala ni Je, huu ni wakati muafaka?
  Lakini pia suala la pili ni tabia yake ya kupenda kumfagilia Januari Makamba wakati kwenye Chama chake kuna wabunge wenzake wazuri sana.
  Hata ukisoma hiyo topic kwy blog yake, utaona imejaa dharau kubwa kwa viongozi wake na wanachama wenzake.
  Zitto ni kibaraka !
   
 12. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Labda ungeenda kwenye hiyo blog yake usome post yake ndio utajua nia yake sio kugombea, bali kuivuruga Chadema.
   
 13. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi nakuunga mkono, Zitto anajua siasa sana, hajafanya alichokifanya kwa bahati mbaya, amemaanisha kabisa kufanya hivyo. Na huenda ni kweli ni katika jitihada za kuisaidia CCM iweze kushinda Arumeru Mashariki! Ila CCM + Zitto tunawapiga Arumeru!
   
 14. +255

  +255 JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,909
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Nimeisoma hiyo makala ka mara tatu sijaona wapi alipokosea kuandika, ila nimegundua haters wa Zitto wapo wengi sana af hawana sababu za maana hata kidogo>>>>
   
 15. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  +255 Post zako zoote huwa unaipigia debe CCM na kuiponda Chadema, leo imekuwaje ?
   
 16. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #16
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Next time unapotukana walau usijijumulishe katika hilo tusi ulotoa.... Inakufanya uonekane hujui nini hasa Unaongea. Labda sababu I like Zitto ila Ukweli unabaki kua ame voice lile ambalo anafikiri; na majority badala ya kuchukua ujumbe ule, kila mmoja ana tafsiri yake mwenyewe ambazo most ni half wrong na half right pia. Na hapo ndio jamii hufurahisha kweli wakati wa kujenga hoja... Yule ambae anatoa maoni juu ya Zitto ambayo wayakubali unakimbilia kujudge moja kwa moja ndio amjua Zitto; yule atae sema tofauti basi amjui...
   
 17. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Ni kijana jasiri na anajua nchi inaenda wapi. Ninachokikataa kwa yeye kugombea Uraisi ni kuwa bado anaupenda ukomunisti . Halafu aliinua mioyo ya watanzania pale alipofichua mikataba haramu ya madini. Maana watu walimshauri asiingie katika tume ya kuchunguza mikataba ya madini ila yeyey alijitosa mpaka akaingia. halafu hakusema lolote mpaka leo ingawa mikataba yote ya madini haijapitiwa upya.

  Tulidhania baada ya kumalizika kwa uchunguzi wa tume yake ya madini angevalia njuga kutaka mikataba ya madini isukwe upya lakini kanyonda! alivulia maji nguo lakini hakuyakoga hapo ndipo Zitto aliponichanganya akiri. Mpaka leo sijui kama he is the hero or a traitor
   
 18. William Mshumbusi

  William Mshumbusi JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 874
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  SI HAYO TU HUYU NI MPINZANI NDANI YA UPINZANI. Si wabunge wa upinzani ata wasisiemu wapigania haki hawamwamini. DA NANI KAONA UNAFAA AKAKUPENDEKEZA WANASIASA HASA WABUNGE FANYA KAZI HASWA WATU WAKUPENDEKEZE NI AIBU KUJIPENDEKEZA MWENYEWE AIBU AIBU AIBU TUPU mi nafumba macho
   
 19. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  zitto ni noma kanafiki kama nini.ADC NI MHASISI KWA NYUMA KUNA NGUVU ZAKE.ASA ZITTO USITULIPE HELA ZETU UTAJUTA
   
 20. I

  ITSNOTOK Member

  #20
  Mar 27, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijawa na mengi sana ambayo nayajua kuhusiana na Zito. Lakini katika wale CHADEMA 100% zito si mmoja wao kwa sasa ninavyoona mimi. Hayo maneno kwenye bold hapo juu ndiyo hasa niliyoyafikiria kuhusu yeye kwa muda mrefu kidogo.
  Nakumbuka kuna mgogoro wake na CHADEMA uliwahi kutokea hapo kabla, hii ilipelekea mama yake Mzazi (wa Zito) Kuingilia kati kumuonya mwanaye huyo kuhusiana na tabia zake (anayekumbuka atachangia zaidi). Lakini pia hapo nyuma kidogo alishatangaza kuwania Urais ingawa baadae ikasemekana alikuwa na lengo hilo lakini haikuwa ni lazima kupitia chama cha CHADEMA.

  Kwa hili la sasa, nafahamu Zito anafahamu kabisa kuwa bado hajaaminika kiasi kikubwa akilinganishwa na wenzake ndani ya CHADEMA (kwa kuangalia kuanzia jimboni kwake -ameshinda kwa kura ngapi uchaguzi uliopita- , ni majimbo mangapi anayokubalika hapa Tanzania (research ?, au alishagombea? .......) pamoja na yote, anatakiwa kufanya kazi kubwa kuwarudisha watu kwenye mstari. Kutokana na hilo haikuwa sawa yeye kujitangaza ingawa ni haki yake, hasa kwa kuwa nilimtegemea kuwa ni mmoja kati ya watu wanaoweza kuitetea Tanzania na matatizo makubwa yaliyopo sasa - sitayataja- (mtazamo wangu). Kuanza kusambaza nguvu ambayo imeshaanza kuaminiwa na Watanzania nadhani ni lengo linaloonyesha upande wa mtu. Zito ni mzuri sana hasa anapowasilisha hoja za CHADEMA, anavyoibua hoja na alivyo na msimamo kwenye hoja za CHADEMA, lakini migogoro kama hii ndiyo inayoongeza umbali kwa wanaCHADEMA kumfikiria kwa asilimia 100.

  Nikiamini Zitto anafahamu anachokifanya, nafikiria zaidi analenga kukivuruga chama chake, nafikiria Zitto anatumiwa sana na Chama kinachotawala hasa ukifuatilia kauli mbali mbali ambazo wabunge wa Chama tawala wamekuwa wanatoa kwake katika vikao vya bunge mfano...(tunakuheshimu sana Zitto).. huwa sifikirii kama huwa ni heshima ya kawaida kwa kuwa, muda kama huo huwa yupo katika uchangiaji makini katika hoja fulani ambayo inaumiza utawala. Hii humaanisha kumpunguza nguvu katika kuchangia suala hilo na hasa kwa kuwa anafikika, natofautisha na Mnyika, na wengine ambao bado hajaambiwa kwamba wanamheshimu kwa namna ambayo zito anapewa.

  Katika kuamini hilo pia, Zito anafahamu chama chake kina utaratibu karibu wa kila jambo, wanafahamu ni kitu gani kinatakiwa kitamkwe wapi na namna gani. Hivyo kwa Zito kuamua kufanya vile anavyoona anapenda ni wazi kwamba anaamua kwenda kinyume na taratibu zao walizojiwekea, na hivyo anapaswa kufuatiliwa aangaliwe.
  Ninaona Zito anabebwa zaidi na chama kuliko yeye anavyokibeba chama kwa sasa, ni gharama sana kumtunza Zito.
   
Loading...