Zitto: Serikali inasema uongo, ni muhimu Bunge lichunguze ziliko shilingi trilioni 1.5

jamani najua humu ndani kuna watu wanafanya ofisi za NAO hvi toka lini CAG anakagua makusanyo yanayokusudiwa,siku zote ukaguzi unafanyika kwa kilicho pokelewa na kilicho tolewa.
 
Mi kilichonishangaza ni hizo bilion 203 za zanzibar,
zimekusanywa kutoka kwenye nini hasa,mbona nyingi sana?,
kuna documents zanzibar kuprove kuwa zimopokelewa na zinaonekana kwenye mahesabu?.

Follow the money trail.....

-kuna documents zinaonyesha malipo ya bilioni 600 na ushee kuonyesha kulipa hati fungani,etc

haya mambo wala hayahitaji kugombana,ni kiasi cha kueleweshana tu,ili kuondoa sintofahamu au kuwajibisha watu,hakuna sababu ya kutishiana DPP or whatever,kuhoji ni kazi ya mbunge ,na anapohoji kwa niaba ya wananchi,apewe maelezo ya kuridhisha ili wananchi waridhike
mkuu kama wangepeleka hizo nyaraka kwa CAG ku verify hayo wanayoyasema hiyo hoja isingekuwepo kwenye riport ya CAG,na CAG asingeweza kuonyesha utofauti wa hela zilizkusanywa na zilizotumika! ni dhahiri kuwa hizo hela zitakuwa hazipo
 
Tatizo la Zitto kujifinya aba akili kuliko watu wote.Kazima ufafanuzi wa serikali aupinge kwa sababu anajua ameshaumbuka.Chadema alitimuliwa kwa kujifanya mjuaji kuliko wote akaondoka na kuanzisha chama chake ila sasa huku anachezea pabayaKutaka kuupotosha umma wa Watanzania kwa kutaka umaarufu kutamsumbua sana.Kiburi na majivuno ta Zitto viliudhi wengi pale alipomjibu waziri lukuvi kwa kejeli kwamba 'hamna fedha ' . Ukishaiambia serikali kwa kiburi,dharau na kejeli kwamba haina fedha, sasa mwenye fedha ni nani? TUACHE KABISA KUMUENDEKEZA ZITTO SASA.
na ww tumia akili ukisoma report tu unaona tofauti ya hela sio lazima akwambie zitto
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Serikali Inasema Uongo, Ni Muhimu Bunge Lichunguze Ziliko 1.5 Trilioni

-Taarifa Ndogo ya ACT Wazalendo Juu ya Majibu ya Serikali Bungeni Juu ya Ziliko 1.5 Trilioni Zisizoonekana Matumizi yake Kwenye Ripoti ya CAG

Tumesoma majibu ya Serikali kuhusu hoja ya Ukaguzi wa shilingi 1.5 trilioni za umma ambazo hazijulikani zilipo kama yalivyosomwa na Naibu Waziri wa Fedha asubuhi hii bungeni. Ni maelezo yale yale aliyoyatoa Katibu Mwenezi Taifa wa CCM, ambayo tayari jana yamejibiwa na Katibu Mwenezi Taifa wa ACT Wazalendo, ndugu Ado Shaibu.

Kwa sasa tuna machache tu ya kueleza:

1.Serikali imesema uongo. Taarifa ya Serikali ya leo na Taarifa ya Fedha ya Benki Kuu, wanaotunza Fedha za Serikali hazisomani kabisa. Tutaongea na waandishi kueleza hili kwa undani zaidi. Ijulikane tu kuwa akaunti za Serikali kwenye Taarifa za Fedha za Benki Kuu hazina hizo Fedha Naibu Waziri ametaja.

2.Ni dhahiri kuwa kuwa ubadhirifu mkubwa wa Fedha za Umma, ndio maana taharuki ya Serikali ni kubwa, kiasi cha majibu ya Serikali kupewa Kiongozi wa CCM kuyasema, na kwa kuwa kashindwa kukonga nyoyo, sasa imebidi Serikali ije yenyewe kuyasema majibu yale yale yaliyosemwa na CCM. Tunashuhudia Kwa mara ya kwanza Zanzibar ikikusanyiwa zaidi ya TZS bilioni 200 Sawa na 20% ya Bajeti nzima ya Zanzibar, makusanyo yote ya TRA Zanzibar na mara 10 ya makusanyo ya Zanzibar kutoka PAYE za Muungano ambazo ndio pekee hukusanywa na TRA. Uongo huu wa Serikali ya CCM lazima unasukumwa na Wizi. Zanzibar hukusanyiwa TZS bilioni 21 tu na TRA, 200B zatoka wapi? Balaa

3.Sisi ACT Wazalendo, tunaendelea kumsihi Spika wa Bunge aruhusu Ukaguzi Maalum wa matumizi ya Shilingi 1.5 trilioni kupitia Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC, kwani hata haya majibu ya Serikali yanapaswa kuhakikiwa kwanza na CAG kabla ya kusomwa Bungeni, jambo ambalo halikufanyika. PAC wanajua kuwa makusanyo ya Serikali ni CASH BASIS na sio accrual. Serikali imedanganya, lazima PAC sasa wafanye kazi yao.

Muhimu: Tamko la Serikali ni matusi Kwa CAG. Watanzania mjiandae kuilinda Taasisi ya Ukaguzi wa Taifa. Serikali ya CCM inataka kuivunja vunja taasisi hii ya uwajibikaji. Tusikubali.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Aprili 20, 2018

Pia, Soma Naibu Waziri wa Fedha atoa kauli kuhusu kutoonekana kwa sh. Trilioni 1.5 kwenye ripoti ya CAG

Mh Zitto, ni fedheha kwako, kama Mbunge, kuonesha umbumbu wako kwa madai kwamba Tumesoma majibu ya Serikali kuhusu hoja ya Ukaguzi wa shilingi 1.5 trilioni za umma ambazo hazijulikani zilipo kama yalivyosomwa na Naibu Waziri wa Fedha asubuhi hii bungeni. Utaheshimika ukiyakanusha kwa ushahidi.

Mh Zitto elimu yako ya "Financial Accounting/ Management" ni ya kuungaunga hata unashindwa kutofautisha kati ya "Revenue" na "Cash".

Mh Zitto na usomi wako hujagundua tofauti ya taarifa iliyomo kwenye ripoti za CAG (ya Kiingereza na Kiswahili), kuweza kujisahihisha na kuomba radhi?

Ripoti ya Kiiengereza (Ukurasa wa 32) imeandikwa: Out of the collected revenue of TZS 25,307.48 the Treasury released TZS 23,792.30 billion for Personnel Emoluments, Other Charges, Development and Consolidated Financial Services.

Wakati katika Ripoti ya Kiswahili (Ukurasa wa 34) imeandikwa Kati ya Shilingi bilioni 25,307.48 zilizokusanywa, Shilingi bilioni 23,792.30 zilitolewa kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi, matumizi mengine, matumizi ya maendeleo na fedha kwa ajili ya kulipa madeni yatikanayo na amana za Serikali pamoja na riba.

Pia Mh Zitto, naamini pia unajua tofauti ya "Profit and Loss (Income) Statement" na "Cash Flow Statement" kutambua CAG alimaanisha nini kuhusu hiyo tofauti ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2916/17.

Kama alivyoandika Mh Mdee, ukampamba, siyo tu uombe radhi ila nawe CHUTAMA ujisetiri. Kichwa chako kiko tupu.
 
sasa hapa ndio umeeleza nini!!!!!!!
 
Zitto mpenda kamati,hatuna hela ya utani ya kuwapa hao watu wa kuchunguza huo upuzi,hizo hela mnazitaka mjipitishie wenyewe ili mzile kwa ulaini,tume ngapi za kuchunguza matukio zimepatwa kuundwa na kinacholetwa ni upuuzi tu.Kwanza tuambie ahadi yetu uliyosema utawataja walioficha pesa yetu Uswisi, jinsi miaka inavyozidi kwenda Zitto anazidi kuwa mzito kuelewa.

Kwanza tumchunguze yeye kwa alivyokuwa anaitumia vibaya kamati ya mashirika ya umma alipokuwa mwenyekiti wa hiyo kamati na atwambie huo utajiri kaupataje wakati hadi anamaliza Chuo Kikuu alikuwa lofa tu na hajawahi kufanya kazi yoyote zaidi ya ubunge. Kama ubuge ni utajiri basi wabunge wote wangekuwa mamilionea kama alivyo Zitto.
..ila pesa za kununulia wabunge na madiwani mnazo!
 
Back
Top Bottom