CCM yalisema UKAWA haiwezi kufika mwezi mmoja tangu waondoke bungeni BMK, wakasema ati posho itawarudisha wengi. Hakurudi hata mmoja. Wakasema madaraka yatawasambaratisha kwani kila mmoja ana uchu wa madaraka. Mpaka leo, uchaguzi wa serekali za mitaa umeonesha ukomavu wa UKAWA yene miezi tuu tangia izalike.
Sasa, walisema akiondoka ZZK CDM kwisha habari. Wakaona hakuna mtikisiko. Sasa wanataka kumleta UKAWA ili waseme CDM ni wabaguzi, lazima wampokee kwani ni wa upinzani.
Waambieni maccm, ACT si wapinzani, walianzishwa na ccm kuuharibu upinzani, wamefanikiwa kumnasa huyo mbigili zzk ili akiweza tu kuupenya upinzani, baasi aanze fitna zake na mbwembwe zake atuvuruge. Tumejitosheleza, hatuhitaji mtu mwenye mvuto wake pekee, tunataka chama chenye mvuto sio mtu.
Ushauri kwa zzk, amwone mzee wa Kiraracha, amwone mzee mapesa, wako kina UPDP wako wengi tu waliokaa BMK wakivuta noti zao. Huo ni mtaji tosha kununulia kura.
Sisi tulio waachia hizo noti, hatuna kitu cha kuhonga, tutawaendea wananchi tuwaeleze ya moyoni hatuhitaji kujulikana kwa mtu ni chama. UKAWA yatoshaaaaaa.