Zitto: Nimechukua hatua juu ya taarifa za tishio la maisha yangu, chama changu kitatoa taarifa baadae

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Ninafahamu kuhusu taarifa zinazosambaa juu ya tishio la maisha yangu, chama changu kimechukua hatua dhidi ya taarifa hizo. Maelezo zaidi yatatolewa katika wakati muafaka.

Zitto.png


Issue ilianzia hapa.
IMG_20180422_211443.jpg
 
Utawala huu kila kona ni vilio vya matishio tu.
Ngoja ninukuu maneno ya Askofu Bagonza leo

Kasema:

Hatuna duka linalouza hekima. Hakuna mganga wa kienyeji toka Sumbawanga anayeweza kuzindika hekima. Hatuna daktari wa kufanya operesheni kuingiza hekima kichwani. Hakuna muujiza wa maombezi kuingiza hekima vinywani na kwenye bongo zetu.

Uzoefu (experience), haina mbadala. Twazingatia:

-Ukiwa mwongo, usiwe msahaulifu.

- Ukijifunza wizi, jifunze na kukimbia.

- Ukikosa uaminifu, jifunze uangalifu.

- Usibadili aibu kuwa hasira.

-Asojua ubaya wa makalio, huyageuza mto wa kulalia.

- Waweza kuwadharau siafu, lakini huwezi kuwakalia.

- Nyumba yenye njaa, haikosi kelele.

Mungu wetu ni msingi wa demokrasia. Aliumba wenye nguvu na wanyonge, wajinga na werevu, watawala na watawaliwa. Uhuru wa mihimili ni utashi wa muumba ili amani iwepo. Mungu akikupa nguvu anakunyima hekima ili ushauriwe; akikuumba mfupi, anakupa akili za kutumia warefu wakuchumie maembe. Dunia ya wafupi tu ni taabu. Ya warefu tu ni balaa. Ya wababe tu, mnyonge ndiye kiongozi.

Maisha yakiwa magumu, wote tunageuka wana falsafa. Tunda letu limepotea, humu ndani hapakaliki. Aliyekula na aliyekosa, wote wanalia.

Tuwahi nyumbani, ofisini hapakaliki na mitaani mafuriko.


Mwisho wa kunukuu...
 
Ninafahamu kuhusu taarifa zinazosambaa juu ya tishio la maisha yangu, chama changu kimechukua hatua dhidi ya taarifa hizo. Maelezo zaidi yatatolewa katika wakati muafaka.
 
Itakuwa Ni tishio toka Kwa Wafurukutwa wa ACT waliokerwa na Kitendo chako cha kushindwa kuandaa report ya Fedha ya ACT Kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 na kuzipeleka Kwa CAG Kwa ukaguzi,

Serikal uwadhibiti wana ACT hao wakorofi
 
Back
Top Bottom