Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Nimeshangazwa na kushtushwa na kitendo Cha Jeshi la Polisi kumkamata Bunge wa Mbozi ndg. Pascal Haonga nje ya Geti la Bunge bila kuheshimu sheria za nchi yetu. Tabia Hii ilikuwa imeanza kukoma baada ya kukamatwa na Mbunge Godbless Lema wa Arusha Mjini na Tundu Lissu wa Singida Mashariki na kuleta malalamiko makubwa ya Wabunge kwa Spika Job Ndugai.
Baada ya kuwakwepa Polisi mjini Kahama Polisi walitaka kunivizia na kunikamata nje ya Geti la Bunge na tulipojua mtego wao tukamtaka Spika aeleze msimamo wa kisheria, kanuni na utamaduni wa Jumuiya ya Madola Kuhusu Mbunge kukamatwa. Spika Ndugai alitoa maamuzi kuwa kabla ya Mbunge kukamatwa ni lazima ajulishwe kwanza.
Nimeshangaa sana kuwa Polisi wamekiuka maagizo ya Spika na kudharau sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ambayo inazuia Mbunge kukamatwa wakati shughuli za Bunge zinaendelea. Utamaduni wa Jumuiya ya Madola unasema, nanukuu kwa Kiha
“As there is no privilege, of which the House of Commons have always been, and indeed, ought to be, more jealous, than the security of the persons of the Members, “that they shall be under no undue restraint from being able to attend their duty in Parliament””
Kazi ya Mbunge ni kuwa Bungeni na Wajibu wa Spika ni kuhakikisha hakuna kinachomzuia Mbunge kuwepo Bungeni. Spika Ndugai anapaswa kulieleza Bunge mapema kesho asbh, tarehe 7/5/2019 saa Tatu asbh KAMA ALIRUHUSU MBUNGE HAONGA KUKAMATWA NA POLISI NJE YA GETI LA BUNGE