ZITTO NDIO AMECHANGANYIKIWA ZAIDI KULIKO CCM

Joined
Oct 12, 2016
Posts
15
Reaction score
42
Siku ya tarehe 08/10/20016 kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo ndugu Zitto Zubeir Kabwe alinukuliwa akimshambulia Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania DR.John P. Magufuli kua ni mbinya demokrasia na hafuati utawala wa kisheria.
Hakuishia hapo akakishambulia pia na chama cha mapinduzi (CCM) kua kimechanganyikiwa na kwamba kimepoteza dira
.
Zitto huyu anapaswa aelimishwe kwamba Rais sio mbinyaji wa demokrasia na anafuata misingi yote ya utawala wa kisheria, na ingekua ni mbinyaji wa demokrasia sidhani hata kama mkutano wake wa jana angefanikiwa kuufanya.
Alichosema Rais ni kwamba kila mtu akafanye mkutano katika eneo alilochaguliwa ili kuepusha wananchi kutumia muda mwingi katika mikutano na maandamano ya kisiasa ambayo mingi imekua haina tija kwa wananchi.Wananchi inabidi wakafanye kazi ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na sio kushiriki katika maandamano na mikutano ambayo wazungumzaji wake wanakua wanawachochea wananchi kugomea shughuli za kimaendeleo zinazoletwa na serikali sambamba na kuwatukana viongozi wa serikali.

Tumeshudia wananchi wasio na hatia wakifariki,huku wengine wakibakia na ulemavu wa kudumu kutokana na mikutano hiyo iliyopigwa marufuku ambayo kimsingi ilikua imejaa viashiria vya uvunjifu wa amani.

Nitakua mtu wa mwisho kuamini kua Zitto Kabwe hafahamu hili maana kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa alipokua naibu katibu mkuu wa CHADEMA katika mkutano mmoja kule jijini Mwanza alishuhudia jinsi kijana mmoja alivyopoteza maisha kutokana na matamshi ya uchochezi yalitotolewa na mmoja wa wazungumzaji pale mkutanoni ambayo yaliamsha hasira na hatimaye ugomvi uliochukua uhai wa kijana yule.
Sitaki kuamini kwamba Zitto bado anatamani damu zisizo na hatia ziendelee kumwagika kwa maslahi ya wanasiasa matapeli.

Pia Zitto anadai Rais Magufuli anajenga himaya ya ufisadi kutokana na kutokuruhusu mikutano ya kisiasa.Ningependa kujibu hili kwa takwimu.Miaka 10 iliyopita mikutano ya kisiasa ilikua ni ruksa kufanyika lakini hali ya ufisadi na rushwa nchini ilikuaje? Kama ufisadi ulitamalaki kipindi hicho ambacho mlipewa midomo ya kusema na kuzunguka nchi nzima katika operesheni zenu , basi mikutano ile zile operesheni zenu zilikua ni "hewa".
Chini ya uongozi wa Rais Magufuli kumejengwa mahakama ya ufisadi hii inaonesha utayari wa serikali ya ya Mh Magufuli ya kukomesha ufisadi, rushwa, na uhujumu uchumi hapa nchini.

Zitto pia anadai serikali haijielewi katika suala la viwanda katika kuelekea katika mpango wa kuelekea nchi ya viwanda na kwamba inakimbilia kuzindua miradi ya viwanda vya sekta binafsi.
Hapa nachelea kusema kua Zitto anaumwa ugonjwa wa wivu.Yani anataka Rais Magufuli au waziri mkuu Majaliwa wakialikwa katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda kinachomilikiwa na watu wa sekta binafsi wagomee kwenda kukizindua kwa kua tu hakijajengwa na serikali,? hiki ni kichekesho kingine.
Inatambulika na waziri wa Viwanda na biashara Mh Charles Mwijage ameshashema kule bungeni kua serikali haitojenga viwanda bali itakachofanya ni kuweka mazingira bora na rafiki ya uwekezaji na biashara hhapa nchini ili kuwavutia wafanyabiashara wa ndani na nje kuwekeza kwenye sekta ya viwanda hapa nchini.Hivo ndivyo serikali inavyofanya sambamba na kuwanyanga`nya mabepari waliohodhi viwanda kwa muda mrefu bila ya kuviendeleza wala kuzalisha.

Zitto kabwe anapata wapi ujasiri wa kuhoji kuhusu ujenzi wa viwanda,kwanza atueleze zile hekta 350 alizohodhi katika eneo la KISEZ na kuhaidi kujenga kiwanda cha kuzalisha mafuta ya mawese, amezifanyia nini.??
Zitto Kabwe ameingiwa na mchecheto baada ya kusikia mifuko ya hifadhi ya jamii inajipanga kuanza kujenga viwanda vya aina mbali mbali mwakani .Anajua fika hadi kufikia mwaka 2020 viwanda vingi vitakua vimejengwa sambamba na kufufuliwa kwa viwanda vingi.vilivyokufa hapa nchini , kwake hatua hizo ni pigo kwa mustakabali wa siasa zake hususani ubunge wake ukizingatia ametoka kuzomewa kule jimboni kwake na ndio maana anatumia kila jukwaa kumshambulia na kumvuruga Rais Magufuli juu ya sera yake nzuri ya Tanzania mpya ya viwanda.

Zitto ndio anapaswa kuchanganyikiwa maana ameshindwa kulipia kodi za pango katika ofisi za ACT-WAZALENDO katika mikoa mbali mbali pamoja na kuhaidi lakini ameshindwa kutekeleza ahadi yake hiyo, hivyo kupelekea ofisi hizo kufungwa.

Zitto anapaswa kufahamu chama cha mapinduzi ni taasisi kubwa inayofanya kazi zake kiuweledi na kifanisi zaidi na ndio maana kimeendelea kuaminiwa na mamilion ya watanzania miaka nenda miaka rudi, kwa kukipa madiwani wengi zaidi, wabunge wengi na Rais, tofauti na chama chake ambacho bila yeye Zitto chama hakiwezi kujiendesha
 
Siku ya tarehe 08/10/20016 kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo ndugu Zitto Zubeir Kabwe alinukuliwa akimshambulia Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania DR.John P. Magufuli kua ni mbinya demokrasia na hafuati utawala wa kisheria.
Hakuishia hapo akakishambulia pia na chama cha mapinduzi (CCM) kua kimechanganyikiwa na kwamba kimepoteza dira
.
Zitto huyu anapaswa aelimishwe kwamba Rais sio mbinyaji wa demokrasia na anafuata misingi yote ya utawala wa kisheria, na ingekua ni mbinyaji wa demokrasia sidhani hata kama mkutano wake wa jana angefanikiwa kuufanya.
Alichosema Rais ni kwamba kila mtu akafanye mkutano katika eneo alilochaguliwa ili kuepusha wananchi kutumia muda mwingi katika mikutano na maandamano ya kisiasa ambayo mingi imekua haina tija kwa wananchi.Wananchi inabidi wakafanye kazi ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na sio kushiriki katika maandamano na mikutano ambayo wazungumzaji wake wanakua wanawachochea wananchi kugomea shughuli za kimaendeleo zinazoletwa na serikali sambamba na kuwatukana viongozi wa serikali.

Tumeshudia wananchi wasio na hatia wakifariki,huku wengine wakibakia na ulemavu wa kudumu kutokana na mikutano hiyo iliyopigwa marufuku ambayo kimsingi ilikua imejaa viashiria vya uvunjifu wa amani.

Nitakua mtu wa mwisho kuamini kua Zitto Kabwe hafahamu hili maana kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa alipokua naibu katibu mkuu wa CHADEMA katika mkutano mmoja kule jijini Mwanza alishuhudia jinsi kijana mmoja alivyopoteza maisha kutokana na matamshi ya uchochezi yalitotolewa na mmoja wa wazungumzaji pale mkutanoni ambayo yaliamsha hasira na hatimaye ugomvi uliochukua uhai wa kijana yule.
Sitaki kuamini kwamba Zitto bado anatamani damu zisizo na hatia ziendelee kumwagika kwa maslahi ya wanasiasa matapeli.

Pia Zitto anadai Rais Magufuli anajenga himaya ya ufisadi kutokana na kutokuruhusu mikutano ya kisiasa.Ningependa kujibu hili kwa takwimu.Miaka 10 iliyopita mikutano ya kisiasa ilikua ni ruksa kufanyika lakini hali ya ufisadi na rushwa nchini ilikuaje? Kama ufisadi ulitamalaki kipindi hicho ambacho mlipewa midomo ya kusema na kuzunguka nchi nzima katika operesheni zenu , basi mikutano ile zile operesheni zenu zilikua ni "hewa".
Chini ya uongozi wa Rais Magufuli kumejengwa mahakama ya ufisadi hii inaonesha utayari wa serikali ya ya Mh Magufuli ya kukomesha ufisadi, rushwa, na uhujumu uchumi hapa nchini.

Zitto pia anadai serikali haijielewi katika suala la viwanda katika kuelekea katika mpango wa kuelekea nchi ya viwanda na kwamba inakimbilia kuzindua miradi ya viwanda vya sekta binafsi.
Hapa nachelea kusema kua Zitto anaumwa ugonjwa wa wivu.Yani anataka Rais Magufuli au waziri mkuu Majaliwa wakialikwa katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda kinachomilikiwa na watu wa sekta binafsi wagomee kwenda kukizindua kwa kua tu hakijajengwa na serikali,? hiki ni kichekesho kingine.
Inatambulika na waziri wa Viwanda na biashara Mh Charles Mwijage ameshashema kule bungeni kua serikali haitojenga viwanda bali itakachofanya ni kuweka mazingira bora na rafiki ya uwekezaji na biashara hapa nchini ili kuwavutia wafanyabiashara wa ndani na nje kuwekeza kwenye sekta ya viwanda hapa nchini.Hivo ndivyo serikali inavyofanya sambamba na kuwanyanga`nya mabepari waliohodhi viwanda kwa muda mrefu bila ya kuviendeleza wala kuzalisha.

Zitto kabwe anapata wapi ujasiri wa kuhoji kuhusu ujenzi wa viwanda,kwanza atueleze zile hekta 350 alizohodhi katika eneo la KISEZ na kuhaidi kujenga kiwanda cha kuzalisha mafuta ya mawese, amezifanyia nini.??
Zitto Kabwe ameingiwa na mchecheto baada ya kusikia mifuko ya hifadhi ya jamii inajipanga kuanza kujenga viwanda vya aina mbali mbali mwakani .Anajua fika hadi kufikia mwaka 2020 viwanda vingi vitakua vimejengwa sambamba na kufufuliwa kwa viwanda vingi.vilivyokufa hapa nchini , kwake hatua hizo ni pigo kwa mustakabali wa siasa zake hususani ubunge wake ukizingatia ametoka kuzomewa kule jimboni kwake na ndio maana anatumia kila jukwaa kumshambulia na kumvuruga Rais Magufuli juu ya sera yake nzuri ya Tanzania mpya ya viwanda.

Zitto ndio anapaswa kuchanganyikiwa maana ameshindwa kulipia kodi za pango katika ofisi za ACT-WAZALENDO katika mikoa mbali mbali pamoja na kuhaidi lakini ameshindwa kutekeleza ahadi yake hiyo, hivyo kupelekea ofisi hizo kufungwa.

Zitto anapaswa kufahamu chama cha mapinduzi ni taasisi kubwa inayofanya kazi zake kiuweledi na kifanisi zaidi na ndio maana kimeendelea kuaminiwa na mamilion ya watanzania miaka nenda miaka rudi, kwa kukipa madiwani wengi zaidi, wabunge wengi na Rais, tofauti na chama chake ambacho bila yeye Zitto chama hakiwezi kujiendesha.

AUGUSTINO CHIWINGA
KADA MFIA CHA CHAMA CHA MAPINDUZI.(CCM)
Laana ya usaliti.
 
Mleta mada unajisumbua , chama kikuu cha upinzani ndani ya mioyo ya watanzania ni Act wazalendo .

Na wala siyo ile Sacco's ya wabadili gia za angani.
 
Mkuu Mzalendo wa Tanzania, kajifunze kitu kinachoitwa "managing divesty" halafu nenda kwenye "political diversity" na "political tolerance ", then yaheshimu mawazo ya Zitto Zuberi Kabwe! .
Pasco
 
Ukiheshimu mawazo ya Zitto utakuwa una prove utafiti "KILA WATANZANIA WANNE MMOJA NI KICHAA"
Masikitiko yangu ni kuwa wewe utakuwa ndio huyo mmoja aliyeainishwa na utafiti.

Mkuu Jogi you are right, mimi ni mmoja wa wanne hao.
Pasco
 
Kumshambulia zitto,ni kupoteza muda lipumba mmemshidwa sasa munakuja na ID za kubumba eti "mzalendo tz" huna uzalendo wowote "adui ya muha ni muha mwenzake"
 
Asante msemaji pia mtetezi wa JPM. nadhani umepewa buku saba na hakuna uliloongea zaidi ya kujikomba konba tu....

unahiita ccm taasisi kubwa ilojaa uoga. lini taasisi kubwa ikawa na uoga ikiwa ninpamoja na unasahau inasurvive kwa wizi wa kura pia kwa ubabe pia kuogopa kutupa tume huru ya uchaguzi.
ata kuzuia mikutano ni uoga uloijaa ii taasisi

nadhan siasa kufanyika ni kwa mujibu wa katiba ya nchi na si mapenz ya mtu. nadhan mabadiliko kt katiba yangefanyika ili ku..suit matakwa ya lumumba o.w ukuta unapaswa kuwa practiced..

pia umecomplicate maelezo yako.. unasema anadaiwa kodi kt ofisi za act mikoani halafu pale pale unasema zzk akafanyie siasa zake kigoma tu anaporuhusiwa.... kwa mantiki iyo je izo ofisi ni za kaz gani??? IQ yako ndogo

watu wanafariki pale polisi ikijiingiza kt mikutano ya opposition na si matakwa ya opposition leaders.

ata kuzuia watanzania tsijue kinachoendekea bungeni ni sawa kabisa na kutufanya tusijue kinachiendelea bungen ili mafisad waendelee kustawi
 
Back
Top Bottom