Well said mkuu, kula likes zangu. Hili ndilo tatizo letu kuu, tumeacha hoja kuu ya TPDC kugomea mikataba ya rasilimali za nchi tumeng'ang'ana na Zitto as if hiyo kamati ni yeye peke yake!
Nchi ina hali mbaya sana shauri ya mambo haya haya badala ya kuendesha mijadala humu mitandaoni na kwingineko kuiunga kamati mkono na kuibana serikali mikataba itolewe ili tujue wanaotuhujumi tuko bize kulumbana wenyewe kwa wenyewe.
Kama akina Chenge walipewe mabilioni kwenye dili la rada ni nini kitazuia hawa watendaji wa TPDC na wizara wasihongwe ili kuingia mikataba isiyo na maslahi na nchi yetu?? Jiulize kwa nini wanaifanya siri hata kwa kamati za bunge?? 2 yrs now hawataki kabisa kuitoa why??
/
Ni Kweli waliteleza ...walitakiwa kupata Kibali cha spika ...kabla ya kuwatia ndani wale Jamaa ...,Sioni kwanini hawakuomba kile kibali ..week Moja kabla ..unless walikuwa na mashaka kuwa spika angepitisha wakamatwe ..
Wamefanya kazi nzuri though Jamaa wanaweza KUDAI fidia...UJUMBE umefika .....though Kisiasa wanaweza Kuiweka Kama vile wajumbe walitaka kupata faida ya kisiasa
kwanza inaonyesha kila dalili kuwa wale jamaa waliandaliwa kiaina kabisa kwamba watapelekwa polisi then wataachiwa, inaonyesha huo mpango uliandaliwa mahsusi tangu awali ili kuanza kuliinua jina la msaliti juu, bahati mbaya halijainuka,
Pinda aliyatoa hayo baada ya sheria kuvunjwa, kwa utetezi wake akazidi kuvunja sheria. Kina sita wamevunja sheria kuhalalisha maslahi ya kikundi chao tena ya watu wachache, viongozi wamekuwa wakivunja sheria kwa namna nyingi na tofauti tofauti kwa maslahi yao au ya familia au mitandao yao sio kwa manufaa ya nchi. Kote huko hakuna hatua yoyote tangible mloichukua. Kibaya zaidi wataendelea kuvunja sheria hizi tena kwa maslahi yao na hamtawafanya chochote. Leo hii zitto anapindisha taratibu kwa kutetea maslahi katika rasilimali zenu, mnamuona scrapegoat?
Huwezi kusimamia sheria moja kwa kuvunja sheria nyingine, harafu unatumia lugha rahisi "zito kapindisha sheria" hii haikubaliki katika demokrasia za kweli, hapa naona unaungana na kina makamba kuutaka udikteta ila kwa kuwa makamba upo CCM huwezi kusema moja kwa moja kuwa unamuunga mkono. Zitto na kamati yake wamevunja sheria, waombe radhi kwa kuvunja sheria za nchi. Hatutegemei kamati ya Bunge kuvunja sheria, ni aibu kwamba wanatunga sheria halafu wenyewe hawazielewi.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zikiwemo Kamati zake mbalimbali za Kudumu, linaongozwa na Katiba, Sheria na Kanuni za Kudumu za Bunge hilo. Kila jambo Bungeni husimamiwa na sheria tajwa. Hivi karibuni, kumetokea sintofahamu kati ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Mashirika na Taasisi za Umma (PAC) na viongozi wa TPDC.
Iliripotiwa kuwa viongzi husika waliagizwa na Kamati ya Zitto kuwasilisha nyaraka mbalimbali mbele ya Kamati hiyo. Ikaripotwa tena kuwa kufuatia kukaidi kwa viongozi hao kuwasilisha nyaraka,walikamatwa na polisi na baadaye kuachiwa baada ya kuhojiwa.
Bunge linapewa nguvu kupitia Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge ya 1988 iliyofanyiwa Marekebisho mwaka 2004 kupitia Sheria Nambari 3 ya 2004. Binafsi nimevutiwa na kifungu cha 17(2) cha Sheria tajwa ya 1988 ambacho hakikuguswa na marekebisho ya 2004. Sakata la viongozi wa TPDC linahusiana nacho.Kifungu kinasomeka hivi:
17 (2) Where any person ordered to attend or to give evidence or produce any document before any committee refuses to answer any question that
may be put to him or to produce any such document on the ground that. the same is of aprivate nature and does not affect the subject of inquiry,
the chairman of the committee may report such refusal to the Speaker with the reasons therefor; and the Speaker may thereupon excuse the
answering of such question or the production thereof.
Ni wazi, kama ilivyoripotiwa kuwa viongozi wa TPDC waliagizwa na Kamati ya Zitto kuwasilisha nyaraka.Pili, kwa maneno au matendo hawakuwasilish na hivyo kuonekana wamekataa. Mwenyekiti wa PAC angeweza kuripoti kwa Spika wa Bunge akiainisha sababu za kuripoti kwake na mwisho mwishoni Spika angeweza kusamehe kutolewa kwa nyaraka hizo.Yaani, Spika angeweza kulazimsha au kusamehe uwasilishwaji wa nyaraka husika.Hapo nimetafsiri kifungu cha hapo juu pamoja na kilichoripotiwa.
Hivyobasi, PAC haina na haikuwa na mamlaka ya kuwakamata au kusababisha kukamatwa kwa viongozi wa TPDC. Kama ilifanyika kinyume na utaratibu uliowekwa na Sheria, PAC iliteleza.
Je kuna watu wanaruhusiwa kusimamia sheria kwa kuvunja sheria ila wengine ndo hawaruhusiwi? Huyo uliyequote, pinda, alivunja sheria pia akidhani anasimamia sheria. By the way, kama kweli una mtazamo wa sheria itawale kila sehemu unawezaje kusema waliovunja sheria waombe radhi? Au ndo unaendeleza kile kizazi cha EPA kilichoomba msamaha? Kama ni utawala wa sheria ufatwe na watu wote kwa kila jambo, sio wengine waonekane wanaruhusiwa na wengine sio.
Kumbuka kuwa sio Zitto au kamati ya PAC waliochukua hatua hizo wao pia walishirikisha wanasharia wa bunge na hata walipokamatwa na kuwekwa ndani mwanasharia wa bunge alifafanua kwa kina kuwa walikuwa na mamlaka hayo.
Hebu pitia maelezo ya mwanasharia wa bunge aliyotoa kabla kutolewa amri ya kukamatwa kwa viongozi hao.
Lakin kwa upande mwingine kama viongozi hao wataona hawakutendewa haki na kamati hiyo ya PAC wana HAKI YA KWENDA MAHAKAMANI KUDAI HAKI YAO.
Tuvute subra tuona kama watakwenda mahakamani kudai haki yao ya kudhalilishwa na PAC
Kwangu mimi wote hao wanamakosa, Pinda, Zito na genge lake, makamba na wengine. Tofauti yangu na wewe ni kuwa wewe unaona Zitto yupo sahihi ila kina pinda na ndo wamekosea. Hapa ndo shida yetu. Pinda, Zitto na genge lake hawawezi kusimami sheria kwa kuvunja sheria, tu ahatupaswi kumsifia Zito na genge lake kwa uovu huu. Kama tulivolaani kwa Pinda ndo tunapaswa kulaani kwa Zitto. I am using my head, and I can see your using your "heart" its ok to use your heart to look for a wife, not in choosing political leaders.
Katika hili naipongeza kamati ya PAC chini ya mwenyekiti wake Ndg Zitto na Ndg Filikunjombe. Wameonesha ni kwa jinsi gani wanachukizwa na uzembe, ujinga na ubinafsi wa watu wachache ambao kwa ubinafsi wao wameisababibishia nchi umaskini huku wao wakineemeka kwa mikataba bibovu. Nasema hivi kwa sababu kuna ulazima gani wa mikataba kama hiyo kufichwa. Nilitegemea mikataba ya rasilimali za taifa iwe public document ili kila mmoja ajue nani analipa nini kwa muda gani. Lakini pia nilijifinza kitu kimoja kwenye maojianao ya Zitto na Mkurugenzi wa TPDC. Kwamba mkurugenzi wa TPDC ama bado hajaelimika au ni ulimbukeni. Eti hawezi kutoa mikataba mpaka apate ruhusa ya wazungu wawekezaji. Hivi hata kama kipengele hicho kimo, ili hitaji kuwa amemaliza darasa la saba ili kuweza kugundua na kukikataa kifungu hicho kabla ya kusign!!! Huu si mwendelezo wa utumwa na mikataba ya Chief Magungo wa Msovero. Yeye anatofauti gani na huyo Chief??? Nachukizwa na watu amabao bado wanawanyenyekea wazungu wakidhani bila wao mambo hayaendi. Rasilimali ni zetu hivyo mdundo wowote unaochezwa lazima uwe ule tunaouchagua sisi. Kamati ya PAC imeonesha mwanzo wa huko tunakoelekea. Kwamba huko tunakoelekea watu watataka kuona kila kitu kweupe. Haya mambo ya kuficha ficha mnaficha nini. Na siku tukigundua kuwa kuna watu wachache walijinufaisha kwa mikataba ya kijinga si wao wala watoto wala wajukuu na vitukuu watakuwa salama. Wako salama kwa muda tu. Tumechoka na hivyo tumeanza kusaka watu wanaotuibia na kuwawekea dot. Kazi ikianza ya kuwashughulikia, si muda neema itakuwa kwa wananchi.
Kwani tunaingia hasara gani KWA SABABU TU Mikataba imefichwa?
Safi sana.
Lakini HEAD ndio HEART. Kwa basis ya maelezo yako.
Sangara natumaini akili zako nyingi kuliko samaki sangara (no offence Mtanzania is meant), hapa namaanisha ni imani kuwa unaweza pia kumudu maisha ya nchi kavu (to decode hidden meangs of the words) sio kama samaki sangara anayemudu maisha ya kwenye maji tu (to undersant only the diretct meaning of the words).
Using your "head or sometimes referred to as brain" would mean being rational as informed by facts, which is contrally to using your "heart" where feelings driven by love lead your action or deeds.
Unaweza pia kusikiliza wimbo wa Lady JD - usiusemee moyo au Lauren Hill - zion. utapata vitu humo juu ya tofauti kati ya kutumia "moyo" na kutumia "akili".
Kama mwananchi wa kawaida ninatakiwa kujua nchi yangu ananufaika vipi na mikataba inayoingia na wawekezaji. N apengine kwa kujijua tungeweza kuiboresha ili kuleta tija zaidi. Lakini kama mikataba inafichwafichwa namna hii basi ni dhahiri tunaendeleza hasara ambazo tumezipata kwenye mikataba ya madini. Nadhani tunaowataalam wengi nami nikiwepo, kama mikataba ya kitaifa ingekuwa ni public document basi kila mmoja angekuwa anajua ni kiasi gani tunapata. Nakama tunakosa / tunapata hasara kwasababu ya vipingele vya mikataba basi vingerekebishwa kwa mikataba mingine. Kuna nini nyuma ya kuficha mikataba kama si uovu uliopitishwa ama kwa makusudi baada ya kupata mlungula ili mambo yaende na hivyo kutusababishia hasara ya mapato kama nchi. Kama kila kitu kiko sawa kuna uoga gani wa kuiweka wazi. "Eti mpaka tupate ridhaa ya wawekezaji" Hiyo kweli ni akili, kama ulionakipengele hicho ulishindwa nini kukiondoa au kukikataaa kabla ya kusign huo mkataba. Ilitakiwa wajiulize kuna nini cha kufichaficha. Kwanini??? Kuna mambo mengi ya kujiuliza, hata mengine ni aibu kutamkwa na hao tunaowahita wasomi na wanasheria. Eti nao waliridhia!!! Pengine serikali imepunjwa mapato, baada ya hao wawakilishi kupewa mlingula na kuandaa mkatana wa hovyo. Au wameweka loop holes za kwemwezesha mwekezaji kukweka mapato baada ya kukatiwa chao na wao kukubaliana na vipengele vya kijinga. Ni ujinga kukumbatia mtu mpumbavu hata yeye atakuona ni mpumbavu hata kama hakwambiii.