Zitto na movement for change (m4c-chadema)

Zitto ni ugonjwa kwa walio wengi wasio ijua Chadema vizuri, bila Chadema no Zitto na bila Zitto hakuna Chadema imara (atleast kwa sasa).

Kitu kimoja cha kukinote hapa ni kwamba Chadema ndio chama tegemewa kuchukua madaraka 2015 au 2020, kwa hiyo lazima kutaibuka migongano ya kimaslahi kwa sababu sio mtu mmoja tu anayehitaji madaraka kwenye chama hicho, ni kila mmoja.

Kwa sasa wagombea urais kupitia CDM ni Dr Slaa, Shibuda, Mh Mbowe na Mh Zitto (kama kuna wengine tutajua soon), hivyo migongano ya kisiasa lazima itokee na hii inaambatana na wafuasi wa upande mmoja kumshambulia kiongozi wa upande mwingine.

Hizo ni changamoto ambazo chama cha siasa lazima kikumbane nazo, so swala la Zitto hatumwoni hapa au pale na kuanza kutangaza kwamba sio mshiriki mzuri bila kujiuliza kapewa majukumu mengine yapi ni la kishabiki zaidi.

M4C
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nimekuwa nikifuatilia operation ya vua gamba vaa gwanda katika sehemu mbalimbali. Mhe. Zitto Zuberi Kabwe haonekani kwenye mikutano ya hadhara. Kama unajua sababu ambazo zinamfanya mheshimiwa huyu kutoshiriki tupia hapa.
Peoples
Power
Hakuna kulala
mpaka kieleweke

Yupo bize kwenye kamati ya bunge ya mashirika ya umma.

Ndio yeye alishindikiza mpaka JK akawatoa wakina Mkulo.

Mwacheni Zitto aendelee kupiga kazi
 
kwani hata tundu lisu ameonekana ? tuache unafki wengine wapo kwenye majukumu mengine

Hawa watu wote wanashiriki sema kwa kiwango gani ndiyo inatofautiana na hii inachangiwa na mgawanyo wakazi pamoja na majukumu mfano Lema kwasasa ndiyo anaeonekana kuitendea haki M4C na sababu kubwa ni kwamba Lema hana majukumu ya kibunge na kamati baada ya ubunge kutenguliwa..lakini haiimanishi kwamba hawashiriki mfano Lisu alifanya mkutano mkubwa pale Babati na kuvua watu magamba vya kutosha tulijuzwa hapa JF....Zitto wakati inazinduliwa yeye alikuwa anamajukumu miko mingine kama Mwanza na Songea.....
M4C siyo ya viongozi tu hata sisi watanzania kwa ujumla tushiriki kubadilisha watu fikra ndiyo tutafanikiwa kumuondoa mdudu CCM lakini tukiwategemea viongozi tu kazi bado ngumu sana...
 
Jamani tofautisheni kati ya CDM na CCM!! CDM wao wanagawana majukumu kulingana na mashambulizi ya kivita yanavohitaji, hawaendi kama kweleakwelea as CCM!!

CDM 2015 wanachukua dola hivo ni lazima kujipanga kila nyanja! Sio kundi zima wakimbilie M4C, mtu makini utawashangaa! Tazama Halima, Lissu, Kabwe, Mnyika, Nasari(mara moja), hawa wanashambulia upande mmoja.

Lema, Msigwa, Dr. Slaa, Sugu, Wenje, hawa ni upande wa pili wa mashambulizi, yaani kwa ufupi CDM nzima ina majukumu hakuna alielala labda Shibuda a.k.a vuvuzera!!
 
Ukanda na Ukabila CHADEMA unamvunja nguvu.Chama kimekua cha watu wachache ambayo ni hatari kwa ustawi wa chama,mwenye mawazo mbadala anaonekana 'mamluki'.
Chama kinatakiwa kivae taswira ya jina lake, Chama cha demokrasia, hayo maendeleo ni longterm.
Hayuko happy pale chadema (kama alivyo Sitta pale CCM) ila ni mtu makini sana hawezi kukurupuka ila akipata mbadala anaweza kuhama
 
4MC- movement for Chagaz, kwa bahati mbaya yeye siyo mchaga!!

Toka mwenyekiti wako hamwezi kula hadi mliwe kidogo lakini hana maana hiyo,maana ya huo msemo ni ipi? jk kala kona labda weye tujuze ulo karibu nae. Hakuna cha kusomba watu na malori kesho kama nyie gambaz.
 
CHADEMA.jpg

so-called m4c ni mpaka kwenye tanzanian diaspora
 
Dah! Hata mm nilikuwa na swali kama hilo lako mkuu nikijiuliza, acha tusibiro wanojua waje watupe majibu.

ficha uso!..... kwa aibu!

Nadhani unapata picha watu wanavyomchukulia Zitto sasa, mmezoea kupandikiza chuki mkijiita wanachadema......sasa watu wameishagundua na nyie mliobaki taratiibu mnazidi kuez exposed....ficha uso mkuu!
 
4MC- movement for Chagaz, kwa bahati mbaya yeye siyo mchaga!!

you are wrong kk,!! you'll remained tied with you awkward thoughts while the intelligent are moving forward. which ever your trib is, point out your contribution in liberating tanzanian from the hungry vultures -CCM. think wisely and cretically befor you vomit non senses. If it's chaggas, what is your position as a Tanzanian in liberating the country! Zito's two facedness is what make people believe something round. He never effectively joined the battle vs our enemies. if he is with us, he should join us effectively and show his strength as a young man in front line rather than the way he is now.
 
Dah! Hata mm nilikuwa na swali kama hilo lako mkuu nikijiuliza, acha tusibiro wanojua waje watupe majibu.

Mkuu Mh Zito yuko nchini Uholanzi kwenye ziara ya kibubge na akina Kafulila, wanajifunza juu ya namna Uholanzi ilivyoweza kunufaiuka na utajiri wa gesi, ili itumike katika kuboresha sheria yetu ta gesi na mafuta. Ubalozi wa uholanzi umefadhili safari yao hii, hata hivyo si unajua ni mwenyekiti wa POAC, na vikao vyao vya maandalizi ya bajeti. TUPO pamoja sana wakuu wangu msihofu
 
Nimekuwa nikifuatilia operation ya vua gamba vaa gwanda katika sehemu mbalimbali. Mhe. Zitto Zuberi Kabwe haonekani kwenye mikutano ya hadhara. Kama unajua sababu ambazo zinamfanya mheshimiwa huyu kutoshiriki tupia hapa.
Peoples
Power
Hakuna kulala
mpaka kieleweke

its not all about zitto ila ni namna ya kugawana majukumu ndani ya chama
 
kwani hata tundu lisu ameonekana ? tuache unafki wengine wapo kwenye majukumu mengine

big up mkuu...watu humu wamejaa ushabiki wa kijinga wa kufikiri kushiriki maana yake ni watu wote wawe sehemu moja..vita gani inapiganwa hivyo????!!!!

jifunzeni wakati wazungu wanataka kumtoa Saddam, wamarekani na washirika walipiga kutokea magharibi wakiilenga Baghdad wakati Waingereza na washirika kutokea kusini wakiilenga Basra n.k. muhimu ni kuwa kila mshirika alijua lengo la vita nini na nafasi yake ni ipi basi.
 
Swali lako halina utafiti, na kumbukamkutani ni Wehrmacht ya majukumu ya Ghana, mengine yapping na ni mengi makubwa mno, Mr. Kuitwtea nchi, kupinga unyonyaji na sisi from ccm, kushughulikia wananchi wa Jimbo husika na majukumu mengine ya Bunge.
 
Acheni Majungu na kupandikiza chuki kuhusu Zitto kuna mbunge gani ndani ya Bunge aliye jembe kama zitto??!!!
 
Back
Top Bottom