Zitto, Mnyika wafichua upotoshaji bajeti ya Mkulo; Spika Makinda akiri, amtaka Mkulo arekebishe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto, Mnyika wafichua upotoshaji bajeti ya Mkulo; Spika Makinda akiri, amtaka Mkulo arekebishe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rmashauri, Jun 8, 2011.

 1. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wakuu, pendekezo la Zitto Kabwe la kutumia asilimia 4 ya "Skills Development Levy " iliyokuwa inaingia serikali kuu kusomesha vijana wetu limetekelezwa kwenye bajeti ya mwaka 2011/2012.

  Nanukuu

  "79. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82 kama ifuatavyo:

  Kufanya marekebisho katika mgawanyo wa mapato yatokanayo na tozo ya kuendeleza ufundi stadi (Skills Development Levy) ya asilimia 6 ili asilimia 4 zipelekwe kwenye Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, na asilimia 2 zipelekwe Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Vocational Education and Training Authority - "VETA"). Lengo la hatua hii ni kuongeza fedha za mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu.
  Hatua hii katika Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi haitarajiwi kupunguza wala kuongeza mapato ya Serikali."

  ========================

  Zitto naye katoa Tamko:

  [FONT=&amp]JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA[/FONT]
  [FONT=&amp]BUNGE LA TANZANIA

  [/FONT]
  Simu Na. 026 2322761-5
  Fax Na. (255) 026 2324218
  E-Mail: poctz@parliment.go.tz

  (Barua zote za kiofisi ziandikwe kwa (Kiongozi wa Upinzani)
  Unapojibu tafadhali taja:

  OFISI YA BUNGE
  S.L.P. 941
  DODOMA
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  9 Juni, 2011
  "Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/2012 ina upotoshaji mkubwa"

  Kutokana na Hotuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha, Mhe. Mustafa Mkullo (Mb), aliyoitoa jana bungeni Dodoma tarehe 08/06/2011, kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012. Kambi ya Upinzani tumeshtushwa na upotoshaji mkubwa wa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa na serikali kwa lengo la kuwajengea matumaini hewa wananchi kuwa watapata nafuu ya maisha kupitia bajeti hiyo wakati hali halisi haipo hivyo.

  Yafuatayo ni baadhi tu ya maeneo ya waziwazi ambayo serikali ya CCM kupitia kwa Waziri wake Mhe. Mkulo iliamua kuupotosha umma wa Watanzania kwa makusudi kama ifuatavyo;

  1. Wakati Waziri akitaja kuwa kipaumbele cha kwanza cha bajeti hiyo ni kumaliza tatizo la Umeme na hivyo kutamka kwamba ametenga shilingi 537 Bilioni, , upembuzi uliofanywa na Kambi yetu ya Upinzani kwenye vitabu vya bajeti (Kitabu Namba II na IV) vilivyotolewa na serikali yenyewe, umebaini kuwa Wizara ya Nishati na Madini imetengewa jumla ya kiasi cha shilingi 402,402,071,000 kwa mujibu wa fungu la 58. Fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya Matumizi kawaida shilingi 76,953,934,000 na kwa upande wa bajeti ya Maendeleo zimetengwa shilingi 325,448,137,000. Shilingi Bilioni 325 zilizotengwa katika Bajeti ya Maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa 160MW, 100 Dar es Salaam na 60 Mwanza. Hakuna mradi wowote mpya wa umeme unaonekana katika Bajeti. Ni dhahiri kuwa kauli ya Mkulo ililenga zaidi kuwajengea wananchi matumaini hewa kuliko kuchukua hatua za kweli za kumaliza tatizo la umeme.

  2.
  Wakati Waziri na Serikali wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa bajeti ya mwaka huu imeongezeka kuliko ilivyokuwa mwaka 2010/2011, ukweli ni kuwa hakuna ongezeko halisia (real term increase) lililofanyika. Bajeti iliyopita ilikuwa kiasi cha shilingi 11.6 trilioni wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya shilingi 13.525 trilioni. Kati ya ya fedha hizo za mwaka 2011/2012, kiasi cha shilingi 1.901 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 14.06% ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la Taifa. Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha shilingi trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 (Japo thamani ya shilingi imeanguka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010/2011). Tunasisitiza kuwa hii si bajeti ya maendeleo, hii ni bajeti ya madeni.

  3.
  Wakati Waziri akisema Bungeni kuwa Bajeti ya mwaka 2011/2012 itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kuthibiti matumizi, nanukuu "kupunguza malipo ya posho mbalimbali yasiyokuwa na tija (uk.53)", ukweli ni kuwa Bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 imetenga jumla ya shilingi 0.987 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 13 % ya bajeti yote ya serikali kwa ajili ya kulipa posho chini ya vifungu vinavyojulikana kama "Personnel allowances (non discretionary na In-kind"). Kwa hiyo, kauli ya Waziri Mkulo kuwa serikali itapunguza posho sio kweli. Tunautaka umma wa Watanzania usikubali kurubuniwa.

  4. Wakati Waziri akisema kuwa ili kuthibiti matumizi watapunguza posho mbalimbali, kwenye hotuba yake uk.66, waziri amependekeza kufanywa kwa marekebisho ya sheria ya kodi ya mapato SURA 332 na anasema kwenye (i) "kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa serikali na wanaofanya kazi kwenye taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya serikali" . Hii inaonyesha dhahiri kuwa kauli ya Kufuta au kupunguza posho ilitolewa na Serikali ili kupumbaza wananchi lakini haina udhati.

  5.
  Bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 imewaongezea mzigo mkubwa sana wananchi na haswa wajasiriamali wadogo na vijana ambao wamejiajiri ama kuajiriwa kwenye biashara ya usafiri na usafirishaji. Tunasema hivyo, kwa sababu serikali katika bajeti vyake rasmi vya bajeti imeamua kufanya marekebisho ya sheria ya usalama barabarani sura 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati mtu akiwa anaendesha gari yaani (Traffic Notification Fee), kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 300,000. Lakini Waziri Mkulo katika Hotuba yake aliyoitoa jana ukurasa 74, alitamka kuwa wataongeza kiwango cha faini hadi kufikia shilingi 50,000. Ni dhahiri kuwa kauli ya waziri ya kusema faini itafikia 50,000 wakati kwenye vitabu rasmi vya bajeti faini hiyo inaonekana itafikia 300,000, hivyo alilenga kuuhadaa umma na kuupotosha.

  6.
  Kambi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya Serikali kutenga zaidi ya robo ya Bajeti kulipa Madeni na Kulipana Posho (Asilimia 27 – 14% kulipa madeni na 13% kulipa Posho mbalimbali).

  7. Kambi ya Upinzani itawasilisha Bungeni Bajeti Mbadala siku ya Jumatano tarehe 15.6.2011, saa tano asubuhi ambayo itakuwa inajali masilahi ya Watanzania yenye lengo la kukuza Uchumi wa Vijijini (rural growth) na itajikita katika kupata vyanzo vipya vya mapato na kubana matumizi ikiwemo kufuta Posho mbalimbali.

  Imetolewa leo, Mjini Dodoma, na  Zitto Zuberi Kabwe

  Waziri Kivuli wa Fedha
  [FONT=&amp]Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni[/FONT]
   
 2. mbasajohn

  mbasajohn JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni vizuri kama ametekeleza maana sasa faida ya upinzani inaanza kuonekana bungeni
   
 3. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Lakini isitekelezwe kinadharia bali kivitendo
   
 4. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Natumai watatekeleza kwa vitendo. Na hizo ni pesa nyingi sana na kwa maana hiyo tunatarajia kuona idadi ya wanaopata mikopo inaongezeka ili vijana wetu wapate kusoma kwa wingi.
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA[/FONT]
  [FONT=&quot]BUNGE LA TANZANIA

  [/FONT]
  Simu Na. 026 2322761-5
  Fax Na. (255) 026 2324218
  E-Mail: poctz@parliment.go.tz

  (Barua zote za kiofisi ziandikwe kwa (Kiongozi wa Upinzani)
  Unapojibu tafadhali taja:

  OFISI YA BUNGE
  S.L.P. 941
  DODOMA
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  9 Juni, 2011
  "Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/2012 ina upotoshaji mkubwa"

  Kutokana na Hotuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha, Mhe. Mustafa Mkullo (Mb), aliyoitoa jana bungeni Dodoma tarehe 08/06/2011, kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012. Kambi ya Upinzani tumeshtushwa na upotoshaji mkubwa wa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa na serikali kwa lengo la kuwajengea matumaini hewa wananchi kuwa watapata nafuu ya maisha kupitia bajeti hiyo wakati hali halisi haipo hivyo.

  Yafuatayo ni baadhi tu ya maeneo ya waziwazi ambayo serikali ya CCM kupitia kwa Waziri wake Mhe. Mkulo iliamua kuupotosha umma wa Watanzania kwa makusudi kama ifuatavyo;

  1. Wakati Waziri akitaja kuwa kipaumbele cha kwanza cha bajeti hiyo ni kumaliza tatizo la Umeme na hivyo kutamka kwamba ametenga shilingi 537 Bilioni, , upembuzi uliofanywa na Kambi yetu ya Upinzani kwenye vitabu vya bajeti (Kitabu Namba II na IV) vilivyotolewa na serikali yenyewe, umebaini kuwa Wizara ya Nishati na Madini imetengewa jumla ya kiasi cha shilingi 402,402,071,000 kwa mujibu wa fungu la 58. Fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya Matumizi kawaida shilingi 76,953,934,000 na kwa upande wa bajeti ya Maendeleo zimetengwa shilingi 325,448,137,000. Shilingi Bilioni 325 zilizotengwa katika Bajeti ya Maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa 160MW, 100 Dar es Salaam na 60 Mwanza. Hakuna mradi wowote mpya wa umeme unaonekana katika Bajeti. Ni dhahiri kuwa kauli ya Mkulo ililenga zaidi kuwajengea wananchi matumaini hewa kuliko kuchukua hatua za kweli za kumaliza tatizo la umeme.

  2.
  Wakati Waziri na Serikali wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa bajeti ya mwaka huu imeongezeka kuliko ilivyokuwa mwaka 2010/2011, ukweli ni kuwa hakuna ongezeko halisia (real term increase) lililofanyika. Bajeti iliyopita ilikuwa kiasi cha shilingi 11.6 trilioni wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya shilingi 13.525 trilioni. Kati ya ya fedha hizo za mwaka 2011/2012, kiasi cha shilingi 1.901 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 14.06% ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la Taifa. Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha shilingi trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 (Japo thamani ya shilingi imeanguka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010/2011). Tunasisitiza kuwa hii si bajeti ya maendeleo, hii ni bajeti ya madeni.

  3.
  Wakati Waziri akisema Bungeni kuwa Bajeti ya mwaka 2011/2012 itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kuthibiti matumizi, nanukuu "kupunguza malipo ya posho mbalimbali yasiyokuwa na tija (uk.53)", ukweli ni kuwa Bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 imetenga jumla ya shilingi 0.987 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 13 % ya bajeti yote ya serikali kwa ajili ya kulipa posho chini ya vifungu vinavyojulikana kama "Personnel allowances (non discretionary na In-kind"). Kwa hiyo, kauli ya Waziri Mkulo kuwa serikali itapunguza posho sio kweli. Tunautaka umma wa Watanzania usikubali kurubuniwa.

  4. Wakati Waziri akisema kuwa ili kuthibiti matumizi watapunguza posho mbalimbali, kwenye hotuba yake uk.66, waziri amependekeza kufanywa kwa marekebisho ya sheria ya kodi ya mapato SURA 332 na anasema kwenye (i) "kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa serikali na wanaofanya kazi kwenye taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya serikali" . Hii inaonyesha dhahiri kuwa kauli ya Kufuta au kupunguza posho ilitolewa na Serikali ili kupumbaza wananchi lakini haina udhati.

  5.
  Bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 imewaongezea mzigo mkubwa sana wananchi na haswa wajasiriamali wadogo na vijana ambao wamejiajiri ama kuajiriwa kwenye biashara ya usafiri na usafirishaji. Tunasema hivyo, kwa sababu serikali katika bajeti vyake rasmi vya bajeti imeamua kufanya marekebisho ya sheria ya usalama barabarani sura 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati mtu akiwa anaendesha gari yaani (Traffic Notification Fee), kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 300,000. Lakini Waziri Mkulo katika Hotuba yake aliyoitoa jana ukurasa 74, alitamka kuwa wataongeza kiwango cha faini hadi kufikia shilingi 50,000. Ni dhahiri kuwa kauli ya waziri ya kusema faini itafikia 50,000 wakati kwenye vitabu rasmi vya bajeti faini hiyo inaonekana itafikia 300,000, hivyo alilenga kuuhadaa umma na kuupotosha.

  6.
  Kambi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya Serikali kutenga zaidi ya robo ya Bajeti kulipa Madeni na Kulipana Posho (Asilimia 27 – 14% kulipa madeni na 13% kulipa Posho mbalimbali).

  7. Kambi ya Upinzani itawasilisha Bungeni Bajeti Mbadala siku ya Jumatano tarehe 15.6.2011, saa tano asubuhi ambayo itakuwa inajali masilahi ya Watanzania yenye lengo la kukuza Uchumi wa Vijijini (rural growth) na itajikita katika kupata vyanzo vipya vya mapato na kubana matumizi ikiwemo kufuta Posho mbalimbali.

  Imetolewa leo, Mjini Dodoma, na  Zitto Zuberi Kabwe

  Waziri Kivuli wa Fedha
  [FONT=&quot]Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni  Kutoka Ofisi za Upinzani Bungeni
  Regia E Mtema
  Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
  [/FONT]
   
 6. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hongera Chadema kweli mnastahili kuwa kambi rasmi ya upinzani bungeni na chama kikuu cha upinzani.
   
 7. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #7
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndivyo inavyotakiwa siyo kwa vile imesomwa basi wote tuishie kupiga makofi, Hongereni kwa uchambuzi huu; CDM inaonyesha mmejipanga kwa kazi ya kuwatumikia Watanzania
   
 8. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2011
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Doh! Mmenifungua Macho! Wanachakachua hata bajeti! Makubwa! Asante sana, nadhani saa ya ukombozi i karibu sana sasa! Mungu awabariki azidi kuwapa upeo huu mkubwa wa kuona, ili kumkomboa mtanzania.
   
 9. p

  politiki JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  nina ombi kwako mheshimiwa mtema, naomba hii budget yao ya kitapeli ipitishwe kila mkoa kutapokuwa na maadamano na ichambuliwe ili wananchi wa chini especially vijijini waone utapeli wa seriakali yao. hatuna uwezo wa kufanya lolote kwa maana ya kuikataa kwa kura kwa maana wako wengi bungeni lakini tutachoweza kukifanya ni kwenda straight kwa wananchi na kuwa expose jinsi walivyo.
   
 10. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii habari inatisha.

  Jana niliongea na baba yangu huko kijijini nikamuuliza vipi bajeti? Mzee akasema "Ni nzuri sana, tena ina unafuu kwetu sisi wakulima", then nikajua basi wamejitahidi, kumbe changa la macho!!
   
 11. m

  mdawa Senior Member

  #11
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nadhani hiyo budget ikataliwe warudi kwenye drawing board waandae budget nyingine halafu baada ya hapo wawajibishwe.

  Hizi sio zama za usanii, ni zama za innovation na entreprenuership. Sasa kama haupo innovative na kuwa na mawazo ya entreprenuership huna nafasi katika dunia ya leo zaidi ya kuwa mtumwa wa wengine.

  Tubadilike jamani.
   
 12. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tuko pamoja nanyi, jipangeni vizuri ili atakaye simama afikishe ujumbe kwa watanzania, kwa kuwa watanzanaia wanafahamu idadi ya wabunge wa CCM ni kubwa nakwamba wataitumia vibaya kama historia inavyotwambia, mnapozungumzo kuweni mashujaa na umma tumewapa masikio na akili zetu.

  Tunajua vita hiyo siyo yenu bali ni yetu sote ninyi ni kikosi ambacho kipo mstali wa mbele. Safari hii wasipowasikiliza tunajua watatusikiliza sisi kwa lazima. Hii ni vita dhidi ya ujanja ujanja, ni vita dhidi ya utapeli, ni vita dhidi ya ufisadi, ni vida dhidi ya unyanyasaji, ni vita dhidi ya matumizi mabaya ya vyombo vya dola, ni vita dhidi ya uonevu, ni vita dhidi ya umaskini wa mali, akili na serikali isiyokuwa na vipaumbele vinavyozingatia vitendo vyake.

  Umakini na nia ya dhati ya serikali ya kuleta maendeleo siku zote huonekana kupitia mipango yake na bajeti. Serikali hii inadhani watanzania ni wa mwaka 1950, tuwaonyeshe kuwa sisi ni kizazi cha dot com, kizazi che maarifa kuliko watawala
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,611
  Trophy Points: 280
  Asante Mhe. Regia kutuletea hii. Tunaisubiri kwa hamu bajeti mbadala.
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hongereni vijana wa kazi. Mmeonyesha ukomavu. Jana niliongea na kamanda Slaa na aliniambia kuwa alikuwa anapitia bajeti. Nawakubali, 2015 haiko mbali. Natumaini mtashila dola. VIVA CHADEMA, wafumbueni macho chama cha MAGAMBA.
   
 15. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  That's why we need strong opposition to analyse critically
   
 16. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hili laweza kuwa kweli maana nimesikia hata baadhi ya watu wakisema kuwa bajeti iliyosomwa ni tofauti na ile iliyowasilishwa kwa "mabwana" zao kule Ulaya..........huu ni ushenzi mkubwa kusoma kitu tofauti na uhalisia....

  Kwa nini tu hawaelewi kuwa zama zinabadilika? If they think is some kinda political game hata kwenye issue serious kama bajeti basi wanalolitaka toka kwa watanzania ni janga kwenye mahubiri ya amani
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye nyekundu unajipaisha pasipo sababu!

  Back to the topic....

  Ninaunga hoja hii serikali ni ya kitapeli, imecheza na takwimu kupiga rangi uwongo

  Bajeti tegemezi tena yenye madeni makubwa.

  Kifupi uchumi wa nchi unazidi kudidimia na umasikini kuongezeka. Siwezi shangaa Tanzania Ikawa ni nchi masikini zaidi dunia kwa mwaka ujao wa fedha.
   
 18. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  1. Nadhani Zitto anajua kuwa nishati hapa Tanzania hujengwa kutokana na misaada na mikopo kutoka nje.Hata TANESCO hutafuta funds na mikopo kutoka nje ya serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali,mfano ule wa kusambaza umeme kilomita 667 toka Iringa mpaka shinyanga ambao umekuwa funded na European Investment Bank,shs bilioni 150...je ulikuwa kwenye bajeti yoyote?

  2.Kulipa deni la taifa ni moja kati ya matumizi ya maendeleo,ina facilitate uwezo wa kupata mikopo.

  3. Kuhusu posho, ni wajibu wetu watanzania, hasa wafanyakazi wa serikali kuamua au kujitolea kutokuzipokea au kuomba kupunguziwa kwa asilimia hamsini..... hapatakalika!

  4. Jumatano nakuchallenge Zitto, usome bajeti itakayoonyesha vyanzo mbadala vya kodi na makato ya matumizi, ili elimu iwe bure!...cos you promised this in your campaigns na ilani ya CDM, kama haita-include free education huo utakuwa ni uhuni tu! Ninayo video ya Mnyika akielezea what you will do in your first year kwenye utawala kama mngepata ridhaa.
   
 19. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mimi natarajia kwa waraka huu wa Zito magamba watajibu kwa hoja bungeni na jamvini maana humu wamo kuitetea magamba (vijana wa nepi), nawasubiri faizafoxy na wenzake wajibu kwa hoja maana wanamageuzi hawana hoja
   
 20. Gwaje

  Gwaje JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 271
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 45
  Hongereni wapiganaji wetu
   
Loading...