Zitto matatani - Hii imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto matatani - Hii imekaaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mukuru, Jun 2, 2009.

 1. Mukuru

  Mukuru Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safari ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe nchini Hispania katika mkutano wa kuwakilisha shirika lisilo la kiserikali la Majirani Wasio na Mipaka (NWB) la mjini hapa, imezua mtafaruku mkubwa miongoni mwa viongozi na wanachama wa shirika hilo. Mtafaruku huo unatokana na kitendo cha baadhi ya wanachama kuhoji sababu za Zitto kuliwakilisha shirika hilo katika mkutano huo wakati Mbunge huyo hana nafasi yoyote ndani ya shirika hilo.

  Hayo yalibainika katika mkutano mkuu wa shirika hilo uliofanyika juzi mjini hapa na katika kujadili hoja hiyo, wajumbe walitoa azimio la kutotambua uwakilishi wa Mbunge huyo kwenye mkutano huo. Katika maazimio yao, wajumbe wa mkutano huo, walisema chochote kitakachofanywa na Mbunge huyo katika safari na mkutano huo kisihusishwe kwa namna yoyote na shirika hilo.

  Akisoma maazimio hayo, mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, Pashal Likutuye, alisema pamoja na maazimio hayo, pia wajumbe walilaani kitendo cha Mwakilishi wa Shirika la VSF la Hispania, John Shaaban, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Naibu Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Shaban Mambo (Chadema) kumteua Zitto bila kuitaarifu Bodi ya NWB. Hivi sasa Shaban amefukuzwa nchini kutokana na mtafaruku huo na kufanya kazi nchini bila kibali, sambamba na kukiuka taratibu za hati zinazomruhusu kuishi nchini.

  Mwanachama mwingine, Saidi Maulid, alidai kuwa kwa kiasi kikubwa uteuzi wa Zitto kuliwakilisha shirika hilo Hispania uliegemea kwenye maslahi ya kisiasa kuliko hali halisi, na kuhoji kama shirika hilo halina watu wanaokidhi vigezo vya kuhudhuria mkutano huo na kuliwakilisha shirika badala ya Zitto. Akijibu hoja hiyo, Mwakilishi wa VSF ambayo inatoa ufadhili kwa NWB, Mambo alidai kuwa yeye binafsi ndiye aliyemteua Zitto kuhudhuria mkutano huo.

  Mambo alidai kuwa sababu kubwa iliyomfanya amteue Zitto ni kutokana na mradi mkubwa wa utalii unaotarajiwa kuanza mkoani Kigoma na kwamba anahitajika mtu mwenye uwezo wa kujenga hoja kwa ajili ya wananchi wa Kigoma. Katika hatua nyingine, mkutano huo ulitoa azimio la kumtaka Naibu Meya huyo kuacha kuingilia mambo ya ndani ya NWB kwa vile yeye si kiongozi wala mwanachama wake. Akihitimisha mjadala huo, Mwenyekiti wa Bodi ya NWB, Iddi Ndabhona, alitoa mwito kwa watu kufuata sheria, kanuni na miongozo ya kiutendaji ya shirika hilo.

  Ndabhona alisema kamwe Bodi yake haitakubali watu wachache wajichukulie madaraka ya kufanya mambo kwa niaba ya shirika bila Bodi kuhusishwa na kutoa baraka kwa jambo hilo kufanyika. Hivi sasa kumezuka mtafaruku mkubwa kati ya NWB na wafadhili hao VSF hata kusababisha kusimamishwa ufadhili huo hali ambayo imeanza kuliathiri shirika hilo. Kwa upande wake, Zitto alikiri kuliwakilisha shirika hilo Hispania ambako lilijadili masuala ya utalii. ''Ni kweli nimeshakwenda hiyo safari ambayo hata hivyo nilijilipia mwenyewe nauli ila malazi ndiyo nililipiwa na barua zao za kunialika ninazo.''

  Alisema shirika hilo limekuwa likitoa misaada Kigoma lakini kwa taarifa alizonazo ni kwamba uongozi wake umekuwa katika mgogoro ambao ulifikia hadi kumfikisha mwenzao, Shaban, Uhamiaji kwa madai kuwa anafanya kazi nchini bila kibali jambo ambalo yeye (Zitto) alizungumza na Uhamiaji akaachiwa. ''Labda kwa hilo ndio wamenikasirikia, lakini ninachosema sitaki kabisa wanihusishe na ugomvi wao, mimi kweli si mwanachama wa shirika hilo lakini ni Mbunge ninayewakilisha wananchi, hivyo safari hiyo imekuwa na manufaa kwa jimbo langu hususan upande wa utalii,'' alisema Zitto.

  Alisema hana ugomvi wowote na mwanachama wa shirika hilo na kama ni hiyo safari, hakwenda kwa manufaa yake, bali kwa manufaa ya wananchi jambo ambalo limemfanya mpaka sasa awe anadaiwa na wakala wa usafiri wa Interline dola 1,400 za Marekani za nauli ya safari hiyo. Aliwataka viongozi wa shirika hilo kuacha kuzozana na badala yake watafute mwafaka ili kutowasababisha wafadhili kukimbia kwa maslahi ya wachache.
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  kama ni mwandishi wa habari alipelekea editor hii habari na akaitoa hivi basi nina mashaka na ufanisi wa chombo hicho cha habari (gazeti). Ukiisoma habari kwa makini utagundua negativity mwanzo na positivity somewhere ambao ndiyo ukweli wa kwa nini Zitto aliteuliwa kuhudhuria, if at all it is true.

  Hakuna substance hapo kama ni siasa za kuchafuana Yes!!!! Kwa nini tusihoji zile za Marekani na kwingineko i.e kusafiri about 300 days in a year of 365 days?? Kwa safari hizi utapumzika na kufikiria kwa kiasi gani kwa manufaa ya nchi??? Please, bring critical info here.

  Zitto tupe habari kamili hapa.
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sickness; imekaa kimaslahi binafsi; huenda mkuu huyo alitaka aende yeye ndio aone kazi imefanyika; kumbuka zitto ni MP; kinachotakiwa Zitto aseme ameleta maslahi gani ( tusiwe tunaongelea maslahi ya wananchi); yapi? kama hayakuwepo basi pia aseme kuwa ile ilikuwa safari ya hasara otherwise it was a nice opportunity for the Kigoma people
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wabongo tushazoea ku-politicize kila kitu, sasa mtu hana designation yoyote anapelekwa tu. Halafu hawa ndiyo viongozi wetu wa upinzani walio prominent.

  Zitto naye anataka kukubali safari bila kuielewa designation yake na kama kuna any impropriety?

  Hawa ndio watu wanaoweza kushika serikali kweli? Wana tofauti gani na CCM? Kuna integrity hapa?
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  cha msingi hapa ni Zitto atueleze nini kilitokea maneno mengi hayana maana.
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Na asipokuja kueleza? kama tutasubiri kila mtuhumiwa aje kujieleza hapa tutakuwa na forum kweli?
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hapa naona kama akina Serukamba wako nyuma ya malalamiko haya dhidi ya Zitto.
   
 8. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  mambo si mambo utakua ni mchezo wa kuigiza tu kama katiba aito badilishwa haya bwana Zitto labda wanataka kukushutumu kwa nia mbaya. wakati we una-represent kwa nia njema tunasubiri reaction yako lakini so far sioni shutuma za ubaya bali shutuma ni tukuangalie nyendo zako na we si mwema wanachotaka kutuambia au?
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kitu muhimu zaidi ya nani yuko behind malalamiko haya ni, je yana merit?
   
 10. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Merit ya criticism ni idea ngeni kwetu.

  Unajua ndo kwanza tunaibuka ibuka kutoka enzi za kusifia sifia viongozi na kuimba nyimbo za CCM kwa kila kitu.

  Sijui kama ulikuwa unapenda mpira lakini ukienda uwanja wa Taifa enzi hizo, Yanga ikifunga goli inashangiliwa CCM, CCM, CCM! Simba ikirudisha bao, CCM, CCM, CCM! Wakati ule umasikini umekithiri hamna mfano, ukikutwa na mfuko wa sukari ndani -muhujumu uchumi, tunalishwa ugali wa njano kwa kwenda mbele. CCM, CCM, CCM!

  Utamaduni wa criticism bado hatujauzoea. Huyo alieyeandika inawezekana kabisa kabisa hampendi Zitto. Lakini, je, alichoandika ni kweli uongo? Watanzania bao tunapata tabu kutathmini viongozi wetu.
   
 11. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  sasa yeye kaenda kama mbunge na kuzumngumzia swala la utalii na kasema kajilipia tatizo liko wapi? au kwa vile ni zitto kabwe? kama watu wengine walitaka kwenda na wao kwanini wasingejilipia safari hio?
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Habari inaeleza kuwa amewakilisha shirika la Majirani Wasio Mpaka (NWB) bila ya kuwa na nafasi yoyote katika organisation yao wala kufuata utaratibu wao, nilivyoielewa habari ni kwamba wanasiasa wa Kigoma wamekaa na kumpeleka Zitto huko kama mjumbe wa NWB, sasa kama Zitto ana positions zake zilizo tofauti na za NWB, na amepelekwa huko kama muwakilishi wa NWB bila ya mawasiliano rasmi wala kufuata utaratibu, huoni hapa kutakuwa na conflict?
   
 13. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama walivyochangia wengi, hii issue imekaa kisiasa zaidi. Mwandishi kaelemea upande mmoja. Hao viongozi wa hiyo taasisi wamekaa ki-CCM pia. Hawajatuambia vigezo vya wahudhuriaji ni vipi, lakini wanakimbilia kumponda Zitto. Waweke wazi kwanza nini vigezo vya uwanachama na vigezo vya kuhudhuria mikutano yao. Watuambie ni vipi Zitto ameshindwa kumeet hivyo vigezo.
   
 14. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kigezo kimoja cha wahudhuriaji walitakiwa kuwa ni wajumbe wa NWB. Zitto si mjumbe wa NWB na hivyo hakuwa na sifa ya kuiwakilisha NWB.

  Habari hata kama ina motivation za kisiasa huwezi kusema imekaa ki upande mmoja, kwani hata Zitto mwenyewe amepata nafasi ya kujitetea katika hiyo article na kuna direct quotes kutoka kwake.
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,944
  Trophy Points: 280
  Labda tunahitaji more info,hapo chini Zitto kasema alitumiwa barua,na akapatiwa malazi,je barua hiyo imetoka huko Spain ama Kigoma?
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hii imekaa vibaya.......lakini itategemea zaidi zitto kaalikwa na nani kwenda.
  iwapo yeye aliteuliwa bila kufatwa sheria na jina lake likapelekwa spain na yeye akapata mualiko kutoka spain ( bila ya kujua kuwa aliteuliwa kinyuma cha sheria) anaweza kuwa hana kosa.
  lakini kwa kujua ameteuliwa kimakosa na hali yeye si mwanachama wa NWB na akenda kuwawakilisha huo, amekiuka taratibu .
   
 17. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe kama siyo mwanachamawa asasi fulani halafu unakwenda kuhudhuria kikao kisichokuhusu una maadili kweli? Nashindwa kuwaelewa mnaosema hii imekaa kisiasa. Zitto siyo mwanachama wa taasisi hiyo, alifuata nini???? Hii hoja mbona haijibiwi badala yake zinaletwa hoja uchwara wa safari za rais ili kuficha uzito wa safari hii isiyomhusu Zitto.

  Eti yeye ni mwakilishi, je anawakilisha kila kitu?? Je, ikitokea safari ya Kanisa Katoliki Kigoma kwenda Vatican atakwenda kwa kuwa yeye ni mwakilishi wa watu wa Kigoma? Ikitokea safari ya kwenda Sumbawanga ya watu wa ukoo wa akina Kalumanzila atakwenda kwa kuwa yeye ni mwakilishi??

  Hiyo asasi inauongozi wake unaoeleweka, nani alisema hawajui kujieleza hadi aende Zitto peke yake hata kama hahusiki. Wanaeleza ukweli watu wanaingiza siasa. Hivi hata siku wakienda watu kwenye sherehe ya harusi Mkoani Tabora italazimu Zitto aende kwa kuwa ni mwakilishi wa Kigoma?? Nasema hapa kachemsha na wahusika wana kila haki ya kulalamika bila woga. Tusipende kudandia mambo yasiyotuhusu.
   
 18. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe Zero, kweli zero kweli kweli. Kila kitu CCM, watu wasiseme ukweli??? Utabaki hivyo hivyo tu kwa kupenda chongo unaliita kengeza.
   
 19. T

  TrueVoter JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 873
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 80
  Huwezi amini gazeti lililoandika makala hii ni HABARI LEO linaloendeshwa kwa kodi zetu,hawa wameishiwa wanalipwa mishahara ya bure kwa kuandika uppumbbavu wa namna hii!!!
   
 20. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Zitto alialikwa kwenye mkutano huo na anasema barua za mwaliko anazo,Kwanini asakamwe Zitto badala ya yule aliyemwalika,Mjadala unabidi ukite kwa aliyemwalika Zitto na si kumsakama yeye wakati alikuwa mwalikwa tu.Tatizo si Zitto kualikwa na wala si umuhimu wa kile Zitto alichokiwakilisha...Tatizo ni huyo au hao waliomuzwa na kualikwa kwa Zitto bila kujali kile alichowakilisha na manufaa yake...YAWEZA KUWA KUNA MTU KAKOSA KUPANDA PIPA TU kwa Zitto kwenda kwenye mkutano.
  Leteni katiba ya chama chenu na maudhui ya huo mkutano tuone kama kweli Zitto hakustahili...
   
Loading...