Zitto: Manji anakomolewa, sasa anyang'anywa hisa zake za Tigo na Serikali

Binafsi si amini katika kuonewa.Huyu bwana mkubwa alikuwa ana uwakilishwa mpana na mawakili wanne. Alipata nafasi ya kui-address mahakama na Upande wa pili walifanya majumuisho ya hoja zao. Mahakama ikafanya maamuzi kulingana na uzito wa ushahidi uliomo kwenye jalada na sheria za jinsi zinavyoelekeza. Kuonewa kumetoka wapi tena? Au mahakama ku -move suo motto. In many instances the court of Appeal has been doing so.
 
Zitto zuberi kabwe ulikuwa tegemezi kweli kuokoa jahazi pale madudu yanapotokea bungeni inakuwaje leo uwe upande wa wale wenye hatia na kusema wanaonewa nishawishi kwa hoja nyingine lakini kwa hii hembu jaribu kuchanganua upo...kuhusu tigo we huuoni uhuni wao hasa kwetu ss masikini mpaka wengine tunaamua kuhama mitandao??..sitasema ni uhuni gani lakini naamini kabisa kwamba serekali wameuona na inawezekana pia ikawa sababu ya kunyang'anywa hisa .
Taifa hili ni letu wote kwann unaemtetea leo atuminye alafu na ww usimame na useme anaonewa?...hebu jaribu kutafiti tena alafu tusaidie mawazo ila kumbuka kuungana na serekali yetu ili kuondoa udhalimu kwa pamoja tujenge taifa letu,nakutaki kila la kher na tunakuamini pia katika kutetea haki zetu achana na maslahi yako binafsi kwa sababu hiyo haitakuwa sawa....chiness are saying 'SI SAWA'
 
Serikali inakosea sana kumuhujumu yusuph manji kwa sasa.Sema nae mzee manji alikosea sana kuonesha dharau kwa mkuu wa mkoa hata kama kamzidi umri!!

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
 
Naomba niulizie hapa kidogo.... Hivi nyie watu wote mnaounga mkono kauli ya Zitto kwamba Manji anaonewa, anayofanyiwa ni visasi, mnaweza kunambia Rais Magu au RC Makonda ana kisasi na Manji kuhusu nini? Au mnaounga tu mkono kwasabab mnaamini kila neno analosema Zitto ni sahihi sana? Kwanini mnaona Manji kunyang'anywa hisa za tigo kaonewa? Kwan ni mtu alilala tu na kuamka kumnyang'anya hisa ambazo ni haki yake kabisa bila sababu? Mmefuatilia na kuujua ukweli au mmedandia tu gari ambalo hata hamjui linakotoka wala linakokwenda et kisa tu linaendeshwa na Zitto Kabwe?

Siku zote akili ya kupewa changanya na yakwako.

Huyu ni yule yule Zitto ambaye CHADEMA walimtimua baada kajuthibitisha kwamba ni msaliti. Leo yeye ni mwanachama wa ACT afu anajifanya kuguswa sana na matatizo ya Manji ambaye ni diwani wa CCM, mwana yanga, mtumia Unga, na mengine kibao.... Najiuliza je, wana-kigoma walimtuma hicho? Au anatafuta mdhamini kwenye uchaguzi 2020?
 
Yanayoendelea dhidi ya Yusuf Manji yanashabikiwa na baadhi yetu kwa sababu wanadhani hayatawafika. Tabia ya kukomoa mtu ni tabia mbaya na ina madhara makubwa katika nchi. Ni dhahiri kuwa Manji sasa anaonewa na kudhalilishwa ili kumkomoa kwa sababu ambazo watawala wanazijua wenyewe.

Wakati suala la kutumia unga lipo kortini, Serikali imeamua kumnyanganya hisa zake za Tigo. Sio kwamba Serikali itachukua hisa Hizo, la hasha. Ila Manji azikose tu. Unajiuliza, Serikali hii hii imeacha matapeli wa PAP kuitwaa IPTL na TANESCO inawalipa zaidi ya tshs 300m kila siku.

Leo mpaka mahakama inatumia suo moto kurudisha suala la hisa za Manji kwenye Tigo ambalo halina maslahi yeyote ya Taifa. Kwanini Mahakama haikufanya suo moto kurudisha fedha za Tegeta Escrow?

Watanzania wajue tu kuwa, mwaka 2004 Serikali iliachia hisa zake 20% kwenye Tigo kwa USD 750,000 ( vichekesho) kwa kuiuzia kampuni kutoka Luxembourg. Badala ya Serikali kuhangaika na maafisa wake walioachia hisa kutoka nje ya Tanzania wanahangaika na Mtanzania aliyezirudisha hisa Tanzania.

Uhamiaji wanamwita kuhusu wafanyakazi wake wageni kana kwamba yeye Yusuf ni Afisa Rasilimali watu wa kampuni. Aliko Dangote hakuitwa uhamiaji kwa suala la wafanyakazi wake ila Manji anaitwa.
Wakifanikiwa kwa Manji atatafutwa mwengine, Ni sawa na kula nyama ya mtu. Hutaacha.

Manji anaweza kuwa ana madudu mengi Sana, ahukumiwe kwa haki kwa makosa yake. Asikomeshwe kwani ukomeshaji hautaishia kwake. Asionewe. Atendewe haki. Anyways Kama Mwana Simba, nawasihi Yanga achaneni na mambo ya mabango uwanjani. Hayasaidii lolote.
sheria ichukue mkondo wake. hakuna mkubwa mbele ya sheria.
 
Daaah that is so great my big broder

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Yani serikali ya awamu hii wanafanya mambo kama vile hawataachia madaraka wanafanya kazi kwa visasi na chuki....kila mtu anaona jinsi manji na matajiri wengine wanavyoonewa tusupokemea hili litakuja lingine wanatupanda kichwani sasa shenzi!!! 2020 mabango mtayapata msione tuko kimya alafu na wewe Mtawala usijione rais ukajikuta ushakuwa mungu you only a human acha roho Mbaya

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Tatizo ni kwamba uongozi tulionao sasa unaongoza kwa chuki, wanawachukia sana waliofanikiwa kimaisha kabla, kama mnakumbuka bwanamkubwa aliwahi kusema anataka matajiri waishi kama mashetani akiwa na maana kwamba waishi kama masikini na kitu ambacho hakiwezekani mtu katafuta hela miaka mingi unakuja kumletea jearous kama ulimsaidia katafuta! We have hopples leaders.

Sent from my TECNO F6 using JamiiForums mobile app

Ubaya matajiri wengi Tanzania wametajirika bila ya kufanya kazi. Wametajirika kwa kuwanyonya walio wengi kwa hiyo utajiri wao utaishia njiani, pesa inataka iingie na kutoka, kwa sasa waliokuwa wakiwadhulumu walio wengi Sasa wamekosa deals, soon pesa zao zitaisha, na ndiyo wengi mnaopiga kelele. Serikali ya leo ni ya Watanzania wote, siyo ile ya awali ya watu wachache tu ndiyo wakifaidika kwa kuwadhulumu walio wengi, na wala sio wivu. Mwenye akiri hawezi kumuonea wivu mwizi, kwa kuwa utajiri alionao ni wa bandia. Waliokuwa wakifanya BIASHARA za haki wataendelea vizuri, kwani walikuwa hawategemei kuiba na kujitajirisha kwa wizi bali kwa jasho lao. Na hii ni kweli kabisa, musema kweli ni mpenzi wa MUNGU. Tuache kelele tumuunge Rais mkono kwa kuisafisha Tanzania jamani ilikuwa imechafuka sana.
 
CCM ya Magufuli ni tofauti na CCM ya waliopita, hakuna kulindana! Kudos Magufuli.

Tuna bahati kumpata Rais kama huyu. Hakuna lugha tena ya kusema unanijuwa Mimi ni nani? Lugha ya kuwatisha wengine kwa cheo cha zamana.
 
Yanayoendelea dhidi ya Yusuf Manji yanashabikiwa na baadhi yetu kwa sababu wanadhani hayatawafika. Tabia ya kukomoa mtu ni tabia mbaya na ina madhara makubwa katika nchi. Ni dhahiri kuwa Manji sasa anaonewa na kudhalilishwa ili kumkomoa kwa sababu ambazo watawala wanazijua wenyewe.

Wakati suala la kutumia unga lipo kortini, Serikali imeamua kumnyanganya hisa zake za Tigo. Sio kwamba Serikali itachukua hisa Hizo, la hasha. Ila Manji azikose tu. Unajiuliza, Serikali hii hii imeacha matapeli wa PAP kuitwaa IPTL na TANESCO inawalipa zaidi ya tshs 300m kila siku.

Leo mpaka mahakama inatumia suo moto kurudisha suala la hisa za Manji kwenye Tigo ambalo halina maslahi yeyote ya Taifa. Kwanini Mahakama haikufanya suo moto kurudisha fedha za Tegeta Escrow?

Watanzania wajue tu kuwa, mwaka 2004 Serikali iliachia hisa zake 20% kwenye Tigo kwa USD 750,000 ( vichekesho) kwa kuiuzia kampuni kutoka Luxembourg. Badala ya Serikali kuhangaika na maafisa wake walioachia hisa kutoka nje ya Tanzania wanahangaika na Mtanzania aliyezirudisha hisa Tanzania.

Uhamiaji wanamwita kuhusu wafanyakazi wake wageni kana kwamba yeye Yusuf ni Afisa Rasilimali watu wa kampuni. Aliko Dangote hakuitwa uhamiaji kwa suala la wafanyakazi wake ila Manji anaitwa.
Wakifanikiwa kwa Manji atatafutwa mwengine, Ni sawa na kula nyama ya mtu. Hutaacha.

Manji anaweza kuwa ana madudu mengi Sana, ahukumiwe kwa haki kwa makosa yake. Asikomeshwe kwani ukomeshaji hautaishia kwake. Asionewe. Atendewe haki. Anyways Kama Mwana Simba, nawasihi Yanga achaneni na mambo ya mabango uwanjani. Hayasaidii lolote.
Hata angekamatwa yoyote katika kundi la watu kama hao bado angetokea mtu kama wewe angesema kaonewa kila mtu atashughulikiwa kwa wakati wake at least sasaivi wanakamatwa na tunawasikia wanapata ukumu kulingana na makosa yao. Vipi miaka ya nyuma ? Hili si jambo la mtu mmoja hakuna tena kuwafumbia macho ndo nchi itakavyokuwa kuanzia hapa tulipo nazani tupo katika muelekeo mzuri na sahihi kwa wote.

Sent from my SM-J100Y using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom