Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Vpi kuhusu kushitakiwa MIGA?
Kutoka Mezani kwa Zitto Kabwe,

**********

MAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO.
__________________

Jana, Julai 19, 2019 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick Gold Corporation imetoa Taarifa kwa Umma ya kuinunua Kampuni yake tanzu ya Acacia Mining Plc kwa jumla ya Dola za Marekani Milioni 428. Baada ya malumbano ya takribani miezi 5 Barrick na Acacia wamekubaliana juu ya thamani ya Kampuni ya Acacia kuwa ni Dola za Marekani milioni 951 (wastani wa TZS 2.2 Trilioni).

Itakumbukwa kuwa kabla ya sakata la Makanikia la Mwezi Machi mwaka 2017, Kampuni ya Acacia ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 4,400 (wastani wa TZS 10 Trilioni). Kwa mujibu wa kanuni za Masoko ya Hisa na Mitaji, taarifa za manunuzi ya makampuni huwekwa wazi pamoja na nyaraka nyengine zote husika.

Kwa Watanzania nyaraka muhimu katika mauziano haya ya Acacia, ni ile ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick katika kumaliza mgogoro wa Makanikia na masuala ya Kodi. Nyaraka hiyo (ambayo Serikali imekuwa ikiificha baada ya Majadiliano yaliyofanywa na Prof. Palamagamba Kabudi) sasa imewekwa wazi kama Kiambatanisho namba 4 cha nyaraka za manunuzi ya Acacia.

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na Barrick Gold Corporation mnamo tarehe 19 Mei, 2019. Makubaliano hayo ni MABAYA, ya HOVYO, yasiyo ya KIZALENDO na yanayoumiza nchi kuliko makubaliano yaliyokuwepo kwa Mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010. Kwa ufupi tu ni kuwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi WAMEUZA nchi kwa vipande vya dhahabu. Nitaeleza kama ifuatavyo.

Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.

Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu. Hii ni dharau kubwa ambayo Serikali ya Rais Magufuli imefanya kwa Wananchi na kwa Bunge. Sasa tutazame ni nini Serikali yetu imekubaliana na Barrick Gold katika maeneo matano tu.

1. Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO

Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.

Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.

2. Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M

Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.

Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.

3. Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE

Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.

4. Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote

Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).

Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.

5. Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria

Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.

Serikali mara zote iliambiwa kuwa mabadiliko ya sheria kuhusu ‘arbitration’ hayakuwa halisi na ni ulaghai. Serikali yenyewe imekuwa ya kwanza kuvunja sheria yake yenyewe kwa kuingia makubaliano na Barrick Gold kuwa Mahakama zetu hazitahusika na kutatua mgogoro wowote kati ya Barrick na Tanzania.

Tanzania Imekosa Shilingi Trilioni 2 kwa Sababu ya Viongozi Kukosa Maarifa

Siku za mwanzo kabisa za mgogoro wa Makanikia nilieleza kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina Maarifa ya kuwezesha nchi kupata ushindi katika suala hili, watu wengi walinitukana, lakini leo imedhihirika hivyo.

Wakati ule nilitoa mfano kuwa Acacia ilipotaka kununuliwa na Kampuni nyengine ya Canada kwa thamani ya Dola za Marekani 4.4 Bilioni (wastani wa TZS 10 Trilioni), Tanzania ingefaidika sana kwa kupata Kodi ya Ongezeko la Mtaji ya Dola za Marekani 880 Milioni (wastani wa TZS 2 Trilioni), Serikali haikufanya subira na ikazuia Makanikia na mpango ule wa Acacia kununuliwa ukavubjika.

Leo Serikali yetu imekwenda kuingia MAKUBALIANO YA AIBU kabisa ambayo kiuhalisia tunaishia kufuta kesi za Kodi ya Dola za Marekani 190 Bilioni (wastani wa TZS 400 Trilioni) na tunawalipa Barrick fedha badala ya sisi kupata Fedha. Ni jambo la fedheha mno, wanaojigamba kuwa ni wazalendo leo wametuuza.

Ingekuwa nchi nyengine, Makubaliano haya ya KIMANGUNGO kati ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick, ingetosha kuiondoa Serikali madarakani. Rais John Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi wameuza nchi yetu kwa kipande cha dhahabu. Wamelihujumu Taifa.

Kabwe Z.Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Julai 20, 2019

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe jinga umeshaambiwa kuwa hisa zilikuwa zimesajiliwa DSE tofauti na sasa hivyo watu wazawa walikuwa huru kununua ila kwa sasa hawawezi. Someni muelewe enyi vilaza wa CCM!
Hamaki si jambo jema kwa afya yako, utakufa kwa kushabikia usivyovijua. Unafahamu Mwapachu alipata vipi ukurugenzi wa Acacia?!
 
Vpi kuhusu kushitakiwa MIGA?

Sent using Jamii Forums mobile app

..hawajashtaki kwasababu kwanza Tz imeachana na madai ya usd 191 billion dhidi ya accacia.

..pili, tumeruhusu accacia, ambao tulidai wanatuibia, wasepa kwa kuuza kwa faida hisa zao kwa barrick.

..tatu, tumesaini mkataba mwingine wa kijinga ambao unaruhusu barrick aendelee kutunyonya.

..suala hili CCM mlilikoroga tangu miaka ya 90 mlipopitisha sheria ya hovyo bungeni.

..wako wazalendo wa kweli kama Tundu Lissu na Rugemeleza Nshala ambao walionya kuhusu madhara ya sheria iliyopitishwa na mikataba iliyosainiwa.

..CCM mkubali kuwa mlikosea na mmeisababishia nchi hasara. Haya mashambulizi mnayoelekeza kwa Tundu Lissu ni kuficha aibu yenu kwa sheria za kipumbavu mlizopitisha miaka ya 90.
 
Kutoka Mezani kwa Zitto Kabwe,

**********

MAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO.
__________________

Jana, Julai 19, 2019 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick Gold Corporation imetoa Taarifa kwa Umma ya kuinunua Kampuni yake tanzu ya Acacia Mining Plc kwa jumla ya Dola za Marekani Milioni 428. Baada ya malumbano ya takribani miezi 5 Barrick na Acacia wamekubaliana juu ya thamani ya Kampuni ya Acacia kuwa ni Dola za Marekani milioni 951 (wastani wa TZS 2.2 Trilioni).

Itakumbukwa kuwa kabla ya sakata la Makanikia la Mwezi Machi mwaka 2017, Kampuni ya Acacia ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 4,400 (wastani wa TZS 10 Trilioni). Kwa mujibu wa kanuni za Masoko ya Hisa na Mitaji, taarifa za manunuzi ya makampuni huwekwa wazi pamoja na nyaraka nyengine zote husika.

Kwa Watanzania nyaraka muhimu katika mauziano haya ya Acacia, ni ile ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick katika kumaliza mgogoro wa Makanikia na masuala ya Kodi. Nyaraka hiyo (ambayo Serikali imekuwa ikiificha baada ya Majadiliano yaliyofanywa na Prof. Palamagamba Kabudi) sasa imewekwa wazi kama Kiambatanisho namba 4 cha nyaraka za manunuzi ya Acacia.

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na Barrick Gold Corporation mnamo tarehe 19 Mei, 2019. Makubaliano hayo ni MABAYA, ya HOVYO, yasiyo ya KIZALENDO na yanayoumiza nchi kuliko makubaliano yaliyokuwepo kwa Mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010. Kwa ufupi tu ni kuwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi WAMEUZA nchi kwa vipande vya dhahabu. Nitaeleza kama ifuatavyo.

Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.

Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu. Hii ni dharau kubwa ambayo Serikali ya Rais Magufuli imefanya kwa Wananchi na kwa Bunge. Sasa tutazame ni nini Serikali yetu imekubaliana na Barrick Gold katika maeneo matano tu.

1. Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO

Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.

Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.

2. Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M

Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.

Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.

3. Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE

Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.

4. Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote

Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).

Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.

5. Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria

Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.

Serikali mara zote iliambiwa kuwa mabadiliko ya sheria kuhusu ‘arbitration’ hayakuwa halisi na ni ulaghai. Serikali yenyewe imekuwa ya kwanza kuvunja sheria yake yenyewe kwa kuingia makubaliano na Barrick Gold kuwa Mahakama zetu hazitahusika na kutatua mgogoro wowote kati ya Barrick na Tanzania.

Tanzania Imekosa Shilingi Trilioni 2 kwa Sababu ya Viongozi Kukosa Maarifa

Siku za mwanzo kabisa za mgogoro wa Makanikia nilieleza kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina Maarifa ya kuwezesha nchi kupata ushindi katika suala hili, watu wengi walinitukana, lakini leo imedhihirika hivyo.

Wakati ule nilitoa mfano kuwa Acacia ilipotaka kununuliwa na Kampuni nyengine ya Canada kwa thamani ya Dola za Marekani 4.4 Bilioni (wastani wa TZS 10 Trilioni), Tanzania ingefaidika sana kwa kupata Kodi ya Ongezeko la Mtaji ya Dola za Marekani 880 Milioni (wastani wa TZS 2 Trilioni), Serikali haikufanya subira na ikazuia Makanikia na mpango ule wa Acacia kununuliwa ukavubjika.

Leo Serikali yetu imekwenda kuingia MAKUBALIANO YA AIBU kabisa ambayo kiuhalisia tunaishia kufuta kesi za Kodi ya Dola za Marekani 190 Bilioni (wastani wa TZS 400 Trilioni) na tunawalipa Barrick fedha badala ya sisi kupata Fedha. Ni jambo la fedheha mno, wanaojigamba kuwa ni wazalendo leo wametuuza.

Ingekuwa nchi nyengine, Makubaliano haya ya KIMANGUNGO kati ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick, ingetosha kuiondoa Serikali madarakani. Rais John Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi wameuza nchi yetu kwa kipande cha dhahabu. Wamelihujumu Taifa.

Kabwe Z.Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Julai 20, 2019

Insha hii imejazwa maneno "wastani wa -----'Kila anapotaja thamani ya dola anazozitaja ktk shilingi za kitanzania. Huyu ni mbunge niliyesikia eti anasoma Ph.D, ikimaanisha anayo digrii ya pili, ana uzoefu wa kujisomea, nk. Mara ya kwanza nilidhani ni kosa la uandishi, ikarudiwa tena na tena. Nikathibitisha Zitto uelewa wake ni mdogo. Bado hajui uandishi. Wastani! Yaani hadi leo hajui maana ya neno wastani? Pamoja na mapungufu hayo anaomba tena na tena kuwawakilisha wananchi wa Kigoma!
 
Kwa nini mkataba huu haukuingia Bungeni kujadiliwa na kupata baraka zote za wananchi ...kuna shida gani hapa kuweka mkataba mezani ili watanzania waujue kabla ya kuusign?

Ukitaka kuwaudhi CCM we waambie mikataba iwe inapitia bungeni...!!

Sasa watu wakilalamika ni sawa sababu mambo ya siri huwa hayana baraka.
 
Kaka ni vyema kama unao huo mkataba na sisi tuchambue ili tusiwe gizani maana sio Zitto wala Serikali hawaeleweki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.

Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu. Hii ni dharau kubwa ambayo Serikali ya Rais Magufuli imefanya kwa Wananchi na kwa Bunge. Sasa tutazame ni nini Serikali yetu imekubaliana na Barrick Gold katika maeneo matano tu.
Tatizo la serikali ya Rais Magufuli, tatizo ambalo sasa linajulikana kwamba linafanywa kwa maksudi mazima ni kulidharau bunge.
Amelifanya bunge kuwa ndilo lina matatizo; bunge linamzuia kufanya mambo yake anavyotaka yeye, pamoja na kwamba CCM ndio wenye Bunge.

Anajua hao wabunge wa upinzani wachache waliomo humo, bado watamsumbua kutimiza matakwa yake.

Na kwa vile hawezi kuwafuta wabunge wote wa upinzani waliomo Bungeni, anaona heri asipitishe kabisa taarifa kama hizi Bungeni.

Hii ni tabia yake ambayo sasa inajulikana kwa kila anayetaka kuijua. Maslahi ya nchi nzima, anafanya yeye ndie mwamzi pekee. Hatari sana.
 
Ni mapema sana kujua kuwa ni changa la macho, tusubiri tutakapoanza kukereketwa machoni ndipo tutakapo jua kuwa lilikuwa ni changa la macho.
 
Insha hii imejazwa maneno "wastani wa -----'Kila anapotaja thamani ya dola anazozitaja ktk shilingi za kitanzania. Huyu ni mbunge niliyesikia eti anasoma Ph.D, ikimaanisha anayo digrii ya pili, ana uzoefu wa kujisomea, nk. Mara ya kwanza nilidhani ni kosa la uandishi, ikarudiwa tena na tena. Nikathibitisha Zitto uelewa wake ni mdogo. Bado hajui uandishi. Wastani! Yaani hadi leo hajui maana ya neno wastani? Pamoja na mapungufu hayo anaomba tena na tena kuwawakilisha wananchi wa Kigoma!
"...neno wastani..."; katika yooote yaliyoandikwa, wewe hilo tu ndilo unaloona linamfanya Zitto asiwe na usomi uliodhani anao?

Na bado wewe unayetaka uonekani kuwa na usomi, hujaeleza "...neno wastani..." lilivyofanya andiko lote la Zitto lisiwe la kisomi!
 
..Serikali imepata 16%.

..barrick amepata 84%.

..sasa kwanini serikali wanajiona ndiyo washindi?

..kama sisi tunashangilia 16%, je barrick waliopata 84% wafanye nini?

..na mkumbuke accacia ilianzishwa na ilikuwa inamilikiwa kwa percent kubwa na barrick.

..naomba kuelimishwa kwanini ktk mazingira haya tushangilie kuwa tumepata ushindi.
 
Kutoka Mezani kwa Zitto Kabwe,

**********

MAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO.
__________________

Jana, Julai 19, 2019 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick Gold Corporation imetoa Taarifa kwa Umma ya kuinunua Kampuni yake tanzu ya Acacia Mining Plc kwa jumla ya Dola za Marekani Milioni 428. Baada ya malumbano ya takribani miezi 5 Barrick na Acacia wamekubaliana juu ya thamani ya Kampuni ya Acacia kuwa ni Dola za Marekani milioni 951 (wastani wa TZS 2.2 Trilioni).

Itakumbukwa kuwa kabla ya sakata la Makanikia la Mwezi Machi mwaka 2017, Kampuni ya Acacia ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 4,400 (wastani wa TZS 10 Trilioni). Kwa mujibu wa kanuni za Masoko ya Hisa na Mitaji, taarifa za manunuzi ya makampuni huwekwa wazi pamoja na nyaraka nyengine zote husika.

Kwa Watanzania nyaraka muhimu katika mauziano haya ya Acacia, ni ile ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick katika kumaliza mgogoro wa Makanikia na masuala ya Kodi. Nyaraka hiyo (ambayo Serikali imekuwa ikiificha baada ya Majadiliano yaliyofanywa na Prof. Palamagamba Kabudi) sasa imewekwa wazi kama Kiambatanisho namba 4 cha nyaraka za manunuzi ya Acacia.

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na Barrick Gold Corporation mnamo tarehe 19 Mei, 2019. Makubaliano hayo ni MABAYA, ya HOVYO, yasiyo ya KIZALENDO na yanayoumiza nchi kuliko makubaliano yaliyokuwepo kwa Mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010. Kwa ufupi tu ni kuwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi WAMEUZA nchi kwa vipande vya dhahabu. Nitaeleza kama ifuatavyo.

Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.

Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu. Hii ni dharau kubwa ambayo Serikali ya Rais Magufuli imefanya kwa Wananchi na kwa Bunge. Sasa tutazame ni nini Serikali yetu imekubaliana na Barrick Gold katika maeneo matano tu.

1. Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO

Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.

Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.

2. Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M

Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.

Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.

3. Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE

Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.

4. Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote

Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).

Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.

5. Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria

Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.

Serikali mara zote iliambiwa kuwa mabadiliko ya sheria kuhusu ‘arbitration’ hayakuwa halisi na ni ulaghai. Serikali yenyewe imekuwa ya kwanza kuvunja sheria yake yenyewe kwa kuingia makubaliano na Barrick Gold kuwa Mahakama zetu hazitahusika na kutatua mgogoro wowote kati ya Barrick na Tanzania.

Tanzania Imekosa Shilingi Trilioni 2 kwa Sababu ya Viongozi Kukosa Maarifa

Siku za mwanzo kabisa za mgogoro wa Makanikia nilieleza kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina Maarifa ya kuwezesha nchi kupata ushindi katika suala hili, watu wengi walinitukana, lakini leo imedhihirika hivyo.

Wakati ule nilitoa mfano kuwa Acacia ilipotaka kununuliwa na Kampuni nyengine ya Canada kwa thamani ya Dola za Marekani 4.4 Bilioni (wastani wa TZS 10 Trilioni), Tanzania ingefaidika sana kwa kupata Kodi ya Ongezeko la Mtaji ya Dola za Marekani 880 Milioni (wastani wa TZS 2 Trilioni), Serikali haikufanya subira na ikazuia Makanikia na mpango ule wa Acacia kununuliwa ukavubjika.

Leo Serikali yetu imekwenda kuingia MAKUBALIANO YA AIBU kabisa ambayo kiuhalisia tunaishia kufuta kesi za Kodi ya Dola za Marekani 190 Bilioni (wastani wa TZS 400 Trilioni) na tunawalipa Barrick fedha badala ya sisi kupata Fedha. Ni jambo la fedheha mno, wanaojigamba kuwa ni wazalendo leo wametuuza.

Ingekuwa nchi nyengine, Makubaliano haya ya KIMANGUNGO kati ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick, ingetosha kuiondoa Serikali madarakani. Rais John Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi wameuza nchi yetu kwa kipande cha dhahabu. Wamelihujumu Taifa.

Kabwe Z.Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Julai 20, 2019
Nakubaliana 100% na Zitto. Haya mambo ni size ya wachumi, wahasibu na wataalamu wa biashara. Siyo kila mwana JF anayejua kiingereza anaweza kuinterpret.

Ninachikiona kilichobadilika kwenye mkataba wa Barick ni mrahaba tu kutoka I think 9% (au 6%) alizoacha JK hadi 16%. Lakini naye JK kuna kazi alifanya kwa kuwa wakati wa BWM ilikuwa 3%. Tuendelee hivihivi bila kudharauliana pengine atakayemfuata JPM atatupeleka hadi 20% au 30% kama ilivyo Botswana.

Hii economic benefit ni vague term. Ukisoma kwenye nadharia wanasema yaweza kuwa mapato yaliyopatikana, au gharama zilizookolewa. In short siyo kitu tangible kwa kuwa ni rahisi tu kuambiwa 'hatukupata economic benefits). Hiyo ni changa la macho ambalo negotiations team yetu chini ya Prof Kabudi ilibambikiziwa ikadhani ni kitu cha maana.

Mengine ya USD 190 Bilion maarufu kama Noah kwa kila Mtanzania imekufa na ilikiwa ni ndoto ya mwendawazimu au kwa lugha ya Tundu Lissu Professorial rubbish.

Ile Goodwill ya USD 300 Million imekubaliwa lakini kulipwa ni kwa miaka 6 minus madeni wanayoidai Serikali.

Makinikia yataendelea kupelekwa kama kawaida na Sheria za Tanzania hazitatumika kutatua migogoro, itabaki ni ile ile ya ICSID iliyoko London.

Halafu kuna kigingi kipya kimeongezeka kinasema Mkataba wa Barrick na Tz hautaathirika na sheria za madini zitakazotungwa baadaye.

ACACIA unaweza usiione kewnye logo lakini ACACIA ni Barrick na Barrick ni ACACIA. Makao makuu ya Barrick yako Toronto Canada. Kutokana na namna hizi multi nationals zonavyo manage biashara eapecially baada ya kuwa listed kwenye LSE, ilibidi waunde structure ya management ya shughuli zao London through ACACIA. So don't be fooled kuwa eti kampuni ya ACACIA iliyokuwa inatunyonya imenunuliwa. Bado ipo na kama ni kunyonya itaendelea.
 
Kutoka Mezani kwa Zitto Kabwe,

**********

MAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO.
__________________

Jana, Julai 19, 2019 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick Gold Corporation imetoa Taarifa kwa Umma ya kuinunua Kampuni yake tanzu ya Acacia Mining Plc kwa jumla ya Dola za Marekani Milioni 428. Baada ya malumbano ya takribani miezi 5 Barrick na Acacia wamekubaliana juu ya thamani ya Kampuni ya Acacia kuwa ni Dola za Marekani milioni 951 (wastani wa TZS 2.2 Trilioni).

Itakumbukwa kuwa kabla ya sakata la Makanikia la Mwezi Machi mwaka 2017, Kampuni ya Acacia ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 4,400 (wastani wa TZS 10 Trilioni). Kwa mujibu wa kanuni za Masoko ya Hisa na Mitaji, taarifa za manunuzi ya makampuni huwekwa wazi pamoja na nyaraka nyengine zote husika.

Kwa Watanzania nyaraka muhimu katika mauziano haya ya Acacia, ni ile ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick katika kumaliza mgogoro wa Makanikia na masuala ya Kodi. Nyaraka hiyo (ambayo Serikali imekuwa ikiificha baada ya Majadiliano yaliyofanywa na Prof. Palamagamba Kabudi) sasa imewekwa wazi kama Kiambatanisho namba 4 cha nyaraka za manunuzi ya Acacia.

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na Barrick Gold Corporation mnamo tarehe 19 Mei, 2019. Makubaliano hayo ni MABAYA, ya HOVYO, yasiyo ya KIZALENDO na yanayoumiza nchi kuliko makubaliano yaliyokuwepo kwa Mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010. Kwa ufupi tu ni kuwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi WAMEUZA nchi kwa vipande vya dhahabu. Nitaeleza kama ifuatavyo.

Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.

Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu. Hii ni dharau kubwa ambayo Serikali ya Rais Magufuli imefanya kwa Wananchi na kwa Bunge. Sasa tutazame ni nini Serikali yetu imekubaliana na Barrick Gold katika maeneo matano tu.

1. Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO

Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.

Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.

2. Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M

Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.

Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.

3. Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE

Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.

4. Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote

Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).

Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.

5. Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria

Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.

Serikali mara zote iliambiwa kuwa mabadiliko ya sheria kuhusu ‘arbitration’ hayakuwa halisi na ni ulaghai. Serikali yenyewe imekuwa ya kwanza kuvunja sheria yake yenyewe kwa kuingia makubaliano na Barrick Gold kuwa Mahakama zetu hazitahusika na kutatua mgogoro wowote kati ya Barrick na Tanzania.

Tanzania Imekosa Shilingi Trilioni 2 kwa Sababu ya Viongozi Kukosa Maarifa

Siku za mwanzo kabisa za mgogoro wa Makanikia nilieleza kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina Maarifa ya kuwezesha nchi kupata ushindi katika suala hili, watu wengi walinitukana, lakini leo imedhihirika hivyo.

Wakati ule nilitoa mfano kuwa Acacia ilipotaka kununuliwa na Kampuni nyengine ya Canada kwa thamani ya Dola za Marekani 4.4 Bilioni (wastani wa TZS 10 Trilioni), Tanzania ingefaidika sana kwa kupata Kodi ya Ongezeko la Mtaji ya Dola za Marekani 880 Milioni (wastani wa TZS 2 Trilioni), Serikali haikufanya subira na ikazuia Makanikia na mpango ule wa Acacia kununuliwa ukavubjika.

Leo Serikali yetu imekwenda kuingia MAKUBALIANO YA AIBU kabisa ambayo kiuhalisia tunaishia kufuta kesi za Kodi ya Dola za Marekani 190 Bilioni (wastani wa TZS 400 Trilioni) na tunawalipa Barrick fedha badala ya sisi kupata Fedha. Ni jambo la fedheha mno, wanaojigamba kuwa ni wazalendo leo wametuuza.

Ingekuwa nchi nyengine, Makubaliano haya ya KIMANGUNGO kati ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick, ingetosha kuiondoa Serikali madarakani. Rais John Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi wameuza nchi yetu kwa kipande cha dhahabu. Wamelihujumu Taifa.

Kabwe Z.Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Julai 20, 2019

Sisi tunachojali mauzo ya dhahabu yakifanyika tunapata 50% ya profit ingawa capital yote na uendeshaji umefanywa na Barrick hizo unazosema zimepotea zitarudi kwenye profit tutakayogawiwa ambayo haijawahi kutokea tangu sekta hii ianze
 
..naomba kuelimishwa kwanini ktk mazingira haya tushangilie kuwa tumepata ushindi.
Swali zuri sana, ambalo serikali ingechukua muda kulifafanua kwa wananchi. Lakini najua hawatafanya hivyo. Wao wamekwishatangaza ushindi, na wanategemea wananchi wakubali tu hata bila kuelezwa ni ushindi upi tuliopata?

Hili ni moja ya mambo makubwa sana yanayotofautisha uongozi wa Mwalimu na hawa wengine. Mwalimu angechukua muda wa kulielezea hili na kuwaondoa wananchi wasiwasi. Hawa wengine wanafunikafunika tu, mradi wametangaza ushindi.

Na upande wa pili, pamoja na akina Zitto kuweka jitihada za kuonyesha kwamba hakuna manufaa ya ziada yaliyopatikana nao ingebidi wakayaeleza ya upande wao kwa lugha rahisi ili wananchi wapime na kuelewa.

Katika hali ya kawaida, hili lingekuwa agenda nzuri sana ya kampeni mwaka huu. Lakini najua wahusika wataliachia hapo hapo lilipofikia, na hakuna atakayelikumbuka tena.
 
zitto Alizoea kuhongwa hela na ACACIA yeye na Tundu Lisu .Ana hasira za Mtoa Rushwa ACACIA aliyekuwa akiwapa kufungishwa virago na Barrick kuingia ndani ya nyumba.
Acha kukatakata kiuno hapa..
Jibu hizo hoja 5 za Zitto hapo..
Dimwit..Moron.
 
Back
Top Bottom