Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

”Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.”
Hakuna Acacia tena uelewe nini..?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingekuwa vyema sana ukaweka kiambatanisho kile Na. 4 katika makubaliano kati ya Barrick Gold Mines na GoT kilichotolewa na Barrick Mines kwa mujibu wa kanuni za masoko ya hisa ya Ulaya na USA kama ulivyoeleza ktk andiko lako

Naamini haitakuwa dhambi wala kuvunja sheria yeyote kwa kuu - display hapa kwa sababu tayari hiyo iko wazi kwenye masoko ya huko nje

By the way ni kuthibitisha kuwa ulichokiandika na kukiwasilisha hapa in ukweli halisi na siyo vitu ulivyoandika tu....

Na pia utawanyamazisha wote wanaokuona kama unafanya juhudi za kuichafua serikali yao tu kwa wao kutazamwa na ukweli katikati ya nyuso zao hadi waone aibu...!
 
Magufuli, Kabudi na Dotto Biteku eti ndiyo wanategemewa kutuongoza kiakili. Kimsingi nilishawapuuza kwakuwa ndani ya serikali ya Magufuli kuna kiwango kikubwa sana cha ukilaza. Kazi kujikusanya kwenye TV na kutoa mahubiri kila kukicha.
 
zitto Alizoea kuhongwa hela na ACACIA yeye na Tundu Lisu .Ana hasira za Mtoa Rushwa ACACIA aliyekuwa akiwapa kufungishwa virago na Barrick kuingia ndani ya nyumba.
Atueleze kwa hiyo sheria ya 2010 ni watanzania gani waliomiliki hiyo 30% ya hizo hisa kama sio haohao kina Mwapachu.
 
zitto Alizoea kuhongwa hela na ACACIA yeye na Tundu Lisu .Ana hasira za Mtoa Rushwa ACACIA aliyekuwa akiwapa kufungishwa virago na Barrick kuingia ndani ya nyumba.
Umeelewa hata kilichoandikwa hapo binti.
 
Atueleze kwa hiyo sheria ya 2010 ni watanzania gani waliomiliki hiyo 30% ya hizo hisa kama sio haohao kina Mwapachu.
Na hao Akina mwapachu walikuwa tu proxy wakishililia hisa za wezi akina Lowasa,Zitto Kabwe ,Tundu Lisu na wezi wenzao.

Ndio maana akina Lowasa ,Zitto kabwe na akina Lisu waligeuka matajiri ghafla
 
Mkuu hawa watu hata ukiwaelimisha mwaka mzima juu hiyo mikataba hawawezi kuukubali ukweli maana wao wamefundishwa kushangilia tu
Ingekuwa vyema sana ukaweka kiambatanisho kile Na. 4 katika makubaliano kati ya Barrick Gold Mines na GoT kilichotolewa na Barrick Mines kwa mujibu wa kanuni za masoko ya hisa ya Ulaya na USA kama ulivyoeleza ktk andiko lako

Naamini haitakuwa dhambi wala kuvunja sheria yeyote kwa kuu - display hapa kwa sababu tayari hiyo iko wazi kwenye masoko ya huko nje

By the way ni kuthibitisha kuwa ulichokiandika na kukiwasilisha hapa in ukweli halisi na siyo vitu ulivyoandika tu....

Na pia utawanyamazisha wote wanaokuona kama unafanya juhudi za kuichafua serikali yao tu kwa wao kutazamwa na ukweli katikati ya nyuso zao hadi waone aibu...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
zitto Alizoea kuhongwa hela na ACACIA yeye na Tundu Lisu .Ana hasira za Mtoa Rushwa ACACIA aliyekuwa akiwapa kufungishwa virago na Barrick kuingia ndani ya nyumba.
Ungechambua hoja zake kwa data kama alivyofanya yeye badala ya mipasho !!. Aina ya watu wanaojikomba kwa watawala mna kasoro sana za kiuchambuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania ilifaa tusitishe uchimbaji wa maliasili zote,hasa madini. Sababu kubwa ni kwamba bado hatuna watu wenye ujuzi wa kusimamia sheria madini kati yetu na makampuni ya nje yenye ujuzi na mbinu nyingi za uwizi mkubwa kwa njia za mikataba. (INAUMIZA SANA).

Kuona kwamba toka tuanze kuingia hiyo mikataba ya uchimbaji madini na makampuni ya nje hakuna tunachonufaika nacho,zaidi ya kutuachia mashimo,umasikini uliokithiri na magonjwa ya madawa kwa maeneo yenye uchimbaji. Narudia tena bado hatuna watu wenye ujuzi wa mikataba ya kimataifa kuhusiana na madini.

KIPI TUFANYE BAADA KUSITISHA MIKATABA YOTE?
Tungejipanga kwanza. Serikali ingepeleka kwanza watu wetu wa aina mbili wakasomee kwa hali juu haya mambo ya madini. Kwanza wapeleke watu wengi wakasomee sheria tu zinazohusiana na mikataba.

Pili wapeleke watu wengi wakasomee utafiti wa miamba,madini na mali ghafi zote zinazopatikana chini ya ardhi ikiwemo mafuta na uranium. KWA NAMNA YA HIVI TUTAENDELEA KUIBIWA SANA KWA MIKATABA YA WANAOJUA WANAFANYA NINI. MUNGU IBARIKI TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom