Zitto, Makalla, Ndassa waingia Simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto, Makalla, Ndassa waingia Simba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mdau wetu, Oct 18, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WABUNGE watatu wa Tanzania wameteuliwa kuwa Wajumbe wa kamati mbalimbali ndani ya Klabu ya Simba ya Dar es Salaam.

  Wabunge hao ni Kabwe Zitto wa Kigoma Kaskazini, Richard Ndassa wa Sumve na Amos Makala wa Mvomero.

  Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Rage alisema uamuzi wa kuwaingiza wabunge hao ulifikiwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya Simba kilichofanyika Jumamosi iliyopita na kuamua kufanya mabadiliko ya kamati zake ndogo.

  Kwa mujibu wa Rage, lengo la mabadiliko hayo ni kuboresha mfumo wa uendeshaji wa klabu na kujenga misingi imara.

  Alisema Kamati ya Fedha Mwenyekiti wake atakuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na Makamu wake atakuwa Adam Mgoi huku wajumbe wakiwa ni Said Pamba, Kifiri, Kabwe Zitto na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania, (Taswa), Juma Pinto.

  Rage alisema Kamati ya Usajili itaongozwa na Zacharia Hans Poppe, ambapo Makamu Mwenyekiti atakuwa Kassim Dewji ambaye amepata kuwa Katibu Mkuu wa Simba.

  Dewji ambaye pia ni mmoja wa vigogo wa kundi la vibopa wa klabu hiyo maarufu kama Friends of Simba amewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba miaka ya nyuma.

  Wajumbe wa kamati hiyo ni Francis Waya, Crecentius Magori, Salim Abdallah, Collins Frisch na Gerald Lukumay.

  Kwa mujibu wa Rage, Kamati ya Mashindano itaongozwa na Joseph Itang’are, Makamu wake atakuwa Azim Dewji na wajumbe ni Jerry Ambe, Swedy Mkwabi, Hassan Hassanol, Mohamed Nassoro, Mbunge wa Mvomero, Amos Makala, Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa na Suleiman Zakazaka.

  Kamati ya Ufundi Mwenyekiti wake atakuwa ni Ibrahim Masoud, Makamu wake ni Evans Aveva na wajumbe ni Dan Manembe, Khalid Abeid, Musley, Mulamu Nghambi, Said Tuli, Rodney Chiduo na Patrick Rweyemamu.

  Alisema Kamati ya Nidhamu Mwenyekiti atakuwa Peter Swai, Makamu wake ni Jamal Rwambow na wajumbe ni Charles Kenyela, Evody Mmada na mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Chaurembo.

  Wakati huo huo, Rage amesema kwamba jengo la Klabu hiyo lililopo mtaa wa Msimbazi litavunjwa mwakani na kujengwa upya ghorofa 12.

  “Tumezungumza na benki mbili ambapo moja tutaingia nayo ubia na jengo hili litavunjwa na kujengwa upya kwa ghorofa 12,” alisema.

  Alisema lengo la kulijenga upya jengo hilo, ni kwa ajili ya kuboresha vitega uchumi vya klabu ili iondokane na utegemezi wa watu wachache.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,427
  Trophy Points: 280
  Msije mkaingiza siasa kwenye chama letu...zitto ...na wengine mlioteuliwa kila la kheri tunawatakia
   
 3. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  dah!kweli S.S.C wajanja yaani wamechukua wakali wangu ninaowaaminia katika mambo ya kijamii!....wazee wa twanga pepeta miaka mia!
   
 4. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huenda wakafanya kweli wapewe muda
   
Loading...