Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,629
- 46,718
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Murtaza Mangungu, amesema klabu hiyo haina Mtendaji Mkuu, akieleza kuwa nafasi hiyo ipo katika kampuni ya Simba Sports Club Company, ambayo ina Mtendaji Mkuu wake.
Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, Mangungu amesema kuna Mtu mmoja aliyesajiliwa na Bodi ya Michezo ya Tanzania (BMT), huku mwingine akiwa amesajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), akisisitiza kuwa usajili huo unatokana na sheria tofauti.
“Simba Sports Club haina Mtendaji Mkuu, labda kama yupo basi ni kwenye Simba Sports Club Company ndiyo ina Mtendaji Mkuu, kuna mmoja amesajiliwa na BMT na mwingine amesajiliwa BRELA ni kutoka sheria tofauti, Katiba inasema Simba Sports Club inatakiwa kuwa na Mtendaji wake na tutamtangaza kwa Taifa”