ZITTO:Mahakama ni Chombo cha kutoa haki

Status
Not open for further replies.

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,281
2,000
Mahakama ni Chombo cha kutoa haki. Nimeomba mahakama kuzuia kamati kuu ya chama changu kunijadili mpaka rufaa yangu isikilizwe na Baraza Kuu la chama. Sijaomba kuzuia kamati kuu kuendelea na kikao chake. Nimeomba kamati isinijadili maana nina rufaa kwenda Baraza Kuu kwa jambo hilo hilo ambalo kamati kuu inataka kuliamulia. Wakili wa chama Tundu lissu aliweka mapingamizi akisema mahakama haina mamlaka kujadili masuala ya vyama na wanachama wao. Jaji John Utumwa katupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa na Tundu Lissu.
Mahakama ndio Chombo cha kutoa haki. Asante Wakili Albert Msando.
 

m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,367
2,000
Kufukuzwa kupo pale pale hivyo mwacheni ajifariji kwa kuchelewesha!
 

Danisamweswa

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
453
195
Hivi chombo kilichomwambia Zitto ajieleze kwa maandishi kwa nini asifukuzwe kwenye chama ni kipi? Je anakataje rufaa kabla ya chombo kilichomtaka ajieleze hakijafanya maamuzi ? Rufaa yake ina hoja gani wakati shauri lake na cc halijaamuliwa? Naomba kuelimishwa hapa.
 

peri

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,581
1,225
huyo ndio zito, cdm mmegonga mwamba.
Mnapambana na mtu anaejitambua, mbowe na wenzako jiandaeni kwa anguko.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Alitakiwa ajue mapema kwamba usaliti na ubinafsi ndani ya chama ni hatari kwa mshikamano ndani ya chama, sasa anatapatapa huku na kule. Jamaa huyu ana akili finyu sana labda, labda alidhani madudu yake dhidi ya mshikamano na uhai wa chama yatavumiliwa daima.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom