Zitto live chanel ten asubuhi njema

Pukudu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
3,148
2,219
Mheshimiwa Zitto yuko katika kipindi cha asubuhi njema channel ten anaelezea Bajeti ya Upinzani 2011-2012 inavyomsaidia mwananchi
 
anasema wao ka wapinzani wanatoa bajeti ili kukosoa wale waliopewa ridhaa ya kukusanya na kutumia kodi, anatoa mfano kwamba wao ni kama mbwa wa tajiri na matajiri ni watanzania kwa hiyo jazi yao ni kuwalinda CCM na kubweka ili kumshtua tajiri pindi CCM inapofanya vibaya
 
kalitolea ufafanuzi suala la posho za vikao kuwa, vikao ni suala la majukumu ya kazi so huwezi kulipwa kwa kufanya kazi yako huku ukilipwa mshahara kwa kazi unayoifanya
 
anasema wao ka wapinzani wanatoa bajeti ili kukosoa wale waliopewa ridhaa ya kukusanya na kutumia kodi, anatoa mfano kwamba wao ni kama mbwa wa tajiri na matajiri ni watanzania kwa hiyo jazi yao ni kuwalinda CCM na kubweka ili kumshtua tajiri pindi CCM inapofanya vibaya

Hii imekaa sawa, kumbe anafahamu wajibu wa chama cha upinzani. Ndivyo Wapinzani wa Serikali yoyote ile wanavyopaswa kufanya kwa sababu kazi yao ni kuikumbusha Serikali pale inapokosea. Na pale Serikali inapofanya vizuri ipewe sifa yake. Tatizo la baadhi ya wapinzani tulio nao ni kupingana wao kwa wao, hata kama jambo alilofanya mwenzake ni zuri.
 
pia kuwe na mfuko wa afya , pamoja na pensheni ya wazee.
Vipaumbele ni sula la nini ufanye kwanza na vingine vitafuata baada ya yale ya msingi kufanywa
Anasema bajeti yao ina vipaumbele vya Elimu ikiwa pamoja na elimu ya ufundi mfano kodi ya ujuzi ambayo ni 6% ya payroll anayotozwa mmiliki wa kampuni yeyote yenye wafanyakazi kuanzia sita theluthi mbili iende kwa bodi ya mikopo na inayobaki iende kwenye maendeleo ya elimu ya ufundi. Na serikali imelifanyia kazi so instead ya kwenda serikalini na kulipia gharama nyingine ka posho serikali imekubali kutumia hilo pato kwa elimu
 
Yes, tuko kwenye mwelekeo mzuri na sasa ni zamu ya Mkuro kuonesha kuwa anauwezo wa kulinda uchumi wa nchi hii. Anauwezo wa kupanga bajeti bora kuliko ya Chadema yenye wabunge 40 na kidogo!!! Ila nashituka sana kuona kuwa CCM yenye wabunge zaidi ya 200 haiwezi kutengeneza bajeti bora hata robo ya ubora wa hiyo ya CDM.
 
Nimesikia kwenye Magazeti asubuhi hii wabunge wa CCM wakiongozwa na Chiligatio wakipinga VIKALI uondolewaji wa hizo posho za vikao wanasema hayo ni mawazo ya mtu binafsi na km vipi wapinzani waamue wao wasichukue hizo posho lkn wao CCM watazidaka kwa kwenda mbele tuuu
 
Back
Top Bottom