Zitto kung’oka CHADEMA

Zitto kung’oka CHADEMA

lidoda

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2008
Posts
641
Reaction score
576
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), inadaiwa yupo katika hatua za mwisho kujiengua ndani ya chama hicho alichojijengea sifa kubwa

Kwa mujibu wa watu walio karibu na Zitto, wamelidokeza Tanzania Daima Jumapili, kuwa mbunge huyo alipanga kujiondoa ndani ya chama hicho mwezi uliopita lakini alishindwa kufanya hivyo kwasababu ambazo hazijawekwa wazi.

Inadaiwa Zitto, alipanga kuondoka CHADEMA sambamba na uzinduzi wa kitaifa wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) uliopangwa ufanyike mwezi uliopita.

Novemba 22, mwaka jana, Kamati Kuu ya CHADEMA iliamua kumvua nyadhifa za uongozi Zitto na wenzake wawili (Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba) kwa madai ya kukisaliti na kukihujumu chama.

Zitto alidaiwa kuwa kinara wa mkakati wa kuleta mabadiliko haramu ndani ya chama hicho, huku waasisi hao wakijipa majina ya MM, M1 na M2 ambao ndani yake anadaiwa kuwamo Dk. Kitila Mkumbo, mjumbe wa CC na NEC.

Hata hivyo Mkumbo na Mwigamba walivuliwa uanachama huku Zitto akikimbilia Mahakama Kuu kutaka CC isijadili unachama wake.

Katika hoja ya msingi iliyowasilishwa na Zitto kupitia wakili wake Albert Msando, aliiomba Mahakama Kuu kuwazuia washitakiwa kwa pamoja ambao ni Kamati Kuu ya CHADEMA au chombo chochote kwa makusudi, kujadili au kuamua suala la uanachama wake.

Maombi mengine ya Zitto ni kutaka apatiwe nakala za uamuzi wa Kamati Kuu iliyoamua kumvua uanachama ili aweze kukata rufaa kwa Baraza la Uongozi la CHADEMA.

Katika ombi la tatu, Zitto anaiomba mahakama iwazuie washitakiwa kuingilia kati wajibu na majukumu yake ikiwemo majukumu yake kama mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Mahakama Kuu ilikubali kwa muda kusitisha uamuzi wa CC ya CHADEMA kujadili uanachama wa Zitto mpaka itakapotoa uamuzi wa katika kesi ya msingi iliyofunguliwa na mbunge huyo.

Katika amri hiyo, Jaji John Utamwa alisema kwa kuzingatia masilahi ya pande zote mbili ni vema walalamikiwa wakasitisha uamuzi wowote wa kujadili uanachama wa Zitto mpaka shauri hilo litakapotolewa uamuzi na mahakama.

Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa Zitto, anatarajia kwenda ACT-Tanzania kushikilia wadhifa wa Mwenyekiti wa chama hicho ambacho makada wenzake Mkumbo na Mwigamba wamekimbilia.

Harakati hizo za Zitto, zinadaiwa kushamiri zaidi hivi sasa baada ya CHADEMA kumaliza uchaguzi wake wa kitaifa na nafasi aliyokuwa akiishikilia imejazwa na John Mnyika

Kumalizika kwa uchaguzi wa CHADEMA, uliofanyika kwa utulivu hivi karibuni kunatajwa sababu ya Zitto kukata tamaa ya kurejea madarakani hivyo anaona njia pekee ya kujinusuru kisiasa ni kuhama CHADEMA.

Mbunge huyo kabla ya kukimbilia mahakamani alitaka kiitishwe kikao cha Baraza la Uongozi ili apewe fursa ya kujitetea ambako aliamini atapata uungwaji mkono

Hata hivyo tangu Zitto atoe ombi hilo Baraza hilo limeketi mara mbili bila kuwepo ajenda inayomuhusu kujadiliwa jambo lililoashiria hakukuwa na uungwaji mkono

Zitto afunguka

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, juu ya taarifa za kujitoa CHADEMA, Zitto alisema kwa muda mrefu kumekuwa na taarifa potofu dhidi yake.

Alisema baadhi ya taarifa zina lengo la kumchonganisha na kumharibia sifa yake mbele ya jamii na makada wenzake.

Zitto alisema jambo lolote linalomhusu hatosita kulizungumzia mwenyewe kama alivyowahi kufanya katika masuala mbalimbali.

Alisema kwa muda mrefu kumekuwa na mambo yanayovumishwa dhidi yake ambayo hayana ukweli

Zitto, alibainisha kuwa ikiwa ataondoka au ataendelea kubaki CHADEMA jambo hilo analijua mwenyewe.

"Watu wasema mambo kwa kuhisia hisia, mimi ndiye ninajua ninachokifanya……Hizo nyingine ni hisia za watu siwezi kuzizuia" alisema

"Nawaomba watu wajiepushe na maneno maneno ya mitaani, nina uwezo mkubwa wa kuzungumzia masuala yanayonihusu" alisema.

Dk. Slaa anena

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa, amesema ni haki ya kikatiba na ruhusa kwa mwanachadema yoyote kuhamia chama chochote cha siasa anachoona kinamfaa.

Dk. Slaa, alisema fununu za aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe, kutaka kujiunga na chama kipya cha ACT Tanzania, anazisikia na hawezi kumzuia kuhamia huko.

Alisema haoni kama anayo sababu yoyote ya kumjadili Zitto katika uamuzi wake wa kutoka CHADEMA na kuhamia chama kingine.

"S mimi Dk. Slaa wala CHADEMA, wanayo sababu yoyote ya kumjadili mtu na uamuzi wake mwenyewe …anayo haki ya kuhamia chama chochote ambacho ataona ana manufaa nacho, hana haja ya kupata kibali cha mtu"

"Zitto hatokuwa mwana- CHADEMA wa kwanza kuhama cha hiki na wala hatakuwa wa mwisho ….wengi watahama na wengi watahamia hivyo sioni kama kuna dhambi yoyote hapo" alisema

Katibu Mkuu huyo alisema kwa sasa hayuko tayari kuzungumzia mwanachama anayehama na kuhamia, bali yuko tayari kujadili maslahi ya Watanzania na nchi hasa suala la katiba iliyopendekezwa.

"Kichwa changu sasa kinafikiria ni namna gani kitawasaidia Watanzania waikatae katiba inayopendekezwa ambayo imechakachukuliwa kwa ajili ya manufaa ya watu wachache" alisema.


Chanzo: Tanzania Daima
 
Wanabodi,

Naanza kwa angalizo, hii ni thread ya news tip tuu, for your info!, sio lazima kuchangia!.

Na ikibidi kuchangia, please please please!, usitaje nina la mtu yeyote kwa sababu hata mimi muanzisha thread, sijataja nina la mtu yeyote bali nimeweka sifa tuu!.

Kama wewe uu miongoni mwa wale wajinga wajinga ambao kazi yao ni kutaja taja tuu majina ya watu!, I'm sorry hapa sii mahala pako!.

Mwanasiasa kijana, mwenye mvuto kwa vijana, na nguvu kubwa ya ushawishi, kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja!, ambaye yuko kwenye mgogoro na chama chake, inasemekana hatimaye amekubali yaishe, ataifuta kesi aliyokifungulia chama chake, atabwaga manyanga katika chama hicho, ikiwa ni pamoja na kuusamehe ubunge wake, atafungasha kilicho chake na kujisepea zake, huku akiwaachia wenyewe chama chao, waendelee kungaika nacho!.

Japo taarifa hii niumeipata toka kwa mtu wa kuaminika, naaita tetesi hadi hapo hili litakapofanyika, kwa sababu wanasiasa sio watu wa kuwaaminia sana!, leo anaweza kusema hivi na kesho kuamua kingine, au leo anaweza kuahidi hili na kesho akabadili mawazo!.

Le bila hata kuithibitisha, ni kukupa wewe mwana jf, ile advantage ya "be the first to know!".

Kufuatia ethics za journalism, silitaji kwanza jina, mpaka hili tukio litakapotokea, na pia naomba nisiitaje source yangu, kwa kutumia kipengele kiitwacho "the confidentiality of the source!".

Information is power, be informed kwa jambo hili kubwa kabisa kuwahi kutokea kwenye siasa za upinzani!.

My Take!.

Kama tetesi hizi ni kweli, then hii itakuwa ni one of the best moves mwanasiasa huyo ameweza kuifanya!.

Wengi wa wanasiasa wetu, ni wanasiasa njaa!, siasa kwao ni ajira!, wanautafuta ubunge sio kwa lengo la kutumikia watu bali kutafutia ulaji!, hivyo kwa wanasiasa wengi njaa njaa, ubunge ndio ajira yao, wakiukosa ubunge, wataishia kujifia njaa!. Kitendo cha mwanasiasa huyu, kukubali kuachia ubunge, ni uthibitisho, ubunge kwake sio ajira bali ni utumishi wa watu!, kama hapo ulipo, umefungwa mdomo, mikono na miguu kushindwa kuwatumikia watu, then, unajifungashia virago vyako na kujiondokea kwa amani, kwenda kuwatumikia watu mahali pengine!.

Move hii pia itakisaidia sana chama chake, kitendo cha kukubali yaishe kwa ridhaa yako mwenyewe na kuifuta kesi, ni uthibitisho wa good faith, ikitokea 2015, chama chake kikashindwa kufikia malengo ya kutinga Ikulu, wasndishwe kwa mengine, wasije kumletea, kisingizio, cha kesi!.

Na mwisho, kama ni kweli mwanasaiasa huyu ni msaliti kama alivyoelezwa kwenye chama chake, then, "karma" itamchapa bakora vilivyo!, lakini kama amesingiziwa, na kuhukumiwa kwa maonevyo, hivyo hiyo "karma" ita mu elevate to an imaginable height huko aendako, at the same time, kitakula bakora za "karma" kwa maovu waliomtendea!.

Kama una nyota, una nyota tuu, kama uling'ara, maisha ni popote na utang'ara tuu!, kama huta nyota, bali uling'arishwa, basi ukitoka ni lazima utafifia!. Hata maisha ya kisiasa pia ni maisha popote!.

NB. Baadhi ya thread nyingine zinaita "info pack" kwa ajili ya kutoa tuu information, na sio kujibishana na watu au kuchangia!. Unaweza kusoma tuu na sio lazima kuchangia!, na kuyasubiria haya yaliyozungumzwa humu yameterialize!.

Natanguliza shukrani kwa kunielewa.

Asante.

Pasco

Haya tuliyasema humu, kitambo!.

Pasco
 
Until when mtazunguzia suala hili? Mnataka kuendelea kumpunguzia Umaarufu? Msimtajetaje...

Sio chochote kwenye Siasa ya NCHI ya TANGANYIKA labda kwa SIASA za kulazimisha ubaguzi za KIGOMA...

Our Country POLITICS is tired na Greedy POLITICIANS!!!!!!!!!
 
Pasco kama ulivyosema jamaa karuka mita 100 kweli wanasiasa ni watu wa kubadilika badilika.
 
Last edited by a moderator:
zzk ameshndwa kusaidia jthada za kupata maji kgma kaskazn wanawake wanahangaika kusafir umbal mref kuyafuata maj ila leo mnamwta mtu maarufu?
 
Akili ya zitto peke yake ni zaidi ya uongozi wa chadema taifa kwa pamoja yao
 
Zitto anachukiwa na viongozi wa chadema, wakamfitni kisa hatoki kaskazini. Ubaguzi ndani ya chadema ni mkubwa sana
 
Watasikika wakisema,

Who is Zitto!

Hana impact yoyote ndani na nje ya CHADEMA!

Hata huko Kigoma, hana Wabunge na Madiwani wa CHADEMA!

CHADEMA ndiyo imemfikisha hapo alipo!

Chama hakiwezi kuruhusu wasaliti ndani ya chama!

CHADEMA kwa sasa ni imara zaidi baada ya kumuondoa kwenye uongozi!

Etcetera, Etcetera...
 
Aende tu mnafiki akaendeleze unafki wake huko na usaliti shit.
 
Hadi 2015 atabaki mbowe na mtei tu kwenye hiyo saccos
 
Aondoke mbona anajishaua yuda mkubwa yeye! Magamba lazma yasuguliwe
 
Watasikika wakisema,

Who is Zitto!

Hana impact yoyote ndani na nje ya CHADEMA!

Hata huko Kigoma, hana Wabunge na Madiwani wa CHADEMA!

CHADEMA ndiyo imemfikisha hapo alipo!

Chama hakiwezi kuruhusu wasaliti ndani ya chama!

CHADEMA kwa sasa ni imara zaidi baada ya kumuondoa kwenye uongozi!

Etcetera, Etcetera...

napata wasiwasi sana wewe kumsifia zitto hilo ndilo linalomponza haiwezekani mkamsifia mbunge wa upinzani kama kweli yupo kinyume na nyinyi
mmeshindwa kujificha kama mnamtumia ndio maana tumegutuka
 
Back
Top Bottom