Zitto: Kauli ya Waziri Kabudi kuhusu kutotangaza mapato kutoka Tanzanite One ni ya kitoto na kujidhalilisha

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Taarifa kwamba Waziri kabudi bila aibu ametamka mbele ya Bunge kuwa kiasi kilicholipwa na Tanzanite One kwa Serikali haitaweka wazi kwa Public kwa kuogopa kufunguliwa mdai na wadai wetu ni ya kitoto na ya kujidhalilisha.

Nashukuru Tundu Lissu amelisemea vizuri. Mimi niongezee tu kuwa mikataba au makubaliano yamefanywa kati ya Serikali na Kampuni. Kama Serikali imeamua kuficha taarifa ya malipo yaliyofanywa na Kampuni ya Tanzanite kwa Serikali, basi Waziri amejidanganya kwa sababu Kampuni ya Tanzanite kama kampuni zote Duniani zinakuwa governed na sunshine clause na disclosure clause sheria ambazo zinayataka makampuni siyo tu kuyaweka mapato na matumizi yao hadharani, bali pia kupitia taarifa hizo kwa mtu yoyote atakayezihitaji chini ya " right of information."

Kwa hiyo kana ni kweli Tanzanite One wamefika chochote, Public itajua kupitia Tanzanite One. Hakuna siri hapo. Msichana akimwambia mama yake kuwa amepata mimba lakini hataki mtu yoyote ajue, huo ni utoto kwa sababu mumewe atasema na tumbo lake litaonyesha.

Aidha, tamko hilo ni la kujidhalilisha kwa sababu linajenga taswira mbaya kwenye macho ya wengi. Kwamba ufichaji huo una lengo la kutafuna mali za wananchi kimya kimya na bila accountability.

Ukifika hapo ndipo unapoanza kuyakumbuka maneno ya ex PM Jean Chretien wa Canada 1992 aliyesema; " unapoona kiongozi anakuwa na midomo miwili ujue huo wa kushoto ni wake na huo wa kulia ni wa yule aliyempa Cheo.

Na huo wa kulia mara nyingi ndiyo unaochangia kuidhalilidha Serikali na huyo mwenyewe. Kwenye Serikali yangu nataka viongozi wenye mdomo mmoja mmoja tu." Ni kauli ya kitoto na ya kujidhalilisha.

My take
:
Sioni tija wala tofauti yoyoye ile iliyoletwa na hii serikali iliyojaa madokta na maprofesa na ni bora tu wangebaki au warudi vyuoni kufundisha.

Soma: Prof. Kabudi: Tanzanite One imefanya malipo ya awali, mazungumzo na Barrick yamefikia pazuri
 
Tumesema tokea muda mrefu ndani ya utawala huu wasomi watadharaulika ile mbaya. Sasa professor mzima anasema ukitangazwa kulipwa watu wanatokea kukudai. Huku TRA wanasema wanakusanya 1.3t@month na iko wazi na hakuna anayekuja kudai, lakini akisikia umelipwa chini ya 500b anakuja kukudai. Halafu kweli mtu anasema ukiwa msomi umejikwamua!!
 
Tumesema tokea muda mrefu ndani ya utawala huu wasomi watadharaulika ile mbaya. Sasa professor mzima anasema ukitangazwa kulipwa watu wanatokea kukudai. Huku TRA wanasema wanakusanya 1.3t@month na iko wazi na hakuna anayekuja kudai, lakini akisikia umelipwa chini ya 500b anakuja kukudai. Halafu kweli mtu anasema ukiwa msomi umejikwamua!!
Kwa mfano, unatarajia Barrick au Acacia wakakulipa alafu watachokulipa kikafanywa siri kwa wana hisa wao!!.

Kwa kifupi, huenda hakuna tunacholipwa au tunacholipwa ni aibu kukitamka hadharani na hivyo hii ni janja tu ya kuficha aibu hiyo.
 
Kuna mtu ananiambia nikachukue Ph.D....namuuliza Unataka niwe na Ph.D kwa sababu wengine wanayo au unafikiri nitakuwa nimeelimika zaidi?!

Neno pekee ninaloweza kumwambia huyu Prof. Kabudi ni "mpumbavu mwenye dharau".
Nilitaka kushangaa hili lipite bila kusemwa na Zitto
 
Kwa mfano, unatarajia Barrick au Acacia wakakulipa alafu watachokulipa kikafanywa siri kwa wana hisa wao!!.

Kwa kifupi, huenda hakuna tunacholipwa na hii ni janja tu ya kuficha aibu yao.

Uko sahihi kabisa, hakuna tunacholipwa, ili kuficha aibu ndio unaona watu wanaamua kuja na vioja. Jiulize toka $190b mpaka sijui $300b za goodwill. Halafu maelezo ya Kabudi baada ya lile sakata na sheria za madini hayakuwa yanaeleweka kabisa. Sasa kama prof anaeleza jambo muhimu la kitaifa haeleweki, hao watendaji wa std7 sio ndio itakuwa vurugu tupu?
 
Profesa akiingia kwenye siasa hugeuka kuwa Propesa!. angebaki huko vyuoni na kufanya tafiti na kufundisha watoto wetu badala ya kusimama na kutueleza mambo ya ajabu ajabu.
 
Wachumia tumbo wamejaa serikalini.

African mentality ni kwamba hupenda kuwachagua watu wasio na mapenzi na nchi yao na kuwadharau wenye mapenzi ya dhati na nchi yao. Hata wakati mwiingine huwa wanatamani kuwaondoa duniani.
 
Wachumia tumbo wamejaa serikalini.

African mentality ni kwamba hupenda kuwachagua watu wasio na mapenzi na nchi yao na kuwadharau wenye mapenzi ya dhati na nchi yao. Hata wakati mwiingine huwa wanatamani kuwaondoa duniani.
 
Back
Top Bottom