Zitto katika hili la Tigo Umenena

Bahati mbaya sikusikia swali wala jibu, Mdau! weka detail za swali & Jibu. Tumpepete Sitta hapa, wasituletee uzushi wao!Wakati majibu yoote yapo live!

Ishu ya Tigo na makampuni ya simu tunaijua, nje ndani walivyo tuibia haki yetu! Hadi kwenye sheria mbovu ya mawasiliano!!

Kinara wao ni yule Mgosi alikuwaga Katibu mkuu mawasiliano, Prof Nkoma, na advocate Mbuna - aliyefariki ambaye kijana wake, au binti yake wakoa kwa Mkapa.

Kaja Prof. Msola kataka kuyarekebisha madudu, makampuni ya simu yame lobby, na hawa hawa tanzania wenzetu mnao wakenulia kwenye Issa michuzi, mwishowe prof kapoteza uwaziri.

My take - Bravo Zitto,Prof Msola, and the like. Your job is seen - atleast by the few. Na hao kina Prof. Nkoma,Said Mrisho, na wenzenu, iko siku ntaonja chungu- tena ya uzeeni ni soo! Na kama mtakuwa mmekufa, tutawachukia wanenu, na makaburi yenu tutayachapa viboko - to set the History right! Labda mchome majivu.
 
Sio tarbia ya kiusaliti BALI ANAJIAMINI SANA KWA YALE ANAYOAMINI NI SAWA KWAKE.

Kijana mzuri sana na wangepatikana wabunge 15 wenye tarbia kama zake basi Tz mngekuwa pazuri sana. Kwani yeye si miongoni mwa wale wa kusubiri kulishwa.

Hongera Zitto

Barubaru umeibuka tena mkuu,
Ukisikia Zitto amaguswa ni sawa na kusikia cuf imeguswa, lazima utie neno.!!! Kumbe wabunge wenu wa cuf wanalishwa? kuku wa kisasa!!? Nadhani huko mbele ya safari utahamia chadema tu, kumkubali Zito ndio mwanzo wa safari yenyewe.
Hata mie nilishtuka! Barubaru ndani ya nyumba tena.
Kiukweli majibu mengi yanayotolewa bungeni ni mepesi mno! hayana uzito, mtu anajibu ili mradi tu!, tena wakina profesa maji marefu wakipiga makofi ndio bichwa linaongezeka ukubwa!
 
Zito ana uwezo mzuri sana Tatizo lake anadhani yuko pale kama yeye na si Chama na viongizi wenzake pamoja na wanachama. kwa ujumla ana katabia kausaliti sometimes.

kaka umeongea point nzuri sana tena kwa kifupi;hilo ndo tatizo kubwa la zito bt all in all jamaa ni smart sana
 
Waachieni wabunge wa CHADEMA waipiganie Tanzania. Kinachowakwaza ninyi ni nini? Au mnataka Watanzania wawe watumwa daima? Huo ukombozi unaodaiwa kuletwa na Serikali ya CCM (TANU?) mimi bado sijauona. Mpaka leo watu vijijini bado wanaishi kwenye nyumba za udongo, miaka hamsini ya Uhuru wa Tanganyika bado hali ile ile! Halafu wapo wanaosema kuna ukombozi? NYOOOO!
 
Back
Top Bottom