Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe ni kijana ambaye miaka ya 2015 nyuma ulikuwa ni miongoni mwa vijana mahiri na wenye kujenga hoja kweli kweli, binafsi mbali na kutokufuatilia Itikadi zenu za kivyama nilikupenda na kukuheshimu sana.
Hukuwahi kuwa na siasa za kushambulia utu wa mtu, ila ulikuwa na siasa za kushambulia hoja ya mtu, " politics of agenda not inhuman politics".
Nimesoma tweet yako, binafsi nimeumia sana, na niseme tu ningekuwa na uwezo nadhani ulikuwa ni wakati muafaka wa kuvunja katiba na kukushughulikia wewe mtu mmoja ambaye unahatarisha amani ya watanzania milioni 50 na kujenga taharuki kwa kutunga uongo.
Busara inaweza tumika kukuacha uendelee na maisha yako ila nakuhakikishia Kaka yangu na kijana mwenzangu dhambi hii haitokuacha salama kama sio leo basi kesho.
Umenukuu kifungu cha katiba 37 (2) ambacho kwa hakika ni dhihaka kubwa kwa kiongozi wa nchi.
Marekani wana Demokrasia ila hawafanyi hivi,
Uingereza wana Demokrasia ila hawafanyi hivi,
Urusi wana Demokrasia ila hawathubutu kufanya hivi.
Hapa Tanzania kuna nini watu wanavuka mipaka na kudhalilisha utu tena wa Kiongozi Mkuu wa nchi?
Uhuru gani wa kuongea tunaoutaka? Ni huu wa kudhihaki na kudhalilisha utu wa Viongozi tena Mkuu wa nchi.
Zitto umeteleza tena umeteleza sana, binafsi nimeumia sana ila bado naendelea kutafakari je ni wewe ninayekufahamu uliyepita mpaka nyumbani kwetu kuomba kura kwa akili zako unafanya haya ama wewe ni kitangulizi tu?
Zitto kama umeshindwa kumuheshimu Rais Magufuli kwa dhamana aliyonayo basi muheshimu kwa umri wake.
Naamini sana katika uhuru wa mawazo na demokrasia lakini si katika kuutumia kwa ajili ya kutweza utu, kuzusha, kutunga uongo au kujenga taharuki kwa maslahi binafsi ya kisiasa.
Daud Lukanya
Kigoma Ujiji.
Daudlukanya@gmail.com