Kama yawezekana kwa Balozi Mstaafu, basi hata Rais Mstaafu anaweza kuvuliwa hadhi yake

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,800
71,222
Tunaipongeza awamu hii ya Samia kwa kutufumbulia fumbo gumu.

Ametuonyesha kuwa kumbe utawala usipokukubali nawe ni mstaafu unakunyang'anya hadhi yako na kukukosesha stahili zako zote.

Baada ya Rais aliyoko sasa, utawala ujao itabidi nao ufuate nyayo hizi bila kupepesa macho kwa wastaafu wote viongozi kuanzia Marais waliopita, maspika hata na mawaziri pia.

Kama umefanya makosa ambayo ulikuwa unaambiwa kuwa hii sio sawa na ukaendelea kwa sababu madaraka uliyonayo huna wakukuwajibisha au ulilindwa na uchama kwa mfano issue ya mikataba ya gas, unyama kwa wamasai wa Ngorongoro na Loliondo, wizi na ubadhilifu nk.

Hata kama ulikuwa Rais, tutakuvua hadhi ya Urais mstaafu na kukunyima stahili zote kama hivi alivyo vuliwa Dr Slaa hadhi ya ubalozi.

Sheria lazima iwe msumeno kukata mbele na nyuma.
 
Ina nikumbusha Sheria ya Wamedi na Waajemi toka Maandiko Matakatifu, ambayo ikishawekwa kamwe haibadilishwi....

DANIELI 6: 8
"Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika"
 
Kwa ccm hakuna kinachoshindikana
Unajua kama wangekuwa wanajua kuwa ipo siku uovu wao wanaoitendea nchi hii wanaweza kuvuliwa hadhi na kunyimwa stahili zao wangeheshimu sheria na katiba.
Kosa la kuuza bandari, mbuga zetu, kutoa madini na gas kijingajinga ni makosa ambayo kuna nchi adhabu yake ni kitanzi.
Hebu tufikirie upya jinsi ya kuwashughulikia hawa.
Iweje uzunguke nchi nzima kuomba hiyo kazi tena sehemu nyingine unapiga kura na hatimaye bado unaiba na kura kisha ukiingia unajiona mwamba unafanya utakalo?
 
Tunaipongeza awamu hii ya Samia kwa kutufumbulia fumbo gumu.

Ametuonyesha kuwa kumbe utawala usipokukubali nawe ni mstaafu unakunyang'anya hadhi yako na kukukosesha stahili zako zote.

Baada ya Rais aliyoko sasa, utawala ujao itabidi nao ufuate nyayo hizi bila kupepesa macho kwa wastaafu wote viongozi kuanzia Marais waliopita, maspika hata na mawaziri pia.

Kama umefanya makosa ambayo ulikuwa unaambiwa kuwa hii sio sawa na ukaendelea kwa sababu madaraka uliyonayo huna wakukuwajibisha au ulilindwa na uchama kwa mfano issue ya mikataba ya gas, unyama kwa wamasai wa Ngorongoro na Loliondo, wizi na ubadhilifu nk.

Hata kama ulikuwa Rais, tutakuvua hadhi ya Urais mstaafu na kukunyima stahili zote kama hivi alivyo vuliwa Dr Slaa hadhi ya ubalozi.

Sheria lazima iwe msumeno kukata mbele na nyuma.
Kitu kimoja muhimu kitakachofanyika nchi hii mara baada ya kupata uongozi wa wenyenchi ni tume ya ukweli na maridhiano. Matokeo ya kazi ya tume hiyo siyo ajabu kupelekea watu kuvuliwa urais mstaafu!
 
Naiombea hiyo siku ifike haraka; msoga gang na s100 gang wavuliwe hadhi zao za ustafu na waliwe kitanzi hata wakikimbilia uarabuni watafuatwa huko huko.
 
... jeuri iko kwenye kinga ya kikatiba ya kutoshtakiwa hata baada ya kuacha madaraka.

Anyway, Katiba sio msahafu can be reviewed anytime. That's why by hooks and crooks lazima chama kishinde ili kuendelea kufaidi kinga ya maisha.
 
Back
Top Bottom