Zitto kabwe yuko tayari kuiokoa tanzania?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto kabwe yuko tayari kuiokoa tanzania??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Informer, Jun 17, 2010.

 1. T

  The Informer Senior Member

  #1
  Jun 17, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zitto Kabwe agombee ubunge jimbo la Igunga

  Ni ukweli usiofichika kuwa Mbunge wa Igunga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz, hujulikana na baadhi ya watu kuwa "The most powerful man in Tanzania" kuliko hata Rais wa nchi mwenyewe. Wengine pia humuita kuwa ni "Kingmaker" kwa kuwa yeye ndiye aliyefadhili mtandao mzima uliomuweka Rais Jakaya Kikwete madarakani mwaka 2005. By bankrolling Kikwete's presidential bid, Rostam ameibuka kuwa mwanasiasa/mfanyabiashara mwenye nguvu na influence kubwa sana kwenye CCM na serikalini.

  Ametumia ushawishi wake mkubwa wa kifisadi kuzidi kujilimbikizia mali kupitia kashfa mbalimbali ikiwemo EPA, Richmond, uagizaji mchele, pembejeo, n.k. Pia amekuwa akiwatisha maafisa serikalini kuwa ana nguvu kubwa za ku-influence uteuzi au kufukuzwa mtu serikalini.
  Amehusishwa na uteuzi wa mawaziri kadhaa na makatibu wakuu wa wizara nyeti, pamoja na viongozi wa mashirika makubwa ya serikali kama vile TANESCO na TANROADS.

  Mfanyabiashara huyu ambaye wala si mzawa, ana asili ya Iran na uraia wake una utata mkubwa ni "Mr. Untouchable."
  Tanzania is his little playground and he can do whatever he wants to whoever he wants.
  Inasemekana kuwa sasa hivi ameweka kando pesa za maangamizi (war chest) si chini ya shilingi bilioni 500 kuhakikisha kuwa Rais ajaye (2015) anakuwa puppet wake ili azidi kuchota pesa za Watanzania miaka kumi ijayo.
  Ameapa kuwa Wabunge wote wanaopiga kelele za ufisadi hawatarudi tena Bungeni baada ya uchaguzi wa 2010 na anamwaga pesa nyingi sana kuwaharibia mambo majimboni mwao.

  Sekretariat yote ya CCM iliyo chini ya Katibu Mkuu Yusuf Makamba inajulikana kuwa iko chini ya control ya Rostam. Jaribio kubwa la kumvua unachama wa CCM Spika wa Bunge, Samwel Sitta, kupitia NEC ni ishara nyingine za jinsi CCM nzima ilivyo mfukoni mwa mfanyabiashara huyu.
  Enough cannot be said about Rostam Aziz.

  Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ameonyesha tayari kuwa hana ushupavu wa uongozi (courage of leadership) kufanya maamuzi mazito. Hawezi kuwafukuza uanachama wa CCM Rostam na genge lake ili kurudisha umoja, mshikamano na heshima ya CCM.

  Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisema kweli. Bila CCM imara, nchi itayumba. Nchi sasa inayumba kwa kuwa CCM iko mfukoni mwa Rostam Aziz.

  Hapa ndipo tunamhitaji mwanasiasa mzalendo kutoka chama cha upinzani, Zitto Kabwe aiokoe nchi kwa kuiokoa CCM iondokane na Rostam Aziz.
  Katika historia ya nchi hii hajatokea mwanasiasa kuwa maarufu Bungeni kama alivyo Zitto hivi sasa.
  Yeye ndiye mwanasiasa pekee hapa Tanzania sasa hivi mwenye luxury ya kuamua akagombee jimbo gani hapa nchini na ana uhakika wa kushinda popote pale. Ndiyo maana tumesikia akisema anatafakari akagombee Kigoma tena, au Geita au Kinondoni.

  Ni ukweli usiopingika kuwa Zitto anaweza kwenda jimbo lolote la ubunge hapa nchini na kushinda (perhaps with the slight exception of CUF's stronghold in Pemba).
  Ninamuomba na kumsihi Zitto Kabwe akagombee Igunga ili kumng'oa Rostam Bungeni na kuiokoa Tanzania kutoka kwenye makucha ya sumu huyu.

  Kwa kwenda kupambana na kumng'oa ubunge Rostam, Zitto ataweza kufuta mashaka ya baadhi ya watu walioanza kuonyesha wasiwasi na msimamo wake na mwenendo wake. Kumtoa Rostam Bungeni ni hatua kubwa sana ya mwanzo wa kuikomboa Tanzania.
  Sote tumesikia watu wakianza kuhoji Zitto ana ubia gani na Rostam Aziz? Hii ilitokama na Zitto kuonekana kuunga mkono misimamo ya Rostam kama kutaka serikali inunue Dowans, jopo la majaji lichunguze Richmond, Dk. Idris Rashidi aendelee kuongoza TANESCO na kuonekana kumuunga mkono CEO wa TANROADS, Mrema, mwenye kashfa lukuki.

  This is a unique opportunity for Zitto to prove his doubters wrong and rescue the poor citizens of Tanzania from the clutches of colonialism under a subject of Iran, Rostam Aziz.

  Zitto Kabwe okoa Tanzania kwa kugombea ubunge Igunga 2010.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA!
   
 2. R

  Ramos JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa mawazo mazuri. nasikitika kuwa mapendekezo yako hayataweza kutatua tatizo ulilolielezea.

  Kivipi... Ukweli ni kuwa nguvu ya Rostam na hujuma anazofanya hazitegemei kwa namna yeyote kuwa yupo bungeni au la. Hazitegemei kuwa ni maarufu kwa 'watanzania' au la, zinategemea kuwa yeye ndiye aliyebeba silaha ya mwisho na ya maangamizi ya CCM dhidi ya haki na usawa; FEDHA. Kama utapitia kumbukumbu za bunge (kwenye website yao) utaona kuwa kwa kipindi cha miaka karibia mitano tangia bunge hili lilipoanza, Rostam hajauliza swali la msingi, la nyongeza wala kutoa ama kuchangia hoja yeyote bungeni; lakini atarudi bungeni kwa kishindo (akitaka). Thats POWER OF MONEY.

  Kwa hiyo Zito hata asipoteze muda wake kwenda kumng'oa Rostam...
   
 3. Mpenda Kwao

  Mpenda Kwao Senior Member

  #3
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Je ni kweli kwamba Rostam aking'olewa bungeni ndio mwisho wa ucurlprit wao? Si anaweza kuwa nje ya bunge na bado akaendeleza matakwa yake kupitia vibaraka ambao wapo wengi tu? Just to mention few Serukamba, Makamba, Nchimbi Karamagi, Chenge na wengine kibao tu?
   
Loading...