Zitto Kabwe wapiga kura wako wananyanyaswa

rusesa

JF-Expert Member
Jun 1, 2013
538
233
Habari wanaJF,

Wananchi katika jumbo la Kigoma mjini walio jiajiri wenyewe kwa kuchota maji kutoka chemichemi za mto Lutare wameanza kutozwa kodi ya kuchota maji katika chemichemi hizo.

Miaka nenda rudi wachota maji hao wamekuwa wakisambaza maji hayo yanayoaminika na wakazi wakigoma mjini kwa kwa shilingi 500 tu. Ikumbukwe Kigoma mjini kuna tatizo la maji baadhi ya maeneo., mfano Masanga, Mlole na kwingineko.

Kodi hii imesababisha dumu la maji kuuzwa mpaka Tsh. 800 hadi 1000. Kodi hii inatozwa na mkurugenzi was manispaa ya Kigomaa mjini kushirikiana na madiwani na vitongoji waeneo husika.

Zitto njoo uwatetee wachota maji hawa hivi wewe uko upo wapi? wananchi wanakulilia bila mafanikio.

Wanahoji je chemichemi hizi za maji zinahudumiwa na serikari? je kodi hii inaenda wapi? nakwanini imeanza sasa na sio zamani?

Zitto wapiga kura wako wanakulilia huku.

Siku njema!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom